liljeff87
Senior Member
- Jan 3, 2016
- 174
- 85
ZANZIBAR ILIVYOFISIDIWA HADI KUTISHIWA KUKATIWA UMEME
Katika mwaka 1884 Sultan wa zanzibar Sayyid said walitiliana mkataba wa kibiashara na Marekani.
Wakati huo Zanzibar ilikuwa ni Nchi ya mwanzo kutumia Nishati ya umemr katika nchi za Afrika Mashariki ambapo Zanzibar ilikuwa inazalisha Umeme wake kupitia kinu cha Taa ambacho kilipatikana kwa mahusiano ya Zanzibar na marekani.
Uingereza ilikuwa bado inatumia Gesi, kinu cha Taa hicho ambacho kilikuwa eneo la Malindi kiliiwezesha Zanzibar kutokuwa tegemezi katika Nishani hiyo.
Pia ikawa ndio chachu ya Nchi za Bara kupata umeme mpaka Nchi za Afrika ya kati kama vile Congo.
Bwana Abdurahman Babu akiandika utangulizi kuhusu yaliyopita katika mapinduzi ya zanzibar ndani ya kitabu kiitwacho "SIKU 100 ZA KUUNDWA MUUNGANO WA TANZANIA UHASIDI WA MAREKANI KWA MAPINDUZI YA ZANZIBAR" anazungumzia maendeleo ya zanzibar siku za mwanzo ikishirikiana na marekani.
"Wamarekani walijenga kinu cha lifti ya kwanza ya umeme katika Afrika mashariki. Pia Marekani iliiwezesha Zanzibar kufaidi kuwa na Taa za Barabarani mapema mno kuliko hata london ambayo london wakati huo bado inatumia Taa za Gesi".
Si hivyo tu bali kutoka zanzibar mitambo ya simu iliyosambazwa kutoka Aden kwenda London Uingereza kuja Zanzibar.
Kadhalika Mitambo hiyo ilitoka Zanzibar kwenda Bagamoyo leo utaona athar za hayo hapo tunapopaita 'Welesi' ilikuwa Mitambo ya 'Wireless" iliyokuwa ikisafirisha mawasiliano kutoka Unguja kwenda Bagamoyo, Rwanda, Barundi, Uganda mpaka Koñgo. Kadhalika kutoka Unguja kwenda Aden mpaka Uingereza.
Ndio tunasema Zanzibar ni ya Mwanzo kutandaza waya za simu "Wireless" na ikawa ndio ya mwanzo kutumia Lift ya Umeme katika Ghorofa la Baytul Ajaaib.
Ni vijana wangapi leo hii wanaojua kwamba Mji wa Zanzibar ulikuwa wa mwanzo kuwasha Taa za umeme Barabarani na Mitaani zikiitwa 'Taa za Stimu' kabla ya London na New york?
Aliyekuwa Balozi wa Marekani Nchi, wakati anamaliza muda wake, Bwana Mark Green, wakati akitoa khutuba yake ya kuaga alisema
"Meli za Marekani zilikuwa zikitia Nanga katika Bandari ya Zanzibar kuja kununua Mafuta ya Nyangumi kwa ajili ya kwenda kuwashia Taa zao za Barabarani wakati Zanzibar inatumia Umeme".
Swali la kujiuliza haya yote yamekwenda wapi na kwa nini Zanzibar hivi sasa inashindwa kujitegemea na kuzalisha umeme wake kuliko kutegemea Nishati hiyo Tanzania Bara?
Leo Zanzibar inategemea kampuni kibao za Simu zenye makao yake makuu Tanzania Bara
nini kimeisibu Zanzibar ishindwe kusimama kwa miguu yake miwili?
(Marejeo ya makala hii tazama katika vitabu vyangu viwili DOLA KOMGWE YA ZANZIBAR KUTOKA OMAN HADI KONGO na UTUKUFU WA ZANZIBAR )