YUPI ANASTAILI KUWA KIONGOZI

SHADOWANGEL

JF-Expert Member
Sep 15, 2014
528
349
kila naposikia flani ameteuliwa/amechaguliwa kushika nyadhifa flani katika nchi yetu ya Tanzania kumekuwa na mitizamo tofauti juu ya watu wanauchagiliwa wengine kuunga mkono na wengine kupinga,
Je unafikiri mtu wa aina gani anafaa kuwa kiongozi kwako katika sekta binafsi na serikalini?

David Lloyd George aliwai kusema “Raia wako tayari kufanya yote wawezayo maadamu tu wana viongozi, mradi tu Serikali inaeleza malengo yake waziwazi na raia wana uhakika kwamba viongozi wao wanafanya yote wawezayo.”

MANENO ya Lloyd George yanaonyesha wazi kwamba watu wanatazamia viongozi wao wawe hodari na wajitahidi kikweli kuboresha mambo.

Ni kiongozi gani ambaye amethibitika kuwa mwenye hekima sana na nguvu hivi kwamba anaweza kukomesha uhalifu? Kati ya viongozi wa leo ndani ya Tanzania,

ni nani mwenye uwezo na huruma ya kumpa kila mwanadamu chakula, maji safi, na matibabu?

Ni nani aliye na ujuzi na azimio la kulinda na kuweka mazingira katika hali nzuri Tanzania?

Ni nani aliye hodari na mwenye nguvu vya kutosha kuhakikisha kwamba wanadamu wote wanaishi maisha marefu na yenye furaha?

Swali Langu
Je unafikiri mtu wa aina gani anafaa kuwa kiongozi kwako katika sekta binafsi na serikalini?
 
Back
Top Bottom