VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Rais wa Zanzibar,Dr. Ali Mohamed Shein amekwama katika kumteua Makamu wa Kwanza wa Rais wa Visiwani humo. Kikatiba,Makamu wa Kwanza wa Rais anapaswa kupendekezwa na chama chake na kuteuliwa na Rais.
Chama kinachopasa kumpendekeza Makamu wa Kwanza wa Rais ni kile kilichokamata nafasi ya pili uchaguzini na kupata asilimia zisizopungua kumi ya kura zote. Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi,hakuna chama hata kimoja cha upinzani chenye sifa za kumpendekeza mteuliwa wa Makamu wa Kwanza wa Rais.
Siku saba za kikatiba,baada ya kuapishwa kwa Rais,zinaisha leo. Kuanzia leo kutakuwa na mkwamo mpya wa kikatiba na kisiasa Zanzibar. Kwanza,Serikali ya Umoja wa Kitaifa haitaundika kwakuwa hakuna chama cha upinzani chenye sifa za kumtoa Makamu wa Kwanza wa Rais au kushiriki kuunda SUK kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar. Na pili,kukosekana kwa Makamu wa Kwanza wa Rais ni kutotekelezwa masharti ya Katiba.
Dr. Shein yuko njiapanda!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam