Your sad moments in 2012

Your sad moments in 2012

moto2012

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2012
Posts
2,309
Reaction score
1,552
Khabari za asubuhi wanajmvi wenzangu!
Leo ndo siku ya mwisho ya mwaka 2012, na Allah akitujalia kesho tutaanza mwaka mpya.

Huzuni na furaha vyote kaumbiwa mwanadamu, ni kama pande mbili za shilingi.
Ninavyoamini mimi, kila tukio fulani la huzuni linalonipata basi kuna jambo flani kwalo napaswa kujifunza au kuna pahala nilichemka kufanya decision.

Wapo walioondokewa na wapendwa wao The Boss Madame B na wengine, wapo ambao ndoa hazikwenda vizuri Wiyelele na wengine, wapo walopata majanga tofauti tofauti, kama wanafamilia tushrikishane kwa ufupi sana tukio/matukio yalokhuzunisha sana 2012, na unamuomba Allah akuepushie 2013.

Binafsi sitaisahau March 26, 2012, nilimpoteza baba yangu Kipenzi, R.I.P Dady

Karibuni tufarijiane na tukumbushane pia tuombeane 2013 iwe salama kwetu....
 
Last edited by a moderator:
Hebu acha ujinga watu wameshaanza kusahau mambo yaliyowakuta wewe ndo unaanza kiwakumbusha.
Binafsi sijapendezwa na fikra zako juu ya hili, unataka watu waanze kukosa raha tena na kusononeka mioyoni mwao sababu yako. Kama huna chakufanya lala usingizi.
 
Kwanza nashukuru kwa mada hii si mbaya kukumbuka ulikotoka na kumshukuru Mungu kwa jinsi alivyokuvusha,pole sana kwa kumpoteza baba yako Bwana ametoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.Nami sitaisahau tarehe 11.02.2012 saa11 nikiwa KCMC nilimpoteza Baba yangu mpenzi,nikishuhudia kwa macho yangu jinsi baba yangu akimaliza safari ya mwisho kwa mateso makubwa kutokana na ugonjwa ulokuwa unamsumbua,dah! Iliniuma sana sikuwahi kuwaza ingenitokea hivyo tena mikononi mwangu, niliumia zaidi kwan nikitafakar sijarudisha bado matunda kwake kwa kunilea,yaan ndo naanza tu safar ya mafanikio ndo na yy anatoweka,iliniuma zaid siku ya harus yang mwez wa nane nilipokuwa simuon.Lakini ktk yote hayo namshukuru Mungu amenipa amani ya ajabu sijawahi kuiona maishani mwangu,sina uchungu tena moyoni mwangu japokkuwa kila siku namkumbuka lakini si ktk hali ya uchungu,leo asubuhi nikiwa nasal nikajikuta nakumbuka ktk meng Mungu aliyonishindia nikajikuta namshukuru Mungu sana na Kusema HAIKUWA JAMBO RAHISI, kwanini nasema hivyo mie kwetu ni kifunga mimba na ktk watoto wote peke yangu ndo niliyekubal shule na kufika mahali angalau baba alipokuwa anataman wanawe tufike kutokana na hilo liliniweka karibu sana na baba yangu.Mwisho nasema HAIKUWA JAMBO RAHISI kufikia hapa tulipo wana JF ila ni kwa NEEMA YA MUNGU TU,Poleni wote mlofikwa na mabaya AMANI YA MUNGU IPITAYO FAHAMU ZOTE IWAJAZE MIOYO YENU,Mungu atulinde tumalize vyema na tuanze mwaka vyema na kwa upya zaidi.Mungu awabariki wote.
 
Inshallah mwenyezi mungu atupe mwaka 2013 wenye kheir na baraka...
 
so saaaad brother... Kudra za mungu hizo... Umenigusa sana.... ungu akufanyie furaha siku za mbele... Muombee sana dua mzee na ndugu zako waliotangulia...
 
Pole sana kwa kufiwa na baba yako mpenzi.

Aaa mimi sikumbuki mabaya nakumbuka mazuri tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom