Zali la mentali, ushauri tafadhali

hyo tapeli toka naija kama cm yako ina hang out app msearch utamcheck live bila chenga
 
Huu utapeli naujua tokea nipo shule ya msingi.
 
Mpaka leo matapeli wakizamani hivi bado wapo.
Mimi huwa naona wanitumia mara kibao hayo maujinga yao.
Hivi kumbe kuna watu hadi huwa wanaliwa kabisa
 
Daa mi nshapokea km tatu hv za dizaini hiyo mkuu,hao ni matapeli wanajifanya kutumia watu wa dini ili kukulainisha then wanakupiga,achana nae mapema iwezekanavyo
 
Weeeeee kimbia ufe hao ni matapeli tena sijui ndo Huyo huyo aliyekuandikia wewe maan na mimi aliniambia nitume hela ya kutuma
 
Mkuu watu wa humu wanakudanganya na kukupa ushauri mbaya, tuma hizo hela mwaya upate mazawadi yako!![emoji1][emoji1][emoji1]
 
Maui wao ni Nigerian matapeli wakubwa.watch it
 
Tuma mkuu.... So kila kitu uweke mawazo hasi tu... Saa nyingine tunajikosesha bahati kwa kufikiri kuibiwa... Kwan ukiibiwa we ndo utakuwa wa kwanza !!! Kwani dollar 98 kitu gani. ..mbona kunawanotapeliwa maelfu ya dollars... Usiskilize hao wenye mawazo mgando wanafkiri ili uonekane wa mjini lazma kila unachoambiwa uweke kuibiwa mbele (poor thinking) . Tuma na kama utaibiwa nijulishe ntakuchangia nusu... Jiamini hiyo ndo moja ya sifa ya mtu smart... Amini unachokifanya kwani skuzote ukitaka kufanikiwa jaribu kutake risk... Delivered.
 
Hahaha... Nakumbuka 6 years ago nilitumiwa hadi barua kutoka Royal Bank of Scotland [RBS] kuthibitisha kua Kuna hela yangu.. Dah, watu wanajua kufoji asee
Hata mimi mkuu miaka mitatu iliyopita nikatumiwa mpaka barua ya mwanasheria basi nikahangaika sana branchea za CRDB kutafuta swift codes....mwisho wa siku wanasema nitume hela ya kuidhinisha pesa iingie kwenye account nikaona wanazingua....ila kilikuwa kitita cha pesa
 
Duuuh!!! Bado kuna watu wanadanganywa na hawa wapuuzi!!! Ni spams hizo wanatafuta wa kuwatapeli...

Anyway... Kama una hizo hela jaribu ujiridhishe moyo
 
Duuh, mwaka jana nilinusurika hivyo hivyo, alikuja dem mmoja mwingereza anajifanya alishaolewa akaachika halafu kanielewa sana, akanambia anaenda Haiti kama volunteer doctor halafu aje bongo kuniona mimi nikawa namuitikia tu, kanitumia picha za watoto wawili kwamba ndo wake na mimi naendelea kumuitikia tu, baadae akanambia ana zawadi anataka kunitumia nikaendelea kumwitia tu, baadae akaja na e mail nyingine mara kuna rafiki yake anakuja senegal kwenye mambo ya dini so amempa akifika anitumie maana mzigo utakuwa umekaribia nikamwitikia tu,

akanitumia mpaka picha za parcels zenyewe nikamwitikia tu (nakumbuka alitaja vitu vyenyewe vilikuwa laptop 2 toshiba, digital camera, simu 2 I phone, jewellery, bahasha na picha zake nikaendelea kumwitikia) sasa aliye pewa mzigo akaanza kunichek kuwa kafika senegal hivyo nitume usd 100 kama gharama ili anitumie mzigo huku yule mwingine akuendelea kunisisitizia nimtumie huyu sister mapema ili mzigo uwahi kufika, hapo ndo ilikuwa mwisho wa kuendelea kumwitikia nikamjibu kuwa asubiri naenda bank kutuma na mpaka leo bado niko njiani sijafika banki, nadhani bado atakuwa anaendelea kusubiri,

Guys tuwe makini sana maana dunia ya sasa imejaa utapeli sana kila sehemu!!!
 
Hahaha hii ilikuwa ndio kama desturi enzi za Yahoo ...Yaani hao matapeli walikuwa kibao na utapeli wao mkubwa Ulikuwa ndio wa aina Hiyo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…