Zanzibar itakufa kama Tanzania ikifa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar itakufa kama Tanzania ikifa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Semilong, Apr 4, 2009.

 1. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hali ya kisiasa ya zanzibar ilivyo sasa hivi ni kama burundi au rwanda.
  Zanzibar hakuna upinzani wa kisiasa bali kuna ukabila. Waunguja wanapigia kura ccm na wapemba cuf.

  Kwa mantiki hiyo ninaamini kwamba endapo muungano utavunjika na ikarudi kuwa tanganyika na zanzibar, miezi mitatu ya mwanzo itakuwa ni furaha kwa wazanzibar kwa ajili wamekua na nchi yao wenyewe, halafu machafuko yataanza pale uchaguzi wa kumteua rais wa zanzibar utakapoanza. Wapemba watapigia kura cuf na waunguja ccm(asp) na hapo ndio zanzibar itakapopasuka na unguja kuwa nchi na pemba kuwa nchi na rais wake sshamad. Wapemba hatakubali rais awe muunguja kwa ajili imekua hivyo siku nyingi sana na waunguja wanaamini kwamba wapemba ni wabaguzi watawabagua sana.

  mambo yote haya yatatokea katika kipindi cha mwaka mmoja.

  fact: Uk kuna wazanzibari wengi lakini wamegawanyika katika makundi mawili wapemba na waunguja. Waunguja wapo karibu na watu wa bara na wapemba wako wenyewe. Pamoja na kuja ulaya bado wameshidwa kuwa ndugu. Kama wakikuyu na wajaluo uk  Athari za kuvunjika kwa muungano
  1.wa bara waliokuwa zanzibar wataambiwa warudi kwao na wengine hata kupoteza maisha yao. (hawako wengi)

  2. Wapemba ambao wanamaduka bara itabidi wayafunge na warudi kwao, sijui pemba ilivyokuwa ndogo watamuuzia nani vitu.

  3.wazazibari wenye magorofa kariakoo itabidi wayaache na warudi kwao. Hata mzee mwinyi itabidi aondoke aliache lile gorofa lake msasani na white sands hotel.

  4. Kwa sisi tuliooa zanzibar itabidi wake/waume zetu warudi zanzibar na watoto wabakie bara (kitu kibaya sana hichi).

  5. Wakati mamboa yote haya ya kiendelea wananchi wakitaabika viongozi watakua wanagawana madaraka. Je wazanzibari mmefikiria au ni kufuata mkumbo wa viongozi

  mkoa wa kinondoni una watu zaidi ya zanzibar nzima.
  Solution: Kuwa na serikali moja rais mmoja na pemba na unguja kuwa mikoa yenye ma mayor ambao watapigiwa kura na wananchi.
   
 2. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kila mtu ana mtizamo wake katika mambo haya. Siwezi kubeza wako kama ni finyu. Kuna vitu umeeleza ni vizuri tu kwa tahadhari. Lakini wacha nikueleze na nikutoe wasiwasi kuwa Zanzibar kamwe haiwezi kugeuka Burundi au Ruwanda. Wewe hujafika huko Zanzibar kwenyewe na ukaona hao watu wanaoelezwa kuwa wana tofauti- kwa kiasi gani wanakaa pamoja na kufanya mambo yao pamoja pale (kwa mfano Mjini Zanzibar?) Nenda kaishi kule utaona. Hizo kasumba za Seif na CUF yake na Retaliation za CCM -Zanzibar (specifically against Seif and his staunch followers) ndizo zinazokuzonga hapo. Hayo ni mambo ya mpito. Hao watapata solution. But Iam telling u those who call themselves Zanzibaris are very strong and united.
   
 3. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145

  they are united when it comes to muungano(tz) ISSUES, but not united when it comes to zanzibar alone.

  THE WAY PEOPLE VOTE IN ZANZIBAR IS SHOCKING......
   
 4. _SiDe_

  _SiDe_ Member

  #4
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 89
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Semilong hiyo ni imani yako (unavyoamini wewe) kuwa Zanzibar itakufa lakini asilimia kubwa ya Wazanzibar wenyewe wanaamini nchi yao inakufa ndani ya Tanzania (mimi mmojawao). Kutokana na aina ya Muungano uliopo sasa.
  ZANZIBAR IPO KABLA YA TANZANIA, SO WACHA TANZANIA IFE NA ZANZIBAR ITABAKI PALEPALE.
  Na wasiwasi statement yako imetoka kitengo cha propaganda, chini ya Makamba na Tambwe.
  Mkitaka serikali tatu, hamkutaka basi! lakini moja never.
   
