ZADIA (Zanzibar Diaspora Association) yalaani ukamatwaji wa raia wasio na hatia Zanzibar

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482
Sunday, March 20, 2016

zadiaspora@gmail.com

215 459 4449
zadia.org

19 Mach 2016

Wazanzibari walielekea kwenye vituo vya kupiga kura mnamo tarehe 25 Oktoba 2015 kuwachagua Madiwani, Wabunge, Wawakilishi, Marais wa Zanzibar na wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kama inavyokumbukwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Bwana Jecha Salum Jecha, aliufuta uchaguzi wa Zanzibar na matokeo yake, na miezi michache baadye kutangaza uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi 2016.

Kufutwa kwa uchaguzi wa Oktoba na kutangazwa uchaguzi wa marudio ni vitendo vilivyolaaniwa na Wachunguzi wa ndani na nje ya Zanzibar, Jumuiya za Kimataifa na Mataifa mbalimbaili ulimwenguni kwa vile uchaguzi wa awali ulikuwa huru na waki, na kusisitiza kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo.

Vyama vingi vya upinzani kikiwemo kile Kikuu cha Wananchi (CUF) vilitangaza kuususia uchaguzi wa marudio kwa vile haukuwa na mashiko ya Kisheria, na badala yake kushikilia msimamo wao wa kutaka kutangazwa mshindi wa Uchaguzi wa Oktoba.

Kufuatia hali hiyo, kumekuwa na kamata kamata ya viongozi waandamizi wa Chama Kikuu cha upinzani cha CUF pamoja na wafuasi wake au wale wanaodhaniwa kuwa ni waungaji mkono wa chama hicho.


Miongoni mwao ni Mabwana Eddy Riamy, Mansour Yussuf Himid, Hamad Massoud Hamad na Mwandishi wa Khabari Bi Salma Said.

Wakati tukiandaa taarifa hii, Eddy Riamy yuko nje kwa dhamana, wakati ambapo Mansour, Hamad na raia wengi wasiokuwa na hatia bado wako kizuini. Aidha Mwandishi Salma Said ambaye alitekwa nyara na wale wanaodaiwa kuwa ni watu wasiojulikana, bado hajulikani alipo.

Kutokana na hali hiyo, ZADIA inalaani vikali vitendo vya ukamataji ovyo vya raia wasiokuwa na hatia, kwani vitendo hivyo vinakwenda kinyume na haki za binadamu.

Aidha ZADIA inatoa wito wa kuachiwa huru mara moja kwa watu wote waliokamatwa, au kuwafikisha kwenye mahakama za wazi na kuwafungulia mashtaka ili kama kuna kosa walilolitenda lijulikane

Sambamba na hayo, ZADIA inalaani hatua ya kuenezwa kwa wingi vikosi vya Jeshi la Ulinzi na Polisi vya Tanzania katika mitaa ya Zanzibar, na marufuku ya kutotoka nje iliyotangazwa katika Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Hali hizo zinapelekea khofu miongoni mwa raia, kuwanyima haki yao ya msingi ya kutembea na kuzorotesha shughuli zao za kila siku za maisha.

Omar H Ali,
Mwenyekiti, ZADIA
 
Ccm Pamoja Na Jecha ni Wapuuzi Wanafanya Upuuzi Wao Wakidhani Watu Wote Ni Wapuuzi,
 
Back
Top Bottom