Zali la mentali

Dr.adams faida

JF-Expert Member
Mar 11, 2013
1,885
3,343
She is Classy & Beautiful,...Ni miaka minne sasa nampenda sana Najma,..sitaki apate shida,.. pamoja na kwamba Mimi ni Mnyakyusa lakini niko radhi ku-apply Mahaba ya kisukuma ili nimlinde asinikimbie...yaani niko Radhi hata kuuza Figo ili yeye apate Peruvian Weaving!...huu ndio Ujinga Wa Mahaba niliobarikiwa...Nimebarikiwa Mimi tu Mfilipino kutoka Uyole.

"Baby nina Shida na Laki 2 sina Balance kabisa,simu yangu imepasuka kioo,Lotion imeniishia, na vingine vingi tu,Baby si unajua tena Maisha ya chuo?".....Kauli hii ya Najma ilinijia kichwani kila Muda,na huu ndio wakati ambao Salio ndani ya Wallet yangu lilikuwa Tshs 7,200...nitafanyaje?

Simu ya Salimu Bulicheka ndio iliniondoa kwenye Lindi la Mawazo, simu imekuja na Baraka sana hii,Hili Dili analosema Salimu lazima litakuwa la Maana,

"We Salimu huyo Mama Mwenda mmekubaliana Tsh ngapi?"

'' laki 3 Mwanangu, ila zipo nyumba 3 eneo moja, zote atakuonyesha".

''Ok, poa mtu wangu".

Daah! Mungu anipe nini?...nimechanganyikiwa kwa Furaha!, wacha nikapige hii Dili imfae Najma wangu,laki 2 zake, 1 yangu, akitaka zaidi nitampa, nikakata simu.

Sasa nikachukua Vitendea kazi vyangu vyote na kuelekea Makongo juu,Tangu nianze kazi hii hapa Mjini sijawahi kuzibua Vyoo vitatu kwa Mpigo,its a very huge deal ever!,..nilipofika Mbele ya Geti la Mama Mwenda pale Makongo kuna kitu nilikumbuka!, nikapiga simu!

"My Love, nitakupa ile fedha uliyoomba, nipo ofisini kuna Cheques nazisaini hapa,nivumilie kidogo, baada ya Masaa 2 njoo Mbalamwezi Beach nikupe,pia nina hamu ya kukuona pia, halafu nimekuongezea hamsini ununue hata gauni upendeze Darling,ok?''

'ok"

Fasta nikakata simu, kisha nikasukuma geti la kwa Mama Mwenda nikaingia ndani.

Sasa Pale nimeingia tu ndipo nikakutana na Suprise ya Maisha,...wasichana Wa chuo walikuwa wamejaa sana,...aisee kumbe leo nazibua Vyoo vya Hosteli!!!
Hamad! pale bombani yupo Najma wangu ...The Love of my Life,..anasugua Mguu wake kwenye jiwe taratiibu anajiandaa kwenda kuonana na Mimi pale Mbalamwezi Beach nimpatie Mzigo wake!

I was totally Shocked,Macho yetu yalikutana,...yakaumana milele...alinitazama mara mbili mbili...Vipira vyeusi vya kuzibulia choo viliteleza Mikononi, nimesimama wima kwa fadhaa ndani ya Ovaroli la kazi!..honesty am strong enough to face this...nilijipa moyo...this is Real Me!....niliziona Hasira zake...macho yake...mdomo wake ukiandaa michambo takatifu,aisee Sura ilinishuka kwa fadhaa kuu kama Farisayo anasujudu.

"Kaka Mashimo ya Sewage system yapo kwa huku, njoo uzibue!''...Hii sasa ilikuwa sauti ya Mama Mwenda!....lakini sikumjali kabisa, nikasogea Bombani,sasa nilisimama mbele ya Najma, nikapiga goti chini,nikatoa engagement Ring Mfukoni,ni Miaka 8 sasa sikuwahi kuisahau mahali popote, this is the One I truly Love..nilijipa Ujasiri nikatamka! ''MY LOVE, WILL YOU MARRY ME?''

Sasa Najma alinitazama kama Zombi!, kwa mara ya kwanza niliyaona machozi yake and she said.........."I wont, You were fake from the First Day!,ulinidanganya unafanya kazi Stanbic Bank, baada ya Mwaka ukaniambia umehamia Hazina,and now this is Real You! , sikuhukumu kwa kazi yako,kazi ni kazi, nakuhukumu kwa Uongo wako,Mimi sikukupendea Fedha na kipato,nilikupenda wewe kama wewe,lakini ukanichukulia kama Mwanamke wa kununua,ukanilinda kwa thamani ya fedha,...sasa nimefikia Maamuzi kwamba SITAKI....ndio Sitaki kukupoteza...wewe ndiye Mwanaume wa Pekee uliyethubutu kujitoa Mhanga kwa Shida zangu mimi,ukanipenda,ukanithamini,..leo nakuchagua wewe miongoni mwa wote,..and Finally I say to you "Yes I will"

by that Statement Dunia niliiona dhahiri inaungama!..niliiweka pete yangu kidoleni kwake huku nikishuhudiwa na Macho zaidi ya 40,.sikuamini.

''Hivi Wewe Baba! umekuja kuoa au Kuzibua Vyoo???"...kwa mara nyingine tena Mama Mwenda anasumbua!, ...Macho ya Mpenzi wangu yalinipa Green Light, nikaingia Kazini huku Moyo wangu ukiwa Umeibeba Dunia ya Furaha....Hakika leo nitazibua mpaka Vyoo vya Nyongeza!..its a matter of time!..Trust Me.
 
Duuu mfilipino wa uyole umetisha,kama nakuona unazibua na vile vyoo vya makasini pale.
Jf kuna mambo!
 
ni ngumu sana kuubadili mchanga kuwa mchele....na hayo ni mazingaombwe...hakuna uhalisia ...
 
Imetungwa vzr na Mwakauyole.
Hongera sn!
Asa hapo wasukuma wameingiaje?
 
Back
Top Bottom