 5. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  mimi sio mwana ccm na wala siwa support makamba na tambwe nipo uk kwa mda mrefu na haya ninayokuambia yako sasa hivi hapa uk.

  Binafsi nina imani kuwa tz ya rais mmoja ndio nchi, lakini ccm na cuf kutokana na ulafi wa madaraka wanataka iwe kama ilivyo.

  Embu angalia
  1. Rais wa jamuuri ya muungano
  2. Rais wa zanzibar
  3.makamu wa rais
  4. Waziri mkuu
  5. Waziri wa mambo ya zanzibar
  hii ni kupoteza pesa za walipa kodi
  ilitakiwa iwe rais na makamu hivyo vyeo vingine vyote vife.
   
 6. _SiDe_

  _SiDe_ Member

  #6
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 89
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  "Solution: Kuwa na serikali moja rais mmoja na pemba na unguja kuwa mikoa yenye ma mayor ambao watapigiwa kura na wananchi."

  Ndoto za mchana! just endelea tu kuota.
  Mara nyingi mnasema Zanzibar mzigo kwenye Muungano, lakini ni nyinyi mnaolazimisha huu Muungano uwepo.
  Mbona husemi solution Zanzibar wawe kivyao! ili mzigo uondoke?
  Enewei mnaficha maradhi, lakini kifo kitakuumbueni.
   
 7. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #7
  Apr 4, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
   
 8. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  CCM ndio wanaoiharibu Zanziba toka tulipoungana nao. Wao ndio wamekuwa mstari wa mbele kuwabagua wapemba. Hata ukiangalia marais wote wa Zanziba ni wa kutoka Unguja.

  Kuhusu kusema kuwa CUF hushinda Pemba na CCM Unguja, kwa Pemba kweli ni CUF tu ndio hushinda, lakini Unguja CUF wana wanachama, tena sio wachache. Kumbuka uchaguzi wa 1995 CUF walipata majimbo mangapi Unguja. Baada ya ule uchaguzi, CCM wakaongeza majimbo Unguja, na yaliyoongezwa ni sehemu zile zilizokuwa na wafuasi wengi wa CCM. Pia unaposema CUF haipati kura Unguja, wakati chaguzi zote huwa wanashinda na kuibiwa kura. Uchaguzi wenye ushahidi kabisa ni wa 1995 kuwa CUF walishinda, sasa huwezi sema kuwa CUF haina wafuasi Unguja. Hizo ni mbinu za CCM kuidhoofisha CUF ionekane Unguja haina wafuasi.
   
 9. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #9
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  kuna wapemba unguja na ndio wanaopigia cuf kura lakini hamna waunguja pemba
   
 10. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #10
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  "Nje ya Muungano ninyi si wamoja... Dhambi ya ubaguzi itawatafuna"-JK Nyerere
   
 11. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2009
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Dada semilong inaonesha dhahiri wazanzibar wa mekutenda kwa ujumla na hizo hasira zako umehisi kumalizia kwa kuashiria shari ya mauwaji baina ya ndugu hao hapa kwetu visiwani ZANZIBAR TUNA msemo unaosema mchimba kisima hungia mwenyewe na dalili za mvuwa ni mawingu na yameshaanza kutanda huko kwenu TANGANYIKA
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Apr 4, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Tanzania bila ya Tanganyika ni wizi mtupu ,stand for Tanganyika and becomes free from mawazo finyu ,vurugu zote ni kuwa uongoziwa Salatani CCM haupendi kuona waZanzibari wanasikilizana,uongozi huu wa salatani CCM ni mbovu kiuongozi na ni shupavu kwa wizi wa mali na hazina ya Taifa hili ,Uongozi wa Salatani CCM haupendi kuona Katiba ya Nchi hii inafundwa upya ili kukidhi mahitaji ya mkondo mpya wa siasa za Vyama vingi ,ubaguzi unaondoka ikiwa vilingo vya elimu vitazingatiwa ,hivyo nafasi yeyote itachukuliwa na yule ambae analingana na elimu ya sehemu hiyo husika ,hii hupatikana kwa njia ya Interview ,lakini leo nafasi za kazi chini ya uongozi wa Sultani CCM hutolewa kwa mjomba na shangazi.
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Naomba unipe darsa ndugu yagu. Hivi kati ya Wazanzibari na Watanganyika ni nani anachimba kisima?
   
