Yupi mpenzi wa kweli?

uliyekutana naye kwenye shida huyo ndo mzuri
 
uliyekutana naye popote, lakini awe ni mwenye kujitambua nini anafanya.
 
Mpenzi wa kweli anatokana na Mapenzi ya kweli aliyonayo Moyoni mwake juu yako...!

So unaweza kukutana nae kokote iwe kijiweni, kanisani, baa, awe mjane, yuko single,anaishi geto, mfanyabiashara, hajasoma sana, mrefu, mweusi mlikutana gesti yaani yote hayo lakini mapenzi ya kweli ni yeye aamue Moyoni mwake kukupenda kweli!

Kwani kuna watu wamekutana makanisani lakini ndoa zao hazikudumu na kuna watu wamekutana mazingira ya ajabuajabu na wapo kwenye mapenzi mazito kwa muda mrefu.

So sidhani kama haliflani ya mtu au eneo flani mlilokutana lina connection kuubwa na mapenzi ya mtu kwani Moyo ndio unaoamua na sio mazingira,Japokuwa mazingira yanaweza kuchochea mahusiano yenu.

Tembelea thread hii uone watu walivyokutana kwenye mahusiano yao.



Je ulikutanaje na Mumeo/Mkeo Kabla ya kuwa kwenye Mahusiano?
 
Hakuna kanuni ya kumpata mke mwema ina tegemea wapi moyo wako umeangukia haijilishi ni sehemu gani kati hizo ulizotaja
 

wats matter is real love so long as mmekutana sehemu halali
 
Binafsi mke au mume mwema hutoka kwa Mungu tuu. Ni kufunga na maombi ,na roho Wa Mungu atakuonyesha mkeo/ mumeo . Binafsi wengine tunakutana nao makanisani au misikitini lakini kama sio Roho Wa Mungu kukwambia au kama sio kwa mkono kuonyoosha basi huyo si mumeo au mkeo. Kwa experience yangu hao wote uliowataja hapo juu kwenye maada ,kama hawajaguswa na Mungu , basi hawezi kuwa mkeo au mumeo. Tutawapataje wenza ? Kufunga na maombi , kuwa na subira kwa kusimama na neno lake basi yeye hatokuacha.

Wengi wetu sisi binadamu tunakuwa na haraka sana kwenye kufunga na maombi. Huwa tunataka kujibiwa haraka iwezekanavyo , lakini tukumbuke ya kuwa Huyu Mungu hana kanuni na si mwanadamu kama sisi. Saa nyingine huwa anajibu haraka maombi yetu na saa nyingine huwa anachelewesha kutaka kujua hizi Imani zetu kwa kuzipima. Wapendwa Mungu anajibu , haijalishi wapi utakutana na mkeo au mumeo . Akipangacho Yeye mwanadamu yeyote hawezi kukijua ila kwa kupitia Neno lake, Maombi na Yeye atatuonyesha tuu kwa Yale yasioyooneka . Kwa Yeye anajua mpaka namba za nywele zetu , kwa nini asijue mahitaji yetu? Ni kumlillia Yeye Tuy aliye juu mpaka kieleweke , ili mapenzi yake yatimizwe,. Kwa hiyo dear haijalishi wapi mke au mume anakotoka Bali cha muhimu ni kujua Je ametoka kwa Mungu . Kwa kuwa alisema mwenyewe Mke mwema hutoka kwake. Thanks!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…