Yupi anayefaa, Tajiri ila hana muda na mimi au mwenye uwezo wa kawaida ila yupo nami muda wote

vantz

JF-Expert Member
Apr 22, 2016
1,107
570
Kama kichwa cha habari kinavyojielezea,

Mimi ni binti mrembo tu nina kazi yangu nzuri namshukuru Mungu, nimepita kwenye mahusiano kadhaa changamoto hazikosekani, nimekutana na wenye uwezo wanaoweza kanipa nitakacho na wenye uwezo wa kawaida tu.

Nilichojifunza ni kwamba unaweza kuwa kwenye mahusiano na mtu anaejiweza akakupa kila utakacho ila hana muda na wewe hamna out wala muda wa kukaa mkayajenga hata mazungumzo ya kawaida maana mimi ni mpambanaji.

Mkikutana ni show basi siku zinaenda mwaka umekatika hamna la maana na sio kwamba anamahusiano mengine hapana ingawa mwanaume huwezi msemea ila ni mtu ambaye uko nae huru ila yuko busy muda wote hawezi kujenga muda kwa ajili yako ila muda wa kufanya mengine kama kwenda Bar, karaoke nk anao.

Pili mwanaume ambae hawezi kukuhudumia kwa chochote mnapata muda wa kuzungumza kushauriana kupanga mambo ya maendeleo ingawa hamuwezi kwenda out nk kutokana na kipato ila mapenzi mnayafurahia hata kwa kukaa ndani tu coz mimi sio mtokaji na haijawahi kunipa chochote wala sijawahi kumuomba coz namjua hali yake.

Ingawa ana wasiwasi na mimi kutokana na uwezo wake na urembo wangu ila mimi sina tatizo coz najimudu kwa kila kitu. Sasa huyo mwenye uwezo miezi4 hatuko vizuri na naona nimeshindwa mimi kwa moyo mweupe coz sijawahi kuenjoy nae hata siku moja nataka kumpokea huyu wa hali ya kawaida kwa moyo mmoja tujenge familia maana kule naona utumwa.

Naombeni ushauri ndugu zangu.
 
ushauri wangu mkubwa kwako mpendwa wangu...ni kukuruhusu ufanye kile unachoona moyo wako unapenda....najua kuna vigezo unavyo viitaji ili umkabidhi mtu moyo wako...kazi yako kubwa ni kulinganisha sifa kati ya hao wawili ukiona mmoja wapo anazosifa zote unazozihitaji basi moyo wako ndio ulioridhika naye...
 
Umeona tofauti hana muda na wewe lakini bado upo naye kwa sababu ya pesa zake sasa jivue gamba uende kwa huyo suruali afu baada ya miezi 8 utaleta mrejesho
Asikwambie mtu mapenzi na pesa ni vitu vinavyo paa pamoja
 
Kiuhalisia, kama huyo mwenye pesa anakupenda nenda kwake.

Huyo asiye na pesa mtapeana stress muda si mrefu, mapenzi hayalipi kodi, hayalipi ada za watoto, hayalipi bills.

Kama kweli anakupenda huyo mwenye pesa, nenda kwake.
 
ushauri wangu mkubwa kwako mpendwa wangu...ni kukuruhusu ufanye kile unachoona moyo wako unapenda....najua kuna vigezo unavyo viitaji ili umkabidhi mtu moyo wako...kazi yako kubwa ni kulinganisha sifa kati ya hao wawili ukiona mmoja wapo anazosifa zote unazozihitaji basi moyo wako ndio ulioridhika naye...
Asante mkuu kwa ushauri mzuri
 
Umeona tofauti hana muda na wewe lakini bado upo naye kwa sababu ya pesa zake sasa jivue gamba uende kwa huyo suruali afu baada ya miezi 8 utaleta mrejesho
Asikwambie mtu mapenzi na pesa ni vitu vinavyo paa pamoja
Sio kweli sio mara ya kwanza kuwa na mtu asiye na hela
 
Nina tibu mioyo iliyo mipweke, mioyo iliyopigwa na Baridi , mioyo iliyoumizwa, mioyo iliyokosa mapenzi na mioyo yenye Kiu ya mapenzi ninaitosheleza barabaraa
Anza kutoa tiba mkuu
 
Olewa na pesa uwe mpweke
Olewa na suruali myajenge then akumwage baadaye. Anaweza akawa anataka kuoa pesa huyo.
Listen to your heart. Don't use your brain on this.
Na hapo ndio pananipa wasiwasi kumwagwa baadae
 
Back
Top Bottom