Zanzibar I Knew

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,790
Mwandishi mashuhuri wa Uingereza aliitembelea Zanzibar kabla ya Mapindizu matukufu ya 1964, alivutiwa sana na maisha na desturi za wazanzibari mbali na uzuri na mandhari za kimaumbile ya nchi yao. Aliporudi England aliandika kitabu mahsusi kuhusu Zanzibar kama ishara ya kumbukumbu kwake na wale ambao hawajawahi kutalii visiwa hivi.

Alipotaka kukizinduwa kitabu kwenye miaka 1968 aliona bora aifanyie kazi hiyo hapa Zanzibar. Lakini mshituko alioupata kuiona Zanzibar kuwa " upside down country" aliahirisha uzinduzi.Alirudi kwao na kulazimika kubadili jina la kitabu na kukiita Zanzibar I knew

Siti binti Saad , msanii wa kizanzibari mashuhuri wa wakati wote,aliwahi kuimba wimbo maarufu " Zanzibar ni njema atakae aje" . Nyimbo ambayo imenogeshwa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwa kuongezea maneno "...lakini usije kufanya fujo...."

lakini kwa bahati mbaya sana. WAKUJA waliyachukua maneno ya mwisho na kukivamia kisiwa kuleta mfarakano
1. Zanzibar iliozoeleka kuwaona watu wakibarizi baada ya kazi kwa kucheza bao na kunywa Kahawa na visheti, leo haipo tena kuna mazombi na vikosi maalum vy kumahanisha watu

2. Zanzibar iliozoeleka kuwaona watu wakicheza karata saas za usiku, leo haipo tena

3.Zanzibar iliozoeleka kuwaona watu wamejipumzisha nje ya baraza za nyumba zao na kucheza na watoto wao , leo haipo tena

4.Zanzibar iliozoeleka kuwaona watu kukusanyika usiku kula chips na urojo, leo haipo tena

Zanzibar imekuwa " upside down country". Tumepokonywa uhuru wetu. Tumepokonywa Mamlaka yetu.Tumepokonywa haki ya kuchagua viongozi tuwatakao. Tumepokonywa hata ile ya haki ya msingi kutembea.

Zanzibar I knew is no more Zanzibar I know ni Mazombie tu
 
Tatizo ni laana ya toka enzi.
Ardhi ya Zanzibar ina Damu isiyo na hatia inayolia.
 
Back
Top Bottom