Yuko njiapanda

Yuko njiapanda

Verifier

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2019
Posts
457
Reaction score
1,541
Habari za asubuhi wapendwa! Bila shaka mu buheri wa afya mkiwajibika kujitafutia mkate wa siku.

Kisa hiki kimemtokea ndugu yangu, ila nitakiandika kama kimenitokea mimi.

Nipo kwenye mahusiano na mrembo mmoja huu ni mwaka wa pili. Mahusiano yetu kwa muda huu wote ni mazuri, tunapendana na kuaminiana japo mitafaruku midogo midogo/kupishana maneno hakukosekani. Linapotokea tatizo huwa tuna aa chini na kutatua amicably.

Mrembo wangu huyu alishanitambulisha kwa ndugu zake wa karibu hivyo ninawafahamu na wao wananitambua pia. Alinitambulisha kwa "ndugu" yake mmoja aliyekuwa masomoni ughaibuni ambaye alikuwa karibu naye sana. Kwa vile alikuwa ng'ambo sikuwa nimemuona. Alidai ni mtoto wa cousin wake. Mimi pia nilimtambulisha kwa wazazi, ndugu na marafiki zangu.

Mwezi wa tatu mwaka huu, mrembo wangu alipata shughuli nzuri inayolipa mkoani, kwa ushauri wangu nilimuomba aende. Mawasiliano yetu akiwa huko yalikuwa mazuri hakukuwa na shida kabisa. Wiki iliyopita, alinitaarifu kuwa atakuja huku ili kumpokea mgeni ("ndugu") wake aliyekuwa ughaibuni kamaliza masomo anarudi home. Nilifurahi kwa ujumbe huo kwani nilimmisi mrembo wangu na pia nilipenda kufahamiana na "ndugu" yake.

Aliniambia hatafikia kwangu bali hotelini atakapofikia mgeni wake. Nilimsihi sana yeye na mgeni wake wafikie kwangu lakini aligoma. Alikuja kwangu asubuhi na kisha aliniaga kuwa ataenda uwanja wa ndege kumpokea mgeni. Kwa vile ndege ilikuwa inatua mchana, sababu ya kazi, nilikosa muda wa kumsindikiza uwanjani. Bada ya kumpokea mgeni, alinijulisha kuwa watakuwa hoteli fulani. Aliniambia kuwa simu yake itazima muda sio mrefu na alisahau kubeba charger.

Baada ya kutoka kazini na kupumzika niliamza kumtafuta mrembo wangu lakini simu yake haikuwa ikipatikana. Nikaona isiwe shida, mida ya saa mbili usiku nikaenda katika hoteli aliyonielekeza. Nilizunguka maeneo yote (Restaurant & Bar) sikumuona hivyo nikajipa muda wa kusubiri kwa kupiga mvinyo kidogo.

Nilikaa hapo hadi saa tano usiku nikiwa na matumaini watatokea. Ilipofika saa sita kasoro nikaona ngoja niulize reception. Mhudumu alithibitisha kuwa huyo mgeni yupo chumba namba fulani na yuko na mke wake. Niliomba kwenda kuwaona nikakataliwa. Nilimpa mhudumu mpunga kidogo ndipo aliponikubalia.

Nilipanda ngazi hadi na kwenda katika chumba hicho. Niligonga kwa muda mrefu kidogo ndipo mlango ulipofunguliwa na "ndugu" wa mrembo wangu akiwa kavaa taulo, na mrembo wangu alikuwa kakaa kitandani akiwa kavaa kanga moja😭😭.

Niliwasalimia kisha nikafunga mlango na kuondoka. Pombe zote ziliniisha! Nilipofika nyumbani nilimpigia dada yake simu na kujaribu kuhoji juu ya huyu "ndugu" ya mrembo wangu. Sikumwambia dada wa mrembo wangu juu ya niliyoyaona ila nimtaka aniambie uhusiano wao na huyo "ndugu" wa mrembo wangu.

Dada mtu aliniambia "Ina maana mrembo wako hakukuambia kuwa huyo alikuwa ni boyfriend wake wa zamani waliosoma wote?" Niliishiwa nguvu. Hapa bado sijajua nini cha kufanya japo tayari nimeona isiwe shida huenda Mungu hakutaka niishe naye kama mke wangu.

Sijampigia simu wala kumtumia meseji mrembo wangu na nimeblock namba yake. Najipa muda ili nirudi katika hali yangu ya kawaida kisha nimuombe mrembo wangu aje achukue vitu vyake vilivyopo kwangu. Sina haja ya kuwaeleza ndugu zake kilichotokea.
 
Aisee achana naye, maisha lazima yaendelee
 
Life ain't fair in Love and War
Pole zimfikie, na amekuwa mstahimilivu mno pia, muambie hilo nalo litapita, maisha ni lazima yaendelee!
Cc; twinnie cute b pita hapa!!
 
Sasa hapo yupo njiapanda ya kwenda wapi?

Mbona kama njia ishafika ukingoni, kuna kibao kimeandikwa "dead end"...
 
sijui nitumie wino gani kuandika ushauri hapa.

anyway

kila mtu abebe mzigo wake (yaani pambana na hali yako)
tena shukuru umejionea live.
 
Hii haiwezekani.

Yaani naenda kuchepuka na ninataja hadi eneo la kuchepukia? Si na hiyo simu ningeiacha on tu ili nikuelekeze chumba mwenyewe ukifika unibip nikufungulie mlango?

Urongo.
 
Pole sana mkuu (kwa niaba ya huyo rafiki yako).
Wakati mwingine mtu hata akikutambulisha mtu ni ndugu yake usichukulie kawaida fuatilia ujue ukweli wa mienendo yao. Ukiona ukaribu upo sana na wanajidai wanajaliana sana, simu za mara kwa mara, sijui umeamkaje na blah blah nyingi, jua hizo ni RED FLAGS na usizipuuze kabisa.

Ma ex huwa hawaachani kirahisi, na cha kusikitisha zaidi anaweza kutambulishwa kwako kama kaka na akawa kila siku anakuita shemeji kumbe anazini na mke wako.
 
Life ain't fair in Love and War
Pole zimfikie, na amekuwa mstahimilivu mno pia, muambie hilo nalo litapita, maisha ni lazima yaendelee!
Cc; twinnie cute b pita hapa!!
Twinnie asante kwa kuniita.
Nimeshatia neno hapo juu.
Nimejifunza pia, sio kila nitayetambulishwa ni wifi nimwamini. Nitafuatilia hadi mawifi.
 
Twinnie asante kwa kuniita.
Nimeshatia neno hapo juu.
Nimejifunza pia, sio kila nitayetambulishwa ni wifi nimwamini. Nitafuatilia hadi mawifi.
Haha..!!
Hapo pa mawifi umenichekesha, ifike pahala mtu ukuwe FBI Agent kwanza kabla ya kusema 'yes I do'..!!
 
Haha..!!
Hapo pa mawifi umenichekesha, ifike pahala mtu ukuwe FBI Agent kwanza kabla ya kusema 'yes I do'..!!
U FBI unaendelea hata baada ya "yes I do" unaweza tambulishwa mke mwenzako kama wifi ujue, na akawa anakuja kukutembelea kama wifi na kukufulia nguo.
Usiku mume anakutoroka anaenda chumbani kwa wifi wanafanya yao wewe upo tuu unajisifu umepata wifi mzuri hana gubu hadi nguo anakufuliakumbe mwenzako anajua anafanya nini.
 
Dah mkuu imeniuma saana hivi mijiwanawake ipoje? kwanza nitafute pesa tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom