Zambia, Senegal wameweza, Tanzania tunaweza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zambia, Senegal wameweza, Tanzania tunaweza!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbelwa Germano, Mar 27, 2012.

 1. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kuwa Mwanachama au Kiongozi wa chama cha upinzani nchini ni KAZI. Lazima ukidhi vigezo vikuu vitatu:

  1. UJASIRI
  2. UVUMILIVU na
  3. UMAKINI


  • Bila ujasiri huwezi kukabiliana dhulma katika jamii
  • Bila uvumilivu huwezi kukabiliana na changamoto za kisiasa katika jamii
  • Bila umakini haraka unapoteza ujasiri


  Tumeona ni jinsi gani viongozi waliokosa baadhi au sifa zote (kutoka vyama vya upinzani) nilizotaja hapo juu walivyoweza kudhoofisha upinzani nchini. Wapo Augustine Mrema (Uvumilivu na Umakini), Dr. Kaborou n.k.

  Makamanda wa CDM wamekuwa mstari wa mbele katika kufungua darasa jipya kwa watanzania, darasa lenye hoja dhabiti za kufungua mirija ya ufahamu wa Watanzania, kuyeyusha fikra mgando na hatimaye kupata mapambazuko ya kisiasa ndani ya Taifa letu. Bila ujasiri wa Mh. Mbowe, Dr.Slaa, Zitto Kabwe, Halima Mdee na makamanda wengine waliokuwapo kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 wananchi wa Tanzania tulikuwa tumefungwa kwenye wingu zito tusioona nyuma wala mbele na kusahau ule wajibu tulio nao wa kufikiri kwa bidii.

  Wakati wa Mwl. Julius Nyerere ulikuwa ni wakati wa kutafuta uhuru wa kujitawala (Uhuru wa bendera), na baada ya hapo demokrasia ilifinyangwa. Rejea Detention Act, Kufutwa kwa vyama vingi,n.k. mkakati uliolenga kutumikia fikra moja "Zidumu fikra za Mwenyekiti". Sasa ni wakati wa uhuru wa kifikra unaolenga kufungua mirija ya ufahamu kutatua changamoto za nyakati na hatimaye kuelekea kwenye uhuru wa kiuchumi.

  Leo tuna vijana ambao ni hazina kubwa kwa Taifa, tena vijana walio na fikra pana (kuliko Wassira, fikra pana kuliko Makinda, fikra pana kuliko Augustine Mrema) kutoka CDM. Vijana walio nyuma kifikra kama Nchemba na Lusinde kutoka CCM.

  Tuwaambie CCM Finito. Tuwaonyeshe Mlango wa kutokea.

  MAKAMANDA WA CHADEMA SONGA MBELE SIKU ZA WEZI ZINAHESABIKA.
  ZAMBIA,SENEGAL WAMEWEZA,SISI TUNAWEZA
   
 2. T

  Twaa Member

  #2
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ama kweli kamanda wangu! Zambia, Senegal wameweza hata sisi Tanzania Tunaweza pia!
  King cobra kutoka Zambia aliingia madarakani na kuwezesha kuirudisha bank iliyouzwa kwa bei ya kutupwa! Sasa hata sisi tunaweza kuirudisha bank ya NBC kama tutaweza kubadilika kama wazambia au wasenegali!
  kamanda wangu ni heri kufa ukipigania haki kuliko kuishi kwa hofu! Ila CCM ina wana wakati mgumu kwani vijana wanaohitimu vyuoni mwaka huu,kesho hadi mwaka 2015; wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita na kufeli pamoja na wale watakaohitimu kidato cha nne na kufeli pia lazma wataichukia serikali ya CCM na chama chao kwa ujumla! makamanda wangu Tz nasi tunaweza ifikapo mwaka 2015!
  ujumbe wangu kwa watz ''TUNASTAHILI KUA NA FIKRA PEVU ILI TUSIWE WEPESI WA KUDANGANYIKA NA PROPAGANDA ZA KUHUSU MAISHA YA MTU BINAFSI TUWE KAMA WATU WA AFRIKA KUSINI'' Tuko pamoja sana!!!
   
 3. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kwanza chama kimoja kuwa na viti vingi sana bungeni inaharibu uyakinifu wa bunge katika kuleta mipango endelevu. unabaki ushabiki usio na maana. napenda nusu kwa nusu.
   
 4. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  mmh, ukiiga k**** kwa tembo utapasuka msamba.
  Ruksa kabisa ku'copy' ila ni lazima u'paste' kwa akili.

  Tanzania iliwahi tuma wawakilishi kwenda Australia kujifunza utunzaji wa mazingira.
  Sehemu waloenda wakakuta wamepanda mikaratusi, nia yao ilikuwa kufanya water level iwe chini zaidi(kufanya maji yakauke) kwa matumizi yao.

  Watanzania walivyorudi wakaenda hamasisha vijiji vipande mikaratusi kumbe huku kwetu tunataka maji zaidi, acha ardhi iendelee kuwa kame. Baada ya muda sana ndo walikuja gundua.

  Hao walofanya mageuzi walikuwa na sababu zao na options walizokuwa nazo wanazijua wao.

  Na sie tuna vichwa vya kutafakari wenyewe kutokana na matatizo yetu na kujua nani anatufaa.
   
 5. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Si walikuwa wabunge wa chama kimoja fulani hivi, ni kawaida yao.
   
Loading...