Mtemi Mojo
Member
- Dec 17, 2017
- 39
- 44
Nikiwa nyumbani weekend nacheza na wanangu, mawazo juu ya mustakabali wao na nchi yao yakawa yananiijia. Ni wazi Taifa letu bado liko nyuma kimaendeleo lakini cha muhimu ni kuwa bado lipo.
Ninacho jiuliza ni je? Taifa lao Hawa watoto wetu litakuaje, na cha msingi kabisa Litakuwepo?
Naomba tusichanganye Nchi na Taifa,
kama nchi najua itaendelea kuwepo, kutakua na changamoto dhahiri kama za kuongezeka kwa msongamano wa magari, gharama za maisha, madhara yasababishwayo na mabadiliko ya tabia nchi nk. Lakini Nchi hii itakuepo hata kama itabadilika jina lakini nitakuwepo.
Ni muhimu sana kukumbuka kuhusu vizazi vijavyo tukiwa tunaendelea kutukanana, kugombana na kuitana wasaliti. Tukumbuke sisi sote tutapita, pamoja na hao wanaofanya tuchukiane, tutapita. Lakini kila tunachofanya sasa ni mbegu itakayomea na kuota miaka mingi baada ya Historia yetu kufutika katika dunia.
Pamoja na kuwarithisha wanetu Nchi yenye afya, tujielekeze pia katika kulinda utaifa wetu. Tunaweza haribu nchi (kwa ufisadi, Sera mbovu, kukwepa kodi, kuwachekea na kuwalea wahamiaji haramu nk), badae ikatengenezwa. Ila gharama ya kujenga Taifa watoto wetu hawataimudu.
Simaanishi tuwe taifa lisilohoji mambo, au waogawaoga la hasha. Namaanisha tuwe watu wanaojenga hoja, wanaohoji kwa hoja, wasiosaliti misimamo yao kwa ujira (pesa au vyeo), wasiokuwa wepesi kukosoa hata mambo ya msingi kisa kimefanywa na upande asioupenda, wasiotuhumu kwa kuwa kiongozi wao ametuhumu, wanaofikiria kuhusu Tanzania ya Leo na ya vizazi vijavyo.