Huyu jamaa sijui nini kimempata mpaka sasa kawaachia uwanja akina diamond na hakika angeendelea kuimba huyu ndiye angekuwa mpinzani wa kweli wa Simba ila siyo huyu anayepambanishwa naye kwa sasa.
Nakumbuka sana ule wimbo wake anaimba amechoka kupiga honi, aisee wakati unatoka nlikuwa Mkuu high school yaani kuna binti nilikuwa namkubali sana alikuwa form six PCM nami niko five PCM, sijui yuko wapi siku hizi Tele, kweli maisha ni safari ndefu yaani huyu mtoto wa Kihehe alikuwa mzuri sana, mweupe kweli kweli.