Yupi ni mpenzi sahihi?

Yupi ni mpenzi sahihi?

chemistoftz

Senior Member
Joined
Aug 3, 2013
Posts
111
Reaction score
52
Habari zenu wapendwa,

Natafuta mke nahitaji kujua yupi ni mke sahihi kati ya huyu mwenye degree na huyu ambaye aliishia form four na akafeli kwa ufahamu wangu nilionao, ili kuwa na familia bora na yenye mafanikio ni vizuri kuwa na mke mwenye elimu ya kutosha. Namaanisha kwamba watoto wangu nitakaozaa wasijepata shida kipindi nitakapotangulia mbele ya haki.

Naombeni mchango wenu

Kwani wahenga walisema "kosea njia utaelekezwa ila usikosee kuoa"

Seriously

Naombeni mawazo yenu
 
Ngoja waje mkuu but mimi najua kila aina ya mke mwenye elimu ndogo na elimu kubwa kila mmojawao ana Udhaifu na uzuri wake
 
Afadhal kwanza jina lako ni Juma.
Mwanamke huolewa kwa mambo manne.

-Nasaba yake
-Mali yake
-Uzuri wake
- Dini

Chagua mwenye dini upate kufanikiwa,,hao wawili angalia nani amemzidi mwenzie dini na utu,kuhusu elim..kua na elimu haimaanishi kua na hela,rizki anaetoa ni Mungu pekee.
Anaeza akawa hajasoma kama mwenzie lakini akawa mwingi wa fikra na ana mipango endelevu.

Hakika dunia ni starehe,na starehe bora ni kupata mke mwema.Kila la Kheri Mkuu.
 
Juma bana acha hizo mke hachaguliwi kulingana na kiwango cha elimu yake bali tabia,nidhamu nzuri.

Inaonekana unamhofia sana wa degree either huna elimu kama yake au ana ajira ya kipato kinachokupa mchecheto
 
Ahsante kaka
 
Sure kaka....namhofia
Ila nashkuru kwa mchango wako ntaufanyia kazi
 
Nimekua na mama alieishia darasa la saba na mimi niko brilliant as ever! Mama ndo ananipa moyo sana katika masuala ya elimu.
Ko haijalishi kiwango cha elimu, wewe oa unaeona anakufaa
 
Habari zenu wapendwa..natafuta mke
Nahitaji kujua yupi ni mke sahihi kati ya huyu mwenye degree na huyu ambaye aliishia form four na akafeli
Kwa ufahamu wangu nlionao, ili kuwa na familia bora na yenye mafanikio ni vzuri kuwa na mke mwenye elimu ya kutosha
Namaanisha kwamba watoto wangu ntakaozaa wasijepata shida kipindi nitakapotangulia mbele ya haki
Naombeni mchango wenu
Kwani wahenga walisema "kosea njia utaelekezwa ila usikosee kuoa"
Seriously
Naombeni mawazo yenu
Je! Dada zako nao wamesoma elimu ya kutosha nao waje kibaguliwa wakati wakuolewa? Kwa taarifa yako ndoa nyingi za wote wasomi ni ligi ndogo umbabaishe nani wakati wote tuna elimu? Elimu kitu kingine na ndoa jambo lingine
 
Unapotaka kuoa ni vizuri ukaangalia na nguvu kama mojawapo ya sifa kuu za mwanamke maana mambo yakienda kombo anaweza shika hata jembe au kumwaga zege.sio unaoa mwanamke mrembo legelege ambaye ukimsimamisha juan dakika tano anaugua
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Sawa
Nimekuelewa
That's a point
 
Je! Dada zako nao wamesoma elimu ya kutosha nao waje kibaguliwa wakati wakuolewa? Kwa taarifa yako ndoa nyingi za wote wasomi ni ligi ndogo umbabaishe nani wakati wote tuna elimu? Elimu kitu kingine na ndoa jambo lingine
Sina Dada
Tumezaliwa wanne tu
Wote ni wa kiume
Na nimegraduate mwaka Jana July as a chemist
 
Ndg,suala yupi ni mpenzi anaye faa kuoa ni kwamba,ktk mapenzi au ndoa hayo masuala ya elimu,kazi nzuri yenye kipato kizuri,uzuri wa sura umbo sio sifa ya mwanamke mwema na bora wa kuoa,angalia zaidi tabia yake ikoje mambo mengine hayo hayana nafasi ktk mapenzi ama ndoa.
 
Jumaaa...... dini si inaruhusu.... kamata zote bwasheeee..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom