Yule Sokoine wa pili mbona simsikii tena!! Ina maana Usokoine ulikuwa kusaka Urais tu?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,903
2,884
Si mara moja wala mara mbili nilimskia aliyekua Naibu Waziri wa fedha pia naibu katibu mkuu CCM bara ambaye kwa sasa ni waziri wa mambo ya kilimo na mifugo akijinasibu.

Eti watu wanamkubali sana kiasi kwamba wanamwita sokoine wakimaanisha utendaji wake unashabihiana na ule wa Waziri Mkuu wa zamani mheshmiwa Edward Mornge Sokoine sasa tangu JPM aingie madarakani sijamsikia popote tena akiitwa hilo jina nini kimempata Sokoine wetu jamani!!?
 
Kwa kweli nami nashangaa kwani namkubali sana Mh. Waziri huyu. Labda kama anafanya kazi ki,ya kimya. Namshauri aivalie njuga Wizara yake akifanmya mabadiliko itamopaisha tena sio tu kitaifa bali kimataifa!!!
 
Sokoine wa pili yupo hivi majuzi alifanya ziara ya kushtukiza machinjio ya vingunguti, hukusikia???
 
Ule ulikuwa upuuzi mkubwa..mtu huna hata vinasaba naye unajinasibu kuwa reincarnation yake
 
Back
Top Bottom