Yote Kuhusu Magonjwa Ya Zinaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yote Kuhusu Magonjwa Ya Zinaa

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Aug 14, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Magonjwa ya zinaa ni nini?


  Ni maambukizi ambapo virusi, uchafu, bacteria na vijidudu hupitishwa kupitia uhusiana wa karibu wa kujamiiana. Huu mwingiliano huhusisha sehemu za siri, mdomo na ******. Maambukizi mengine hutibika kwa urahisi lakini mengine hayatibiki kama vile Ukimwi – huweza kutibiwa lakini hauponi. Kuna zaidi ya magonjwa 20 ya zinaa. Baadhi ya yale yanayojulikana sana ni; Ugonjwa wa ngozi na vilenge lenge, Chlamydia, kisonono na kaswende. Wale ambao wanaugua magonjwa ya zinaa wana nafasi kubwa ya mara tano kuambukizwa ugonjwa wa Ukimwi iwapo kupitia kwa ngono.

  Jua dalili

  Utajuaje iwapo umeambukizwa ugonjwa wa zinaa? Hutegemea ni ugonjwa gani wa zinaa. Kuna dalili zingine ambazo hutokea na kuonekana haraka. Hizo dalili ni pamoja na;

  Kutoka vitu visivyo vya kawaida kwenye sehemu nyeti, kuhisi maumivu unapokojoa, uvimbe, wekunduwekundu au ugumugumu kwenye sehemu zako za siri. Dalili hizi hutofautiana kwa wake na waume. Maambukizi kama yale ya ugonjwa wa Ukimwi yanaweza kukua mwilini kwa miezi sita ndipo yatambulikane. Ukigundua dalili zozote, muone daktari mara moja na usiendelee kushiriki ngono hadi pale ambapo utakapopata matibabu.

  Jambo lililo muhimu sana ni kuzuia

  Epukana na shida za kisakolojia, kimwili na kifedha zinazoambatana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa kwa kujihusisha na ngono aminifu na salama. Unataka kujizuia kuwa asilimia 100%? Usijihusishe kabisa na ngono. Pata mpenzi mmoja mwaminifu. Iwapo umeamua kushiriki ngono, basi jikinge kwa kipira kila wakati unapojamiiana na mtu hasa wakati ambapo huna mpenzi tu mmoja mwaminifu. Ni muhimu ujue historia ya kingono ya mshiriki wako. Chunguza iwapo wewe tu ndiwe mshiriki wake wa kipekee anayejihusisha naye kwa ngono. Kwani kadri mtu ana washiriki wengi, ndivyo kadri alivyo na nafasi kubwa ya kupata magonjwa ya zinaa. Kuwa makini, jihadhari, jifanyie uamuzi na ulipe kipa umbele, kama
   
Loading...