Hivi najiuliza hali hii ya Zanzibar hadi lini mbona sielewi..
maana hakuna Raisi wala waziri na wananchi wapo njia panda hadi hii leo hawajui kama utakuwepo uchaguzi au haupo..
kama upo kwa sheria gani zinasema na kama haupo kipi kinachofata..
nawasilisha kijihoja
Solution ya Zanzibar ni so simple.
Uchaguzi ulifanyika tarehe 25/10/2015 kwa amani na utulivu.
Waangalizi wote wa ndani na nje ya nchi wakatoa taarifa zao za tathmini ya uchaguzi huo na kuuita kuwa ulikuwa huru na haki.
Mawakala wa vyama vyote vilivyoshiriki uchaguzi huo wakasaini fomu za matokeo hayo na hata washindi wa baraza la wawakilishi wamekabidhiwa vyeti vyao vya ushindi.
Mwenyekiti akaanza kutangaza matokeo ya Urais na baraza la wawakilishi kwenye majimbo mbalimbali hadi yakafikia 34 kati ya majimbo 51 ya Unguja na Pemba.
Ghafla siku ya 3 ya matangazo ya tarehe 28/10/2015 kwa mshangao mkubwa, ndipo tangazo la Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Zanzibar Jecha Salim Jecha, linasomwa kupitia ZBC tena likiwa recorded, akieleza kuufuta uchaguzi huo kwa mamlaka aliyodai anayo, lakini bila kutaja kifungu chochote cha sheria kinachompa mamlaka hayo.
Ni dhahiri kwa mlolongo huo wa mchakato wa uchaguzi Zanzibar ulivyokwenda, naweza kuthubutu kwa kusema kuwa tamko la Jecha ni batili na halina nguvu kisheria, unless serikali ya CCM itake tu kulazimisha na kuamua kulihalalisha tamko hilo la kibabe.
Kwa hiyo solution pekee kwa maslahi mapana ya Zanzibar na Taifa la Tanzania kwa ujumla wake, ni kwa Tume ya uchaguzi Zanzibar kumalizia 'kiporo' cha kutangaza matokeo ya majimbo 17 yaiyokuwa yamesalia na hatimaye kumtangaza mshindi aliyeshinda kiti cha Urais Zanzibar.
Njia nyingine zozote ambazo watawala watataka kuyakataa matakwa ya wananchi na badala yake kutaka wao ndiyo wang'ang'anie madarakani hata kwa kudiriki kuivunja Katiba ya nchi waliyoapa kuilinda, hakika uchu huo wa madaraka wa watawala wetu unaweza kulitumbukiza Taifa hili kwenye machafuko makubwa.