 14. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Inaweza kuzaliwa Zanzibar mpya. Mfano wanaweza kuunda selikari yao ya Muungano wa visiwa vya Pemba na Unguja. Selikari ya Pemba na Selikari ya unguja zikishughulika na mabo yao ya ndani na Selikari ya Muungano ikishughulikia mambo ya Muungano wao.

  Pia maridhiano yanaweza kufanyika kwa raia watakaoamua kubaki kwa hiari yao katika sehemu mojawapo zilizokuwa zinaunda muungano uliovunjika. Tutakapoamua kutumia Busara au Jazba kakika kuvunja muungano ndivyo vitakavyoamu yale yatakayotokea siku ya kuvunjika kwa muungano. Montenegro walipiga kura kujitoa kwenye Muungano na Serbia, Serbia kwa shingo upande wakaamua kuwaruhusu lakini hawakuchukua hatua za kuwafukuza wamontenegro waliokuwa wanaishi serbia. Sana sana Serbia ilitafuta njia nyingine ya kuimarisha mahusiano na Montenegro na si kuendeleza uhasama. Hivyo hata kwa Tanganyika na Zanzibar kuna mambo mengi tunaweza kufaidishana baada kama muungano wetu tutauvunja kwa kufuata taratibu zinazotakiwa badala ya kutumia jazba, kujenga uhasama, n.k
   
 15. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #15
  Apr 4, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nadhani Semilog umejibu kitaalamu hili. Na wapemba wanaokuwepo Unguja katika jimbo lolote lile hawawezi kushinda uwingi wa wa_Unguja waliopo katika jimbo hilo- Ndiyo maana wanashindwa Unguja. Lakini hii hali siyo nzuri Kwa nini watu wapige kura on this basis. Walioasisi mtizamo huo walikuwa na tamaa zao. Sisi kwa nini tunatumbukia huko. Ndiyo maana nasema kule Zanzibar tuachane na CUF , tuachane na CCM, tuachane na kumbukumbu za tuliowazika za ASP na Hizbu. Tuanze upya . tuanzishe vyama vyetu pale Zanzibar( ni kwa ajili ya Zanzibar tu-tupige siasa ) na tuingie katika kura kutafuta Rais na Wawakilishi.Bara hawamo na hawahusiki kwa lolote lile.
   
 16. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #16
  Apr 5, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  NINGEKUULIZA SWALI MOJA HALAFU UKISHAJIBU TUENDELEE NA MJADALA.

  Umewahi kufika Zanzibar. na kama umefanya hivyo umekaa kwa muda gani?
   
 17. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #17
  Apr 5, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  KUMBE !!! Sasa siwezi kushangaa ............!
   
 18. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #18
  Apr 5, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
   
 19. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Naam suala la Muungano ni suala la Wazanzibari wote kama vile mnapoweka mbali nyie tofauti za CCM na CHADEMA dhidi ya Zanzibar.
  Ukija suala la uchaguzi ni suala la Demokrasia na namna chama kinavyokubalika kutokana na sera zake pahala husika. CCM haijajiuza vizuri kwa kule Pemba lakini Unguja wanafanya jitihada za kujiuza sawa na CUF ni Chama ambacho viongozi wake wengi ni kutoka huko na lengo lao la kuona kuwa na Pemba nayo inafaidika ndio inawafanya kutakiwa Pemba. Hapa panataka Digirii ya Mlimani kufahamu hivyo?
  Tofauti za Kidemokrasia si ukabila na kama ni Ukabila basi Tanganyika ni Wakabila wakubwa kwani hamuikubali CUF. Pia Zanzibar vyama vikuu ni viwili tu kwa maana yenu kuna makabila mawili na huku Bara kuna vyama vyenye nguvu zaidi ya vinne je ina maana kuwa bara kuna ukabila Zaidi?
   
 20. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #20
  Apr 5, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135

  Tarime, Buzwagi, Mererani, Mbulu na Mauwaji ya Albino ni baadhi tu ya sehemu zenye visima hivyo.
   
Loading...