Zanzibar kupo ovyo sana. Kweli au nahitaji kueleweshwa?

Mimi nilienda huko nikapanda daladala namcheck konda eti kapaka uwanja aah..sikumweka nikamuuliza ...eti ananiambia ni sunah hiyo ...eeh nikabaki nashanga hawa watu wanaishi maisha ya Karne gani sijui .
Lakini hukushangaa makondakta wanaovaa hereni huko gongo la mboto??
 
Mtoa mada unamatatizo sio bure watu wenye wadhifa wao, utajiri na wafanyabiashara na mashuhuri wanaipenda Zanzibar ni sehemu moja iko kipekee kabisa kama una hela za kutumia nenda Zanzibar Tembelea stone town na uinjoy hotel za kifahari.

inasemekana Zanzibar ni sehemu pekee ukienda msikitini unaweza kuonana na waziri, wabunge , Rpc na ukapiga swaga nao bila shida yoyote ufahari, majivuno hawana wanaishi maisha yakawaida kabisa.
Thats the beauty of Zanzibar
 
Ila Serikali yao inawapenda sana, huduma zote zinazotolewa na Serikali kama Elimu,Afya Umeme,Maji na n.k. aidha ni bure ama kwa gharama ya chini kabisa, hakuna magereza, badala yake kuna vyuo vya Mafunzo na humo ndani ya hivyo vyuo kunapatikana michezo ya kila aina, "mpira wa miguu,basketball,netball,Keram, draft na michezo mingine tele na anaemaliza kifungo chake kuna pesa ya kwenda kuanzia maisha huwa anapewa. Wenyewe wanaita "mshahara"yaani kipindi chote unachokaa jela unakuwa unalipwa.
Na kuna watu wanatoka Tanzania bara na kuja Zanzibar kupatiwa matibabu tu hapo Mnazi mmoja hospital
 
Nimetembelea huu mji, kwa kweli ni mji ambao bado watu wamelala, migahawa ya kumulika kwa tochi vyakula havieleweki, nimeenda hadi forodhani yaani nyama za pale bei juu alafu hazina mvuto yaani rafu rafu tu.

Barabara za lami kama wamemwaga zege yaani, mainjinia sijui wameajiriwa kwa kazi gani, nimehisi nimerudi Dar es Salaam ya mwaka 2000 or ndio mji wa kitalii labda.

Labda nipewe chimbo huenda nimeenda sehemu sio lakini kwaweli ni majanga sana hapa.
Umefika chamba wima? nasikia pako doro sana.

Tembelea na kiembe ladu,
Mfereji maringo..
Kiembe samaki.
 
Nimetembelea huu mji, kwa kweli ni mji ambao bado watu wamelala, migahawa ya kumulika kwa tochi vyakula havieleweki, nimeenda hadi forodhani yaani nyama za pale bei juu alafu hazina mvuto yaani rafu rafu tu.

Barabara za lami kama wamemwaga zege yaani, mainjinia sijui wameajiriwa kwa kazi gani, nimehisi nimerudi Dar es Salaam ya mwaka 2000 or ndio mji wa kitalii labda.

Labda nipewe chimbo huenda nimeenda sehemu sio lakini kwaweli ni majanga sana hapa.

Zanzibar mnatakiwa mbadilike mainjinia sijui mnafanya kazi gani mnashindwa kulipendezesha jiji yaani lami kama zimemwagwa zege hovyo hovyo miji ni michafu hatari. Kuwa jiji la kitalii haimaanishi muwe hivyo pendezesheni mji wenu wekeni pawe pasafi kama moshi, tengenezeni lami za kiaasa kama dar pawe pazuri

