Zahera aisubirisha Zesco, Aussems ajadiliwa Simba

pantheraleo

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
691
878
Jumamosi iliyopita Yanga ikiwa ugenini Botswana ilifanikiwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo baada ya kuichapa Township Rollers ya nchini humo bao 1-0, hivyo kuitoa kwa jumla ya mabao 2-1 kufuatia sare ya bao 1-1 katika mechi ya awali Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere juzi usiku, Zahera alisema kwa sasa anaiweka kwanza pembeni timu ya Zesco ya Zambia watakayokutana nayo kwenye raundi ya kwanza ya michuano hiyo na kuelekeza mipango yake kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting.

"Siwezi kuzungumzia kuhusu mechi dhidi ya Zesco kabla ya iliyopo mbele yangu ya Ligi Kuu Jumatano (kesho) dhidi ya Ruvu Shooting, hivyo tunahitaji kwanza kumaliza mechi hiyo," Zahera alisema.
Kuhusu suala la safu yake ya ushambuliaji kukosa mabao mengi, alisema amebaini kinachowasumbua ni kukosa 'timing' (makadirio) pindi wanaponasa mpira kuanzia wanapokuwa umbali wa yadi 30 kabla ya kulifikia lango.

"Kwa kuwa tutakuwa na muda kabla ya mechi dhidi ya Zesco, tunaweza kulifanyia kazi suala la 'timing' linalowasumbua washambuliaji," alisema Zahera baada ya kuulizwa haoni kuna shida kubwa katika safu hiyo ya ushambuliaji kutokana na mabao yake yote kupata kwa penalti ama faulo.

Katika mechi ya kirafiki ya Wiki ya Mwananchi Yanga ililazimika kutokea nyuma na kusawazisha kwa mkwaju wa penalti wakati ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Kariobangi Sharks, kabla ya kupata matokeo kama hayo ikitokea nyuma tena kwa bao la penalti dhidi ya Township Rollers Uwanja wa Taifa na kisha Botswana ikishinda kwa mpira faulo.

Lakini kwa watani zao, Simba ambao walikutana na balaa kwa kutolewa katika michuano hiyo nyumbani, Uwanja wa Taifa kwa faida ya bao la ugenini na UD Songo ya Msumbiji kufuatia sare ya bao 1-1 baada ya mechi ya awali ugenini kutoka suluhu, sasa mashabiki wamejawa na hofu kuhusu hatima ya Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Mbelgiji Patrick Aussems.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya mechi hiyo juzi, walisema hata kama hakufikia malengo aliyowekewa katika michuano hiyo hakuna haja ya kumtimua kwani Simba ilicheza soka safi ikimiliki mpira kwa asilimia 65, na kilichowagharimu ni kukosa tu bahati.

"Unajua kocha aliwekewa malengo kufika nusu fainali na ikishindikana robo fainali, lakini safari hiyo imesitishwa leo (juzi), hatuoni sababu ya kutimuliwa, anachotakiwa ni kuijenga timu kwa msimu ujao, kwani kubadili makocha nako kunaigharimu timu," walisikika mashabiki wakijadili baada ya Simba kutolewa kwa faida ya bao la ugenini juzi.

Chanzo:Nipashe
 
Siku zote huwa naamini hawa makocha wa kigeni hawapelekeshwi na kufata matakwa ya viongozi!! miaka ya nyuma tulishashuhudia yule Kocha Kerry akilalamika kupangiwa kikosi na Nyange Kaburu ila huyu mbelgiji naona kama anashindwa kufunguka kwa kuogopa kibarua kuota nyasi. Ameletewa wabrazil ambao hawakuwa chaguo lake na yeye akasema ataenda kuwaangalia wakiwa kambini, mwisho wa siku naona anawalidhisha waliowaleta kwa kuwaweka pale benchi ila hawapo kwenye mipango yake!!
 
Back
Top Bottom