Zama tunazoishi na HATMA ya CCM.

Zama tunazoishi na HATMA ya CCM.

the horse

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Posts
652
Reaction score
443
ZAMA TUNAZOISHI.

Siku za nyuma niliwahi kuandika barua, yenye kichwa cha habari "my letter to my father" ndani yake kuna maneno " yes, i want to inherit the country and everything on it.,but please Sir.,handle us a country in peace not in pieces.."

Zama tunazoishi ni zile ambazo watu wake wanaamini zaidi katika fedha na wamepungukiwa na uzalendo.,tena ubaya wake ni kuwa wale waliokuwa katika nyadhifa za kufanya maamuzi, kuweza kusimamia na kukemea ndio hasa wanaongoza kwa kupoteza uzalendo na wakawa na mapenzi ya dhati na noti.

Mwalimu na wazee wenzake wenye hekima waliwahi kuandika katika AZIMIO LA ARUSHA juu ya silaha tuliyoichagua. Akawaasa WATANZANIA kuto-focus katika fedha kwani ni silaha ya mabeberu, si silaha ya wanyonge.

Wakati huo ilikuwa "UTAJIRI" ni moja ya sababu za kukosa uongozi, utajiri wa aina yeyote halali au haramu ulikuwa ni moja ya sifa za mtu kutokuwa kiongozi..

USIA huo haukufanya kazi, imani ya fedha ikashinda mapenzi ya watu kwa taifa lao, watu wakalikataa AZIMIO na kila kilichomo ndani yake, ikiwemo USIA huu na MIIKO YA VIONGOZI.

Wakati huo, ilikuwa ni fedhea kwa familia ikitokea kuna mtoto wao amehusishwa na wizi, uhujumu uchumu au ufilisi na Ukupe.

Tuliyaacha hayo wenyewe na tukatengeneza kizazi chetu chenye mentality ya fedha..kizazi ambacho mwenye fedha ndie mfalme.,ndio anayefaa kuongoza, ndiye mwenye akili na ndiyo mfalme.

Kizazi ambacho fedha ni kigezo cha kuwa kiongozi, kila mmoja wetu ana bei..

Leo shujaa miongoni mwa watu ni yule mwenye fedha.,katika vijiwe vyetu tunawasifu kwa maneno ambayo yanatoka katika dhati ya mioyo yetu kuwa fulani ni mjanja, eti tu kwa sababu ameajiriwa ndani ya miezi sita na ana gari nzuri ya kifahari GX 120, modern Mark X, nyumba ya fahari Bunju na wala hakuna mmoja wetu anayejiuliza kapata wapi pesa hizo.

Na kinyume chake ni kuwa yule aliyeko kwenye ajira kwa miaka mitano, hana kiwanja, hana gari wala nyumba, jamii inamuona ni mpumbavu, lofa na asiye na akili sawasawa, kwanini akose vitu hivyo hali yupo katika nafasi ya kuweza kufanya chochote akapiga nae akaweka heshima mtaani,..


HIZI NDIZO ZAMA TUNAZOISHI...

Wanaccm ni kama wanajamii wengine, tunaishi nao katika mentality hii ya kuamini katika noti.,sio viongozi wala wanachama, kwao wao MWENYE NOTI ndio BWANA...!!

Haya tumeyashuhudia katika kila level ya uchaguzi ndani ya Chama, FEDHA imekuwa ndio ngao, ndio mlango wa kuingilia katika uongozi ndani ya Chama.,leo hii NUSU ya WA-NEC ni wafanyabiashara wakubwa katika maeneo yao huko mawilayani.,na kwa HAKIKA miongoni mwao wapo ambao kutamka AHADI kumi za mwanaccm hawezi.,na ni wengi kati yao...hawa ndio tunawategemea wakafanye maamuzi kwa niaba yetu..,tutegemee nini..

ITAKUWA NI MUUJIZA ikiwa watu hawa watatupatia kiongozi ambae HATOKANI na fedha.,kwani wao wenyewe wameingia kwa fedha, wanaamini katika fedha na kama wangelikuwa wenye kukataa fedha wangeanza sasa, kukataa takrima za sikukuu na posho za vikao zinazotolewa na wagombea.,lakini hivi sasa wanachukua, tunajipa guarantee ipi kuwa siku hiyo HAWATOCHUKUA..??

Watanzania wamechoshwa na RUSHWA..,watanzania wanataka mabadiliko.,na wasipoyaona, wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM..

CCM leo imegeuka kokoro, haichagui wanachama wake wala viongozi wake.,tunao wanachama milioni 6 lakini hatuna hata wanachama laki tano wenye kujua ITIKADI ya chama chao BARABARA..

Yawezekana ni AIBU kuchaguana kwa RUSHWA lakini hiyo ndio njia tuliyochagua.,njia ya AIBU.

Masikini wa nchi hii ni masikini wa kipato lakini si masikini wa fikra.,wanaona haya na wanayashuhudia na ipo siku watachoka na watafanya maamuzi.,tukiwafikisha hapo TUSIWALAUMU kwani itakuwa tumewataka wafike hapo..



ANGALIZO:


Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kuyasema maneno yafuatayo ambayo nami nitayatumia maneno hayo kama angalizo hapa:


”UONGOZI WETU hauna budi utokane na watu wa nchi hii, bila hila, bila rushwa, bila vitisho na bila ujanja wa aina yoyote. Tunapofikia kupata uongozi kwa kutumia hila au rushwa, au vitisho , au ujanja wa aina nyingine yoyote, basi hatukutokana na watu wenyewe na wala hauwezi ukawa uongozi wa haki na hauwezi ukawa uongozi wa watu”

Ernesto Sheka
 
Back
Top Bottom