Plan ya miji iwe kila sehem na migahawa miuzuri na pasafi,

Shida kubwa inayokusumbua huna peda na umefkia sehem za hovyo na unalala pa hovyo na huezi tembea sehem za mana sabbu huna pesa tafuta tax driver wako akutembeze unakotaka na forodhan kale mule kwenye jengo la fish market kalale serena hotel tembo park Hyatt na Kama unataka miji iliopangika mwmbie akuplke huna pesa halafu unalia Lia tafuta pesa uende sehemu za kula bata unalolitaka Zanzibar ni mji wa kitalii huezi pata kila kitu kwa bei rahic kuhusu barabara ni kweli za mjini karbu zote ni za tangu enzi za karume ila zipo sehem zenye road mpya na pana Kama unazunguka stone town tu huo ni mji wa kitalii na hauruhusiwi kujengwa vyengne tafuta pesa mzee
 
Huwa nakwenda Unguja kufuata yale mazingira sometimes kichwa kikishika moto.Mazingira fulani amazing!yanafanana na Dar ya zamani iliyokuwa tulivu.Vile vimtaa kama Casablanca!Upepo na utulivu.Maisha ya uswahili ule wa zamani,wenye ukarimu na mvuto wa kipekee kwa wageni.Wenyeji walio honest!Zanzibar iacheni hivyo hivyo pamoja na watu wake!Wengine tunaona adventure kwenda mazingira hayo!Embu waacheni wazenji wetu.Kama mnataka skyscrapers si muende Nairobi ma Dubai....labda hilo la misosi ndio walirekebishe maana lina ukweli ingawa some of us tunatazama kwa jicho la fursa.Kule hata nyumbani sometimes wavivu kupika so ukiweka mgahawa ukawa na taste na ukauza bei za kawaida utatapika hela!fursa hiyo nimewamegeeni!

Migahawa Zanzibar sio mengi kwasabbu asilimia kubwa ya wazawa wanapika chakula nyumban sabbu ya familia kuwa kubwa wanunuaji sio wengi sana na mama ntilie wachache sana ucku sana watu ndio wanannua chakula kama tu chakula cha mchana kimemlza ndio panannuliwa cha rahic kama mikate chips sehem za mjini za kula kubwa nenda kwa lukman kwa bavuwai Kuna Hadi ugali mnaoupenda vingi mno unachagua nini unapenda ila bill yake sio chini ya elf8
 
Usikimbie hoja jibu hoja..kama ilivyokuja..mbona mnatesa na kutenga waswahili wenzenu ila wazungu mnawanyenyekea na kuwapa huduma ya chakula kipindi cha mfungo?

Dini..umaskini na ujinga ni tatizo kubwa sana kwa waafrika hasa jamii kama zenu.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app

Hii ndiyo hoja uliyoleta ambayo umeunganisha dini na uzungu, vitu viwili ambavyo havina uhusiano:

"Dini ya mudi umewabrainwash wapo kama mazezeta na misukule..wanamuona mzungu kama Mungu..ila mwafrika mwenzao wanamtenga..si upuuzi huu".

inferiority complex ndiyo inakusumbua wewe.
 
Masikini roho yakooooo! Hivi umetokea mikoani huko (tunaita madongo poromoka) umefika Dar ndiyo unajiona uko more civilized than Zanzibaris?

Penye ukweli lazima tuzungumze, Tatizo kubwa la wazanzibari ni Uncivilized, na kubwa Zaidi ni watu ambao ni wagumu sana kubadilika.
Ni kweli mtu anaweza toka mikowani akaja Dar akiwa kiza kabisa lakini with time anabadilika kidogo kidogo, ILa wazanzibar ni shida kwa kweli, unaweza kumkuta Mmkunduchi anaishi Unguja Mjini Zaidi ya miaka 20 ila bado utafikiri bado yupo Makunduchi lifestyle yake.
 
Tatizo wanapenda kufuga majini kila nyumba kuna fugwa jini, kingine wanahamin Sana ushirikina utakuta Mume hajaonekana nyumban siku mbili mke anaenda Kwa mganga ili amsaidie, baadala aende kutoa taarifa polisi na kwenda hospital kumtafuta , chakushangaza wanaenda kwa waganga.
Dah
 
Back
Top Bottom