Yuko wapi Profesa Paramagamba Kabudi?

Retina

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
1,037
1,154
Huyu jamaa anafaa kuigiza, sijui alisomaje sheria, anajua kuishi na mtu kwa speed Sawa. Huyu jamaa alivyopretend aliaminiwa mpaka akapewa jimbo hata wenye jimbo hawajui.

Alituwakilisha Watanzania milioni 60 kuonja dawa Ya covid kule Madagascar akipewa ndege ya serikali kwenda kuleta mabox, sijui yalipotelea wapi.

Alikuja na msemo wa kutoka jalalani mpaka juu, akimaanisha kuwa mhadhiri wa chuo kikuu kumbe ni jalalani, je walimu wa shule za msingi huko tupaiteje.

Alichombeza neno mabeberu, huku tukichukua misaada yao kila kukicha.

Aliigeuka rasimu ya katiba, kama hakushiriki kuiandaa.

Mbwembwe zote za Kabudi zimetulizwa ndani ya miez miwili tu, hakujua enzi Zina mwisho.

Endelea kula kilichobaki, Lakini haupo mstari wa mbele kama ulivyokuwa kwa mwendazake.
 
1622365528856.png
😅
1622365609077.png

... BONGO MUVI IENDELEE!
 
Huyu jamaa anafaa kuigiza, sijui alisomaje sheria, anajua kuishi na mtu kwa speed Sawa.Huyu jamaa alivyopretend aliaminiwa mpaka akapewa jimbo hata wenye jimbo hawajui...
Huyu mzee alikuwa anajipendekeza mpaka nadhani mkewe na watoto walikuwa wanalia wakimtazama anavyohema na kutoa macho huku akijiita majina ya kujitukana mbele ya binadamu mwenzie.

Mfano mimi ni mtu dhalili, umenitoa jalalani, ikafika amamuita binadamu mwenzie Mungu. Akitoa vitisho mbali mbali huku akitema mate na kutoa macho kama mjusi aliyebanwa na mlango... kweli ulikuwa muda wa maigizo na kujibagaza kwa hali ya juu sana.
 
Back
Top Bottom