Yu wapi Bi Naila Jidawi...?

Yu wapi Bi Naila Jidawi...?

The Fixer

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Posts
1,365
Reaction score
596
Wakuu wa JF,

Naulizia tu kwa kujikumbusha historia ya siasa ya Zanzibar kidogo. Yu wapi Bi Naila Jidawi ? Bi mkubwa mwenye makeke sana katika harakati za chama cha CUF kule visiwani Zanzibar

Naomba tu kuweka kumbukumbu sawa kwa kusema mie nlianza kumfahamu huyu Bi mkubwa miaka ya 1994 nlipokuwa Mgambo Jkt kwa kupitia luninga ya TV ZANZINAR yaani TVZ channel kule Mgambo tulifunga antena ndefu sanaa

Sasa huyo Bi mkubwa Naila Jidawi kipindi kile ndio ugomvi wake na Maalim Seif uko juu sanaa , Nnachokumbuka ni kuwa Maalim Seif hakuthamini hata kidogo mchango wa Bi mkubwa huuyoo ambae alitoa nyumba yake kuifanya ofisi na mwisho wa siku Maalim Seif akamfukuza kwenye chama....

Wadau wenye kumbukumbu zaidi, hebu fungukeni zaidi....

Huyu Bi mkubwa ndio anafaa kuwa Rais wa kike ajaye kwa Zanzibar na huku bara tukiwa na Makinda yetu....
 
Hata Mapalala walimfukuza. Hizi siasa za vyama vya magumshi ni TOO RISKY, ndio maana Dr. Slaa kasema ahakikishiwe fungu lake in advance.
Afadhali Nimeianza siku yangu na kicheko......eti "Hizi siasa za vyama vya magumshi ni TOO RISKY, ndio maana Dr. Slaa kasema ahakikishiwe fungu lake in advance". Wamuulize Mrema (Lyatonga)alivyopigika kwa kuingia kichwa kichwa NCCR- Mageuzi.
 
Hata Mapalala walimfukuza. Hizi siasa za vyama vya magumshi ni TOO RISKY, ndio maana Dr. Slaa kasema ahakikishiwe fungu lake in advance.
Mkubwa,

Una uhakika na unachokinena hapa?
Lini Dk. Slaa alisema hivyo?
Hizi Sasa Ndio Siasa za Majitaka, Siasa za kupakaziana uongo!!
 
Hata Mapalala walimfukuza. Hizi siasa za vyama vya magumshi ni TOO RISKY, ndio maana Dr. Slaa kasema ahakikishiwe fungu lake in advance.

mkuu ZeMarcopolo
Umaniacha hoi sana sasa huyu slaa anafanya kazi Chadema kama TX au mtetezi wa wanyonge? Nachelea Chadema wasije wakamuajiri Odinga maana kama mtetezi wa wanayonge anajipangia mshahara na marupurupu sasa hapo anatetea wanyonge au anatetea nafsi yake? Nimepitia majarida mengi ya historia sijakutana na mtetezi wa wanyonge anayetetea kwa kuwakamua wanyonge!
 
Last edited by a moderator:
Mkubwa,

Una uhakika na unachokinena hapa?
Lini Dk. Slaa alisema hivyo?
Hizi Sasa Ndio Siasa za Majitaka, Siasa za kupakaziana uongo!!

Kamanda mbona unataka kuleta majadiliano wakati majibu yote unayo!
 
mkuu ZeMarcopolo
Umaniacha hoi sana sasa huyu slaa anafanya kazi Chadema kama TX au mtetezi wa wanyonge? Nachelea Chadema wasije wakamuajiri Odinga maana kama mtetezi wa wanayonge anajipangia mshahara na marupurupu sasa hapo anatetea wanyonge au anatetea nafsi yake? Nimepitia majarida mengi ya historia sijakutana na mtetezi wa wanyonge anayetetea kwa kuwakamua wanyonge!
Tatizo la Slaa anahisi kwamba kuna sehemu fulani ya maisha yake aliikosea, sasa kama vile anataka kucatch up. Katika kufanya hivyo ndio anajikuta wakati mwingi anafanya uhuni usioendana na umri wake. Age mates wake kina Kingunge na malecela sasa hivi wameshastaafu...
 
mkuu mbona mada haijataja dr Slaa? inazungumzia Zanzibar na Jidawi sasa hayo ya Slaa umeyatoa wapi. Chadema wanawatesa sana nyie ndugu,mtakufa na presha kwasababu ya Chadema wakati wenyewe wanakula bata.
 
mkuu mbona mada haijataja dr Slaa? inazungumzia Zanzibar na Jidawi sasa hayo ya Slaa umeyatoa wapi. Chadema wanawatesa sana nyie ndugu,mtakufa na presha kwasababu ya Chadema wakati wenyewe wanakula bata .
Ni kweli, Slaa anakula sana bata na pesa za Chadema.
 
Ina maana hatuwezi kuzungumzia Siasa kila uzi bila kumtaja Dr Slaa na Chadema jamani.....??

CUF , BI JIDAWI NA MUSTAKABALI WA SIASA ZA ZANZIBAR.....!!
 
Zilongwa mbali zitendwa mbali! Mtoa hoja kauliza kuhusu Bi Jidawi,kwanini vichwa vyetu vinakuwa vigumu kuelewa mada husika? Au ndo madhara ya UTANZANIA wenyewe?
Ok mi nakumbuka mara ya mwisho huyu mama alituhumiwa kuhujumu chama chake kwa kushirikiana na CCM,akafukuzwa na nadhani pia ilileta mtafaruku bungeni manake CUF waliwasilisha kwa spika (Msekwa) barua ya kumfukuza ili pia bungeni asihudhurie lakini spika akagoma na Jidawi akaendelea kuhudhuria,baada ya lile bunge kuisha sijajua kilichoendelea,But alikuwa mwana mama ngangari kwenye medani za CUF at that time.
 
Alipata kuwa mbunge CUF na kuwa mgombea mwenza wa NCCR Mageuzi 2005 chini ya dk. Mvungi lakini kwa muda mrefu sijapata kumsikia tena. Kwa yeyeote mwenye habari yake atujuze.
 
Dah! nakumbuka sauti yake yenye ushawishi. Masikini CUF jamani!
 
mkuu wacha Damu changa ziwaze sasa, umenilkubusha huyu mama alikua Lawyer mahiri Bungeni
 
Yuko huku zenj kajaa tele kama pishi ya mchele.

Anajishughulisha na biashara nafkiri anamiliki hotel shamba.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom