Yusuf Manji awasili Polisi kituo cha Kati kuitikia wito wa RC Makonda

Nadhani ahifadhiwe hapo,mpaka siku ya ijumaa ambayo ndio aliyopangwa,si yeye anavyotaka kupanga.
 
Salute kwako Mkuu nimekuelewa
 
Kisheria yuko sawa Polisi hawana haki ya Kumpangia Mtu siku ya Kuripoti ila wana haki ya kumpa taarifa kuwa anatakiwa Polisi. Mahakama pekee ndo hupanga mda na siku. Mawakili 8 na 2 kutoka nje si wa kubeza.
Hakuna wakili toka nje ya nchi anaweza kufanya kazi Tz bila kupewa kibali cha muda na Jaji Mkuu. Hivi wageni wameshapata hicho kibali ndani ya masaa 24 yaliyopita!? Kama ni kweli basi nasema "shikamoo pesa"
 
Hizi Ni Kodi Zetu Zinachezewa Tu Na Makonda,

Hivi Ni Wapi Naweza Pata Details Ni Kesi Ngapi Serikali Ilipeleka Mahakamani Tangu JPM Aingie Madarakani?

Na Kati Ya Hizo Ni Ngapi Serikali Ilishinda Na Kwenye Kesi Walizoshindwa Ni Fidia Kiasi Gani Wametakiwa Kulipa?

Nafikiri Huu Ni Mwaka Wa Wanasheria Kupiga Pesa, Unapota Mwanya Wanasheria Utumieni

Wajinga Ndiyo Waliwao, Napata Hisia Za Kuanza Kukwepa Kulipa Kodi Sasa
 
Ngoma hapa inakuwa ngumu kwa Makonda kwasababu hawezi kuwatumia Polisi, ku plant kipisi cha bangi nyumbani kwa Manji, kama alivyofanya kwa Wema Sepetu. Nyumba ya Manji inalindwa na CCTV. Sasa sijui exhibit Makonda atakitowa wapi kuishawishi mahakama kwamba Manji anajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya. Hapa wazungu wanasema "Makonda has shoot himself on his own foot" A crippled soldier cant win a war.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…