Zaidi ya watu 20 wafa ajalini Rufiji

Abdull Kazi

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2012
Posts
345
Reaction score
307
Ajali iliyohusisha magari manne imedaiwa kusababisha vifo vya watu zaidi ya 20 ktk eneo la Mkupuka, Kibiti wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia ajali hiyo ni kwamba ajali ya kwanza ilitokea majira ya saa 4 usiku jana kwa gari dogo aina ya Toyota Hiace kuligonga Lori lililokuwa limeharibika njiani pasipo kuwekewa alama ya tahadhari na kusababisha vifo vya watu 15 na majeruhi.

Ajali ya Pili katika eneo hilo lilihusisha gari kubwa la abiria lililokuwa linatoka Kusini kuwagonga majeruhi wa ajali ya kwanza waliokuwa wakipakiwa katika gari la Halmashuri kuwahishwa Hospitali.

Kwa muda huu, Mkuu wa Wilaya ya Rufiji yupo ktk eneo la tukio kwa ajili ya kupata maelezo ya kina.

Chanzo: MTU aliye katika eneo la ajali

=======
UPDATE:
=======

 
Mungu awarehemu, hata hivyo nashauri upeleke habari hii sehemu husika hapa sehemu ya propaganda na maswala yasiyotekelezeka
 
Ajali si imetokea? Sasa hayo mambo ya 'inadaiwa' yanatoka wapi?

Hebu iweke vizuri kaka ieleweke.
 
Mwenye mamlaka kisheria kuthibitisha kifo cha mtu katika jmt ni dk ndiyo maana kwa salsa tunasema inadaiwa/inasemekana nk
 
Ngoja kwanza nipige kimya hadi pale itakapothibitika....

NB;
Peleke Jukwaa husika...
 
Mungu awarehemu, hata hivyo nashauri upeleke habari hii sehemu husika hapa sehemu ya propaganda na maswala yasiyotekelezeka
maswala gani? ya chopa kutokata anga chalinze unamanisha. ok Mungu awarehemu mbele wao nyuma sisi.
 
Ingetokea moshi hii usingeona mzaha unaotolewa hapa kuhusu taarifa ya msiba....watu wa kaskazini huwa hawaamini kuwa maeneo mengine Pia kuna binadamu. Pum..v sana hawa na chadema yao
 
...poleni ndugu na jamaa' pia huu msiba niwa Watanzania wote tumefiliwa...
 
Ingetokea moshi hii usingeona mzaha unaotolewa hapa kuhusu taarifa ya msiba....watu wa kaskazini huwa hawaamini kuwa maeneo mengine Pia kuna binadamu. Pum..v sana hawa na chadema yao
acha tabia za kishetani we muhuni
 
Kwan hujiAmin Nah habari yako ala kaujui be in hell.

Hujui hata unachoandika ndugu, kama jambo hulijui andika kiungwana wanaojua wakufafanulie.

Ni hivi; hata uone mtu amechinjwa hapo huruhusiwi kuripoti kama habari kamili mpaka wanaotakiwa kuthibitisha wafanye hivyo kwanza!! Wanaothibitisha ni madaktari na polisi baada ya hapo ndipo habari hutolewa kikamilifu!!

Huyu aliyeandika huu uzi anajua hilo na ndiyo maana kaandika kama tetesi hata kama kashuhudia!
 
acha tabia za kishetani we muhuni



Kalagabaho na kibibititi, binafsi ningefurahi sana kama sote humu tukabadilishana nawazo na kujengana kimtazamo na kushindana kwa hoja badala ya kutukanana ambako kiuhalisia hakutujengi na kutuweka pamoja, nashauri tupendane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…