Zaharani - Maisha na mashairi

Zaharani - Maisha na mashairi

NGAYANIMO

Member
Joined
Feb 17, 2026
Posts
36
Reaction score
55
ZAHARANI - MAISHA NA MASHAIRI.

Verse..1.

Hizi mbio sio za Baiskeri , Haiwezi kabiri Kasi/
Tahadhari usije Ukaferi , Mbuzi Amzindi Farasi/
Usiwambie Watu watakucheka/
😄 🤣 "hahaha "
Wengi wameishia Sakafuni/

Chunga usipige mweleka , Usafi wa Nafsi sio Sabuni/
Unapozungumzia Hip hop , Lazima Utaniorodhesha/
Me ni postive Hip hop, Na Hii inajionyesha/
Ushairi kwangu ni Dhati, Sanaa sifanyii njaa/
Nadumu na Hizi harakati, Kila siku ,Kila saa/
Haimanishi Ukimya siandiki, Mwandishi Haishiwi Hati/
Walipo wanapatwa kwikwi, wanapagawa na Hi Dhati/
Makusudi najaza Hofu, hawaamini Mpaka wanajamba/
Wanapapaza ka vipofu hawaoni pakushika na Vaba/
Ubora sio wa kichina , Usioshe Fikra zako/
Sio tu ilimradi eti Vina, Wazi Me sio Mwenzako/
Utapotea usifuate nyayo , Yingine hasifatiki/
Ni Bora Tupige Miayo , hata ukibebwa haufiki...

Chorus:
Ni maisha na Mashairi , Mtaani ndivyo Navyoishi/
Nitaacha vipi kuwa mahiri , Na hizi " Mic" hazinitishi/
Ni maisha na Mashairi , Mtaani ndivyo Navyoishi/
Nitaacha vipi kuwa mahiri , Na hizi " Mic" hazinitishi..!

Verse..2

Wanashtuka Huu Muziki , Akili zinawaruka/
Wanaulizana itakuwa Vipi? , Na Mara Wameshaanza Kuanguka/
Wanaona Haya , wanajificha Nafsi zinawasuta/
Wanabaki kufutia Picha, Ninavyo Penya kwenye Ufa/
Najua wanakuna Vichwa, Huku Wanaona/
Ha.!!
Na Sikio alizindi kichwa, Vinywa Wazi wanashangaa/
Yes.!
Ng'ombe Hazeeki Maini , Na Maana Naitwa Run/
Ni ngumu Kunishusha Chini , Sio Rahisi kaa Ulidhani/
Hahitaji Kuumiza Fikra , Ukijua level Ya kweli/
Ni Heri Utulize Fikra , Utaumbuka kwa Hizi Ng'eri/
Jisitiri Usipate Aibu , Basi utadhalilika/
Unamudu Ngono Unaharibu , ukiambiwa unakadhilika/
Level yako ni Ya kitaifa , Bado ukizi Viwango/
Una ng'ang'ana Kimataifa , Ni Bure Tu Ubebe Bango/
Usijipigie Debe kiti , wazi Najua unajua /
Basi Pisha nikizi Beat , We ulokaa Unazingua..

Chorus:

"Ni maisha na Mashairi , Mtaani ndivyo Navyoishi/
Nitaacha vipi kuwa mahiri , Na hizi " Mic" hazinitishi/
Ni maisha na Mashairi , Mtaani ndivyo Navyoishi/
Nitaacha vipi kuwa mahiri , Na hizi " Mic" hazinitishi..!

Verse..3

Kwanza Nakuona Fara , Hip hop Wapi Bila Nguzo/
Huna unachojua , harafu mbishi Kwetu Gumzo/
Mpaka watoto Wadogo , wanajua hujui kitu/
Bado Tuna ng'ang'ana , Upo Tu kila Siku/
Dukani Kwenyewe Hauzi , Harafu Bado Makuzi /
Najua unauza Sura , Ulingoni Wewe haina Ujunzi/
Unashusha Hadhi ya Hip hop , Bado una dhalilisha/
Auendi bila kubebwa , Poyoyo Unasikitisha/
Hip hop imejaa uchafu , Tungo hazina Umahiri/
Ufanisi wenyewe umekopa / Harafu huna Ushairi/
Unataka hadhi ya umarenga , wakati Yupo Zaharani/
Ninajua unajua , Sisemi ni Jinsi Gani/
Weka Mic kado , huna hadhi yakuwa kinara /
Hata upige kelele , Bora u change Tu Biashara/
Hip hop sio Bongo fleva , utavaaje Suti na Dala/
Huna unachojua , Badirisha kila idara..

Ukwaju wa kitambo
0767 542 202
1774249780422.jpg
 
Verse ..3 ( zaharani)

Yo! Watu wanaathirika lakini Bado hawajali/
vipi? Mnakosa fikira za kuweza kufikiria mbali/
watu wanapata shida sio siri Bado ni hatari/
mifano mingi tumeona vipi kuhusu tahadhari/
kila siku watu wanaonya ni wagapi wanajali/
nusura hakuna kupona mapema mjihadhari/
maambukizi juu ya sindano watumiaji mjihadhari/
ukimwi nao umeshika pande zote hatari/
vipi sindano mnadunga hamjui kwamba ni hatari/
Tena moja inazunguka masikani tena bila ya tahadhari/
nyani ndio kwamba hamjari /
au ndio basi ufahari/
Zaharani nini nitasema na hakuna anayejali/
wengi wamekufa masikani kisa wamekosa Gari/
wamekufa KWA kujidunga na madawa ambayo ni hatari/
Ni vipi hauchi starehe Gani hatari/
utumiaji Bado unazindi ifanye nini serikali/
na kuacha watu wakaidi na jela hawajali/
labda ingetekwa sekta nadhani ingekuwa afadhali/
watumiaji wa madawa serikali ingewapa hifadhi/
Pindi wanapoacha madawa/
wapewe matuzo safi/
Kazi na Elimu ya kutosha/
Kuhusu utaraji, nadhani wengi wangeacha/
hata wale wasiotaraji .. ..

( msanii zaharani kwenye Wimbo wa Crazzy Buffa unaitwa " Muelimishaji"

Ukwaju wa kitambo
0767 542 202..

Iweke hii ngoma

Zaharani mzee wa vina, aliteleza vizuri sana kwenye ile ngoma ya ab skills
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom