Yussuf Makamba amwinda Reginald Mengi, yeye awataja mafisadi Papa rasmi!

Imekaa vibaya wala haijatulia, why now near election? katumwa na nani? na bado tutasikia mengi sana prior to 2010
 

Mkuu G,

Mbona sasa unatoka kwenye hoja. Yeye katimiza wajibu wake kwa kutaja 5. Na wewe itisha mkutano leo uongezee wengine kwenye hiyo orodha. Kwani umezuiliwa. Anataja watu ambao ana ushahidi wa kutosha ndo maana hana wasi wasi hata wakienda mahakamani. Naona tunaanza porojo za kupotosha mjadala. Yeye ameonesha mfano na mtu mwingine aje basi ataje wengine. Lazima anazo sababu za kufanya hivyo. Ziwe za wazi au zilizo jificha. La muhimu kwetu ni kumpongeza na kujadili nini kinatakiwa kufuata baada ya hapa.
 

Asante mkuu, watu kama hao wako wengi tu na humu JF ndio wanazidi kushamiri, yaani wao kila kitu kinatazamwa "kidini"!! Yaani wao kila likitajwa jambo wanaangalia wa dini yangu huyu kwanza. Hii ni mbegu mbaya kabisa ambayo naamini kama watanzania wataacha iendelee kukua itaangamiza kabisa taifa letu,.... kama kumtu katukosea tunaangalia ukweli, ni kweli kakosa? sio tuangalie dini! Maendeleo ya kweli tutayapata kwa kujitambua kwamba sisi ni watanzania na tunatakiwa kuwa wazalendo wa kweli kwa nchi yetu. Hayo ya dini yatatupeteza tu.....nyumba za ibada si zipo! tukashinde huko.
 
Mkuu hii ni janja ya nyani tuu,mahindi yanakomaa shambani,Wakati umefika kujitakasa kwa kila njia hata kama ni kuyatosa magabacholi wazawa wasalimike haya.Mengi ni kipaza sauti tuu wala asiudanganye umma waWatanzania,
 
Mzee mengi wala usijali...MIMI NA BAADHI YA WATANZANIA WENGI TULIOKO VIJIJINI TUPO NYUMA YAKO..na mafisadi waambiwe kuwa WE DONT DIE WE MULTIPLY...mungu ibariki Tanzania yas NYERERE.
 
Je vita yetu ya kupambana na umaskini itafanikiwa kwa kuwataja tuu mafisadi hadharani??

Kuna haja ya kupambana na mafisadi wenyewe au wale wanaowapa nafasi nzuri ya kutuibia???

Hapa jamvini naomba tujadili kwa kina na mnisaidie kuelewa zaidi!!!!!

Bado ninaamini ccm ndo tatizo kubwa la umaskini tunaoendelea nao mpaka sasa....
 
Makamba mwenyewe siyo msafi, hilo tunalifahamu. Tunaweza kusema anakumbatia mafisadi, kama moto umeanza kuwawakia hao mafisadi naye babu Makamba aweke kichwa maji, moto huo kuuzima ni ngumu.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Risk taker!!

Big five to Regnald Mengi!
Katika taarifa aliyotoa MwEnyekiti wa IPP kuna kitu kubwa ambacho sijui kwa nini anachelea kukitaja nacho ni suuport ya watu waliokuwepo na waliopo serikalini (zote zilizopita kuanzia ile ya Marehemu Nyerere na mpaka hii awamu ya nne ya JMK) ambao ni wabia wakubwa waliowezesha kufanikisha ufisadi!!

Mafanikio hayo yamewezeshwa kwa viwango mbali mbali katika wizara zote bila kubagua;mashirika ya umma,Benki Kuu;mabenki ya biashara;vyama vya siasa;asasi za kiraia na vyuo vikuu! Wizara ya fedha/hazina ndiyo mhimili mkuu katika kuwezesha uharamia huo because it is said that ''it takes two to tangle''
Rai yangu ni kwamba basi tusiwe waoga tuwataje kwa majina watu wote na wanaofahamika waliokuwa watumishi wa umma kama {akina Edward Lowasa;Robert Mboma; Daniel Yona;Gray Mgonja; Benjamin William Mkapa na familia yake; Cleopa Msuya;Balozi ALIYEKUWA SA jina lake nimelisahau} bila kwasahau akina MASHA ;Nizar Karamagi na wengine wengi tu!! ambao ghafla bin vuu wamekuwa matajiri wa kutupwa!

Na kama kweli JMK sio mmoja wao basi wote wahojiwe watueleze huo utajiri wao waliupata wapi? Wakati tumekua na kucheza nao kuanzia chandimu mara wana makasri Tahadhari Mkapa asiseme nina wivu wa kike!
Naweza nikaandika hata kurasa elfu kutoka kichwani mwangu ila nawaachia na nyie mpasue Bongo!!

Mwisho nimpongeze kaka yangu Mengi kwa ujasiri wa kumtaja Subash Patel hapo umepiga Ikulu ya Mwinyi!! Bado hujawagusa akina Dewji;Bahresa na wale walikimbia Debt conversion mashamba ya Mkonge!! Akina Mkapa walidesa kwa huyu jamaa kwani ni mkimya humdhanii wala hutamskia popote!!! Tete heeee !!! Yahh!!!Simba mwenda pole iko gonjwa!!!! Kula nyama nyingi?
 

kaka nyauba nadhani hatua ya kwanza ya kusolve any problem ni kukubali kuwa tatizo hilo lipo...nalo ni ufisadi, pili ku-identify key elements/actors kwenye hilo tatizo...i.e. kuwataja wahusika kama alivyofanya mzee wetu mengi na tatu ni ku-set/kuweka mipango au mikakati ya kupambana na hao actors wakuu...after mapambano ni kuset new system itakayozuia kujirudia tena kwa tatizo hilo.
nadhani mengi amesema na kutusaidia ku-identify top 5 fisadis..sasa ni juu yetu watanzania ku-deal nao hawa...haiwezekani every mega scam wawepo wao tuu...name any scam in this cpountry ambayo wao hao top 5 hawamo....ni maoni tu coz we dare to talk openly with our heart and inner parts of our minds.
 
Mkuu, licha ya kwamba uchambuzi wa 'negativity' sio kitu kigeni, LAKINI hii itaigharimu Tanzania safari ndefu sana sababu ya uchanga na umasikini wa nchi yetu. Tunajaribu kujenga 'mentality' isiyomwafaka kwa janga la ufisadi ambao wote tunajua kwamba bila ya kuutokomeza hakuna hatua tutakayopiga. Inabidi tubasilike na kufumba macho pale tunapopata mtu anayeweza kujitokeza na kukemea jambo ambalo tunajua linaiangamiza nchi. Mengi, Mwakyembe, Kilango, ..., wamethubutu kusema wazi kile ambacho hakuna yeyote anaweza kupinga kwamba sio cha kweli. Ukiangalia nafasi za hawa watu wote, wanaweza kukaa kimya na wakaendelea kula kuku kwa uhai wao uliobaki, lakini wanasema kwa kuwa wanaguswa na wanataka tubadilike.

BTW, Mengi amesema nchi inatafunwa na watu wasiozidi kumi, yeye ametaja watu wasiozidi watano, ni vema kama Mkodoleaji et al. wangejitokeza wakamalizia list ikiwa pamoja na kumtaja JK (ambaye Mengi ameshindwa kumtaja pengine kwa sababu za kidiplomasia).
 

Makamba mwenyewe siyo msafi, hilo tunalifahamu. Tunaweza kusema anakumbatia mafisadi, kama moto umeanza kuwawakia hao mafisadi naye babu Makamba aweke kichwa maji, moto huo kuuzima ni ngumu.

Mungu Ibariki Tanzania.

Naona watu wengi wameshupalia kwa nini kataja watu wenye rangi nyeupe ...lakini si ndio anao ushahidi wake na amewapa nafasi ya kwenda mahakamani kama wanaweza.

Pili nimesikiliza kwenye audio yake amesema neno moja, kuwa unaweza kubadilisha/kung'oa makatibu wakuu, mawaziri au watendaji wengine kwenye mawizara kwa kosa au tuhuma za kupokea rushwa kutoka kwa mapapa lakini ukaonekana ni mchezo wa kuigiza tu .....dawa iliyo kamilifu ni kudeal na mapapa wenyewe watoaji.
 
Hao mafisadi kawaanika vipi? Kamtaja nani? Kipi kipya alichosema? Mbona tunaridhika kirahisi hivi? Hamna substance katika alichoongea bali posturing tu.

Amandla........
 
Siku zotehuwa nachannganyikiwa na sioni kama ni ukweli:

1. Kumtenga Kikwete na ufisadi
2. kuwa kikwete ana mipnago mzuri na nchi!
3. Kuwa hawa wote hawawataji hao mafisadi na hawana mipango ya kuwapeleka mahakamani kazi kusema tu!

Kama Mengi na mapesa yake hana mpango wa kumshtaki ngau fisadi mmoja kama demo, je mimi ninayetiokea nyarugusu mwanza nitasemaje? sina uwezo wa kupata mwanasheri na kumlipa!

Hiii imebaki wimbo wa mafisadi, mafisadi thinga are not going on, JK wanayemsifia ndiye mwenye Rungu na madaraka yote juu ya mafisadi lakini wapi!!!!!!

anawahamisha toka huku kwenda kule!

Ndani tatizo ni rais, hwa wote watabadilika tu JK akibadilika, hawa wote watafanya watakavyo kama JK naye yuko kama wao.

Mengi kweli unaheshimika, lakini UNAPOTOA KAULI REJEA, ZISIZOPNA IMPACT YOYOTE -zaidi ya publicity, BASI TUTACHEZA TU HUU WIMBO, miaka inaenda....
 
Hao mafisadi kawaanika vipi? Kamtaja nani? Kipi kipya alichosema? Mbona tunaridhika kirahisi hivi? Hamna substance katika alichoongea bali posturing tu.

Amandla........


Naona tuko kwenye boti moja kaka , thanks

Hii style ya kutaka kupendwa na jamii tumeigundua, hana jipya!!!!!!!!!
 
Mkuu hii ni janja ya nyani tuu,mahindi yanakomaa shambani,Wakati umefika kujitakasa kwa kila njia hata kama ni kuyatosa magabacholi wazawa wasalimike haya.Mengi ni kipaza sauti tuu wala asiudanganye umma waWatanzania,

Ujumbe umefika
 

Sio kupotosha amewataja wakati na yeye yumo humohumo ,kila siku tunasema anaeuchukia ufisadi ajitenge ,maana nusu ya wafuasi wa Sultani CCM utawasikia wakisema kama Mengi na wengine kumshinda yeye ,lakini bado wanaonekana wamejibanza humohumo na hawawachukulii sheria yeyote ile si kuwafukuza uanachama wala kuvuliwa madaraka ,wale walioshitakiwa naamini kabisa wanendelea kupokea mshahara wao na wakishinda wanaweza kabisa kuidai serikali fidia ya kuharibiwa jina.

Tunasema wajitenge na Chama Tawala ambacho ndicho chimbuko la ufisadi ,wakae pemeni kuungana na WaTz wengine katika vita hii ,Mengi amewataja wote ni kutoka Chama Cha CCM halafu huko huko anawajazia mipesa , Sasa uhakika gani kwamba feza alioyoichomeka kwa umoja wa wanawake wa CCM huwa hapo sipo zinapoishia isipokuwa ni njia tu ya kupitia ili zifike kunakohusika.

Kuna vyama vya upinzani vinapigana vita hii ya ufisadi kwanini Mengi ikiwa anajiamini asivisaidie kuvitilia fedha ili kufanikisha ushindi lakini badala yake anawajazia mafisadi mapesa kwenye account zao. He is the one hakuna haja ya kupongezwa kama kupongezwa basi wanaohitaji kupongezwa ni wale wanaopanda juu ya majukwaa na kusema CCM ni Chama Cha mafisadi na si kupongezwa Mengi ,wapinzani hawamhitaji mtu kutoka upande wa CCM katika vita hii ,hii ni vita ya upinzani dhidi ya Chama Tawala ,Mengi anamsifu Kikwete wakati ushindi wa 2005 wa Kikwete unahusishwa na fedha ya ufisadi nasema upinzani hauhitaji kampeni za Mengi maana tatizo linaonyesha bado tupo pale kwenye Mwakiembe na Rostam confrontations ,Mengi anaendeleza kwa kutoa sapoti kwa mlango wa nyuma ili kubamiza upande wa Rostam na sio anapiga vita ufisadi kwa kuwa ana uchungu sana na raia ,hivi ni vita ndani ya CCM na sio kuwasaidia watanzania kujikwamua katika hali duni ya maisha ,vita vya kumkomboa Mtz vitaletwa na kusimamiwa na walio nje ya CCM na sio waliondani.
 


- Hapa hakuna kawaida, majina yametajwa rasmi sasa ni wajibu wetu kuchunguza wameiba nini, wapi? Wameshirikiana na nani?

- Tusiwe wazembe wa kusubiri Mengi atufanyie kila kitu, ndio maana tunakwama, maana tufanyiwe kila kitu mpaka kufikiriwa, that is pathetic!

FMES!
 
Makamba and the whole CCM are bunch of liars, they don't deserve more than a life jail time
 
- Afadhali ya Mengi, kuliko upinzani wa CUF na Zitto, wanayecheka mpaka jino la mwisho na JK huku wamevaa kanzu wanakwenda kwenye pilau sio Lipumba na Seif? Unajichekesha na "fisadi" na kwenda kula naye pilau?

- Halafu unamlaumu Mengi anayewachapa bakora fisadis?



FMES
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…