VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Sasa ni dhahiri kuwa CUF hawatashiriki uchaguzi wa marejeo wa Jumapili ingawa majina ya magombea wao yatakuwemo kwenye karatasi za kupigia kura. ZEC ya Jecha ilishasema kuwa hakuna mgombea aliyejitoa kisheria.
Dodosa zangu za hapa Unguja na kule Pemba zinaonesha kuwa CUF hawatashiriki katika uchaguzi huo,ikiwa ni pamoja na kutotuma mawakala wakati na baada ya kupigwa kura. CUF pia imewasihi Wajumbe wa ZEC wanaotokana na chama hicho kujiweka mbali na uchaguzi wa marejeo.
Wakati huo huo,CCM imejipanga kila idara kushiriki uchaguzi wa Jumapili. Imesema kuwa haitishwi na maneno kuwa uchaguzi huo ni wa maruhani na kwamba watajichagua wenyewe kwenye maonesho ya mazingaombwe ya Jumapili. CCM ni mbele kwa mbele!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Unguja,Zanzibar)