Wahujumu uchumi Mkoa wa Kagera miaka hiyo hawatamsahau! Alikuwa mmoja wa washauri mahiri wa uchumi wa rais wa awamu ya tatu!by that time akiwa Kagera nafikiri ilikuwa ni 1983's, inaonekana unamjua sana huyu mheshimiwa; mimi nilikua mdogo sana lkn nimekua napata taarifa zake, watu wa namna hii ndiyo wanafaa kuongoza hii nchi bwana.
He is safe and sound and live a quiet life....
Kwa ufahamu wangu nsa kaisi alikuwa daktari wa wakina mama na watoto muhimbili,. Lakini kwa sasa ni mstaafu,. Sjui atakuwa wapi dsm au kwao mbeya
Duh! Ee bwana ee! Hahahahaaaa! Huyo ndo Nsa Nkaisi! Kwa kweli hawa ndiyo wachache Mwalimu alifauru kuwapandikiza fikra za kizalendo (patriotism) katika itikadi ya Ujamaa na kipaumbele kwao ilikuwa ni kulitumikia taifa and no nonsense! Walikuwa hawahongeki bana.Nakumbuka tetesi hii kutoka kwa Dereva wake wakati akiwa Kagera: Kuna mama mmoja alichukua maziwa lita 5 eti anaenda kumpelekea nyumbani kwake, akamkuta anapiga deki, basi akaambiwa asubiri kidogo. Baada ya kumaliza Kaisi akatoka na Mugs mbili, akamwambia yule mama lazima wayanywe wao wawili mpaka yaishe kwani yeye anakaa peke yake na yule mama anajua hilo (Nasikia alikuwa Secretary wake). Basi zoezi likaanza Mama wa watu akajikuta anakunywa maziwa vikombe kibao bila kutaraijia na yaliyobaki yule mama aliambiwa aondoke nayo.
Kwa kweli alikuwa anaepuka vishawishi vya Rushwa za aina zote.
Namkumbuka lilikuwa bonge la jembe enzi za mwalinu. Alipokuwa mkuu wa mkoa Kagera nakumbuka hakuwa na mke wala hausugeli kwake. Tabia yake hiyo hiyo, ukimsapraizi kwake utakuta anapiga deki (akiwa mkuu wa mkoa) na akikuheshimu sana asikutoe benzi atakutole kiti chini ya mti whoever you are na ataendelea kudeki. Patakapokauka ndo atakukaribisha ndani. Nkais bwana!
Ni kweli huyu bwana ni jembe, akiwa mkuu wa mkoa wa mara kuna wakati alikuwa anatembelea ofisi mbali mbali za umma kujionea ubabaishaji unaofanyika na anaondoka bila hata watendaji hao kufahamu kuwa mgeni wao alikuwa ni nani (kinyadhifa) na hivyo kujikuta watendaji hao wakiitwa ofisini kwake na kuambiwa mapungufu yao kazini.
Nakubaliana na wewe hapo pa bluu. Tatizo ndo hivyo tena wakisha-park wanaanza kulipia gharama ya sadaka waliyolitolea taifa and nobody cares enough for them! Pity for our national heroes.by that time akiwa Kagera nafikiri ilikuwa ni 1983's, inaonekana unamjua sana huyu mheshimiwa; mimi nilikua mdogo sana lkn nimekua napata taarifa zake, watu wa namna hii ndiyo wanafaa kuongoza hii nchi bwana.
Ni kweli huyu bwana ni jembe, akiwa mkuu wa mkoa wa mara kuna wakati alikuwa anatembelea ofisi mbali mbali za umma kujionea ubabaishaji unaofanyika na anaondoka bila hata watendaji hao kufahamu kuwa mgeni wao alikuwa ni nani (kinyadhifa) na hivyo kujikuta watendaji hao wakiitwa ofisini kwake na kuambiwa mapungufu yao kazini.
Siyo kweli na hakwenda vita ya kagera,ana mtoto mmoja.nasikia aliumia vita ya kagera hadi jogoo amenuna! yuko kama dk kamuzu wamuyaya!
siyo kweli jamaa hana tamaa hiyo.