monotheist
JF-Expert Member
- Apr 30, 2017
- 887
- 1,596
Habari wajuvi,
Kuna ndugu yangu anataka aagize charger kutoka aliexpress ila hana sanduku la posta hivyo anataka atumie post code ya makao makuu hapa Dar
Je post code ni ipi na ofisi inapatikana wapi hapa Dar?
Hizi huwa hazifanyi kazi.Ingia web ya TCRA kuna postal code za TZ nzima
Nimeingia ila sielewi naona manamba tu!!Postal and ZIP Code database
Postal and ZIP Code database Postal code - ZIP codes. Download zipcodes listing by countries. Buy postcodes of the world. International zip code database. PIN codes list.www.geopostcodes.com
Habari wajuvi,
Kuna ndugu yangu anataka aagize charger kutoka aliexpress ila hana sanduku la posta hivyo anataka atumie post code ya makao makuu hapa Dar
Je post code ni ipi na ofisi inapatikana wapi hapa Dar?
Utaona manamba ila hayajaanza kufanya kazi hapa TZ yanaandaliwa kama beacon za barabara siku yakianza mtakuwa mmeshajifunza. Nakumbuka zamani miaka ya 2006 kabla sijazijua nilikuwa najaza 255 kumbe siyo. Hizo ni anuani za makazi unaletewa mzigo hadi nyumbani. Badala la ya posta. Nakushauri utumie sanduku la posta halafu kwenye Zip Code jaza 0000 badala ya namba halisi ili wajue kwamba hazitumiki maeneo yako.Nimeingia ila sielewi naona manamba tu!!
😂😂😂Zile chaja ndefu sana kama kamba ya mbuzi nimeiagiza nasubiri wadeliver
AhsanteNdugu postal code ya makao makuu ya posta haitakusaidia mzigo wako ukufikie.
Inabidi ujue postal code ya mtaani kwako kisha na namba ya nyumbani keqko.
Au post code ya mtaa wa ofisini kwenu na namba ya jengo na namba ya chumba cha ofisi yenu.
Mfano kama upo pale CRDB Azikiwe na block namba yake 3, 3rd floor, postcode ya Azikiwe ni 11101 utaandika ifuatavyo:
To
John Walker,
CRDB Azikiwe Branch,
Room No 103, 3rd Floor, Block No3.
Azikiwe Street.
Post code 11101 Kivukoni.
Dar es Salaam, Tanzania.
Kama nyumba ya kawaida huko Sinza.
To
John Walker,
Plot/House No 34
Palestine Street.
Post code 14114, Sinza A,
Kinondoni,
Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa kuijua post code ya mtaaa au kijiji chako tembelea http://tcra.go.tz huko kuna syst3m inaitwa NAPS. Kuna maelekezo na pia kuna PDF ya postal code TZ yote.
Au tafuta Yellow Pages Ltd Telephone Directory ya 2016/2017.
Wilaya, KinondoniUnataka mzigo wako ukufikie wapi nikupe post code yako?
Nitajie Mtaa kwa mijini au kijiji kwa vijijini.
Pia nitajie kata(ward) na Wilaya.
Hii ni ya wapi mkuu?11000
Tumia hiyo hapo chiniAhsante
Ila kuna baazi ya wadau wanadai unaweza ukaudirect mzigo ofisi kuu ya posta mzigo ukifika wanakupigia simu ila sifahamu posta code yao
Sio kweli mkuu.11000
Pamoja mkuuTumia hiyo hapo chini
Posta House, 7 Ghana street, P.O. Box 9551, 11300 Dar es Salaam,
Tanzania.
Hiyo 11300 ndio post code ya posta HQ.
Usisahau kuweka namba yako ya simu ili wakupigie.Tumia hiyo hapo chini
Posta House, 7 Ghana street, P.O. Box 9551, 11300 Dar es Salaam,
Tanzania.
Hiyo 11300 ndio post code ya posta HQ.