Mchezaji wa zamani wa PSG, Kylian Mbappe siku ya Mei 16, 2024 huko Paris nchini Ufaransa, alizindua sanamu lake katika Nyumba ya Makumbusho ya Madame Tussauds, na kuzua gumzo kutokana na kufanana kwa kiasi kikubwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa.
Wakati wa hafla hiyo iliyohudhuriwa na Baba yake Mbappe (Wilfrid) na marafiki zake wa karibu, sanamu hilo lilionesha pozi maarufu la kushangilia ambalo Mbappe hulitumia.
Sanamu hiyo inasimama kama ishara ya athari ya kudumu ya Mbappé kwenye mchezo wa Soka na uwezo wake wa kuungana na mashabiki duniani kote.
Haiwezi kuwa picha ya kushoto maana vizazi vya mbeleni huko vikija kuambiwa huyu alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu kwa jinsi alivyovaa hivyo hawatoamini watahisi pengine alikuwaga msanii/mwanamuziki.