Yericko Nyerere aache upotoshaji

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,874
Nilisema Mimi ni mwana Demokrasia nina amini katika umoja na mshikamano "unity" and "Solidarity" katika jambo lolote.

Hata katika umoja wa vyama vya siasa hasa upinzani ,naamini katika umoja huo ,ndio maana mara zote huwa napingana na anayejiaribu kwa makusudi kuleta mgawanyiko huo.

Tujikumbushe tena maneno
aliyoyasema Kiiza Bisyege wa Uganda "The Opposition biggest challenge is disunity in leadership,the unity of the opposition is the biggest threat to regime ,the regime also works overtime not just 27/7 ,to ensure that unity does not happen " maana kwa ufupi ni kuwa mshikamano wa vyama pinzani ni tishio kwa watawala ,hivyo watawala kupambana sio tuu masaa 24 ya siku 7 kuhakikisha kuwa mshikamano huo hautokei.

Kuna njia nyingi za kutumia ili kuvuruga mshikamano huo ,hata kutumia watu au viongozi hao hao walio katika vyama hivyo pinzani.

Kaka yangu Yericko Nyerere amekuwa kinara,mpotoshaji,na mwenye kuandika taarifa zenye lengo la kuhatarisha umoja na mshikamano kati ya ACT wazalendo na Chadema .Hii imeanza punde tuu baada ya Maalim Seif kuhamia ACT aliapa mbele ya umma kutumia maandiko yake kwa namna awezavyo,kiapo hiki anajua fika siku alichokitoa.

Na amekuwa akiandika mfululuzo ,anajua kama watu baadhi wanavyojua kuwa anatumika na ndio maana maandiko yake yote ni ya kutunga,uongo,kwa lengo la kupotosha umma ili atimize lengo la mission aliyokabidhiwa kuvuruga mshikamano kati ya ACT wazalendo na CHADEMA.

Leo Asubuhi ameamka kuanza kusambaza uongo kuwa Gazeti la Chamvi la habari ni la ACT wazalendo.Nitajibu uongo wake kabla naomba na tujifunze kuhusu taarifa za uongo(False information) za Yericko Nyerere ili siku nyingine zipuuzwe.

Unayesoma ,naomba utafute kitabu cha SRIJAN KUMAR na NEIL SHAH kinaitwa *False information on web and Social Media* .Taarifa yeyote ya uongo imegawinyika sehemu kuu mbili .(1) Lengo au dhumuni (Intent) (2)Ufahamu (Knowledge),Yeriko katika taarifa zake za uongo ana lengo (intent) lake,na lengo/intent hugawanyika sehemu mbili,Disinformatio na Misinformation. Yericko ana nia kufanya Disinformatio kutoa taarifa za uongo kwa umma ili kutimiza adhima na malengo aliyopewa ya kuleta mgawanyiko kati ya ACT wazalendo na Chadema.

Pia taarifa ya uongo ina upande ungine wa ufahamu (knowledge),hapa katika ufahamu imegawanyika pande mbili (1) Opinions based false information yaani taarifa ya uongo kwa kutoa maoni na mawazo yako kwa kutumia hata fake reviews (pili ) fact based false information ,yaani unatumia facts kama kuonesha ukweli ila wakati uongo.

Sasa Kaka yangu yeriko katika nia (intent) ya maandiko yake anatumia Disinformatio,yenye lengo la kudanganya umma(intent to deceive) ili agenda na mission zake zipate aminika na Umma ili kutiza lengo lake la kuvuruga umoja. Katika ufahamu (knowledge) anatumia opinion based false information yaani maoni yake na fikra zake za uongo na uzushi anavyo waza ,ndio maana mara zote anatumia fake reviews, anonymity (watu bila majina ) ,Lengo lake ni kuleta mgawanyiko kwa vyama pinzani.

*HOJA YAKE YA LEO KUWA JAMVI LA HABARI NI GAZETI LA ACT-WAZALENDO DHIDI YA CHADEMA*

Katika muendelezo wa nia yake ya kuleta mgawanyiko kwa ACT na Chadema leo Yericko Nyerere amekiri kusema Gazeti la Jamvi leo ni la ACT -wazalendo dhidi ya Chadema.

Jamani taarifa yake aliyoitoa ,najibu hapa kwa lengo la kuondoa upotoshaji wake na kuepuka nia yake ovu ya kuleta mgawanyiko kwa vyama pinzani (ACT na CHADEMA).

Yericko anasema Gazeti la Jamvi lilisajiliwa kipindi key person akiwa bado yupo CHADEMA (anamjua yeye huyo key person ,hi ni dalili ya taarifa za kutunga),aliyetoa ushauri kusajili Gazeti hili ni anayejulikana kama shangazi na mkimbizi wa mmoja huko Uskochi(hakutaja majina hi ni dalili ya taarifa za kutunga hana ushahidi anaogopa kuombwa ushahidi).Eti walishauri kuwa ili chama kipya kifanikiwe lazima kiwe na *GAZETI LAKE*

Tuelewane neno *Gazeti lake* ina maana kuwa ACT ilishauriwa iwe na GAZETI lake ,Gazeti la chama ,kwa mujibu wa maelezo ya Yericko.

Yeriko akaendelea sema kuwa "baada ya Gazeti hili kuundwa ,likasimamiwa na Habibu Mchange Kama Mkurugenzi wa Gazeti hilo na mhariri msaidizi Khamis Abdallah ambaye ni Afisa habar wa ACT ,Baada ya key person kuondoka Chadema,Gazeti hili likayumba kifedha ,Habibu Mkurugenzi akataka kuliuza mil 5 , ikashinda kwamba Mchange akakaa na key person wakakubaliana aondoke ACT akatafute fedha ya kuendesha Gazeti , System ikachukua mkondo kuanza kulitumia Gazeti hilo kuchafua *wapinzani* "

Akaendelea kusema "Gazeti hilo hadi Sasa linatumika dhidi ya Chadema ,na Mhariri msaidizi ni Abdaah Khamis,wanaokoteza habari zangu huko fb wanaandika katika Gazeti ,na Gazeti hili lilitumika kumfunga Mbowe ndio lilionesha Ticket ya ndege,Ruti,picha aliyopia ubelgiji"

Yericko Nyerere una aibisha jina la *Nyerere*,jina hili ni kubwa,usingeitwa hivyo tuu.

HOJA zake za kutunga.

1.Anasema kuna watu walishauri,Chama kiwe na Gazeti lake ,Jamvi la habari likasajiliwa ,hivyo lilikuwa la chama sio la mtu ,Kama lilikuwa la chama kwanini ,Mchange alivyondoka ACT akaondoka nalo na likageuka kuendelea kushambulia ACT wazalendo , viongozi wake na hata vyama pinzani vingine huku likitete Watawala ? Kama kweli Gazeti hilo ni la ACT wazalendo.

Anasahau anachoandika Mchange katika Gazeti hilo ni maudhui ya wadhamini .(Sponsored contents) analipwa fedha na wadhamini wake ili kuandikia watawala ,(soma udhamini katika uandishi/uhariri )kuna dhamini wa nguvu ,wa ushawishi,na wa dola Mchange anafanya kazi za watu kujiingizia fedha kwa udhamini wa maudhui dhidi ya wapinzani,Sasa iweje Gazeti la ACT lifanye kazi ya kushambulia ACT na wapinzani wengine?

2.Yericko anasema kuwa Mhariri Msaidizi wa Gazeti hilo ni Khamis Abdallah ambaye ni Afisa habar wa ACT ,na anasambaza na kipande cha karatasi cha Jamvi kuonesha namba na jina kuwa anahusika.

Jina katika kipande hiko cha Gazeti ni Abdallah Abdallah , wakati huyo Abdallah Afisa habari wa ACT anaitwa Abdallah Khamis Kombo,haya ni majina mawili tofauti !

Pia kwa uwazi Abdallah Khamis alikuwa mhariri wa Jamvi siku nyingi tangu Mkurugenzi wa Gazeti hilo akiwa bado yupo ACT ,sasa hivi Abdallah Khamis hayupo tena Jamvi la habari, Sasa Yericko anasambaza kikaratasi hiko cha Gazeti bila kujua kuwa Gazeti hilo ni la mwaka gani,bila kujua kuhusu utofauti wa majina hayo.

Anasema kuwa Gazeti hilo ndio lilifanya dhamana ya Mh.Mbowe ifutwe mahakamani,iliandika kuhusu Tickets,Ruti,picha za ubelgiji za Mh.Mbowe na hivyo sababu Gazeti hilo ni la ACT basi walifanya kuandika ili Mh.Mbowe afutiwe dhamana.

Hivi Yericko anafanya watu mazuzu ,ACT wazalendo inufaike na nini dhamana ya Mh.Mbowe kufutwa? ,ACT wazalendo ina mamlaka yapi ya kuandika habari Jamvi ikiwa wadhamini wa Habibu Mchange(Mkurugenzi) wanajulikana?, ACT wazalendo ilipata wapi habari za safari ya Mh.Mbowe hadi Tickets zake ikiwa wewe ndio Muandamizi wa karibu wa Chadema na viongozi wake ?

Kama andiko lako liliwezwa andikwa Jamvi la habari na inajulikana ni kwa matakwa yako ,sio kwamba waliandika tuu sababu pia Mkurugenzi wa JAMVI Habibu Mchange alikuwa anasambaza andiko lako whastsp ,unawezaje sema waliiba Facebook,sasa Kama yote haya yanawezekana kweli inashindikana ,vipi siri za Tickets,picha na safari ya Mh.Mbowe ubelgiji zisijulikani na Gazeti la Jamvi ? Usijiulizi kwanini Gazeti la Jamvi liliandika habar ya Mh.Mbowe hadi kufutiwa dhamana,Jiulize Gazeti hilo lilipata taarifa hizo wapi ?

Najua wajua kuwa wapo wanachama na viongozi baadhi wa CHADEMA wapo karibu na Mchange na mara kwa mara huenda ofisi kwake ofisi ya Gazeti hilo,najua viongozi wakuu wachadema wayaone haya ili kuepuka mgawanyiko.

Lengo sio kuleta mfarakano lengo hapa ni kudumisha umoja na mshikamano,hivyo Yericko Nyerere acha kupotosha umma kwa maslahi yako na wengine wanaokutumia Kaka yangu.

Viongozi wako wote wajuu wanajua nini maan ya mshikamano ,ndio maana wapo imara na hushirikiana vyema na vyama vingine ila wewe hujui sababu upo kazini.

Kwanini maandiko yako dhidi ya ACT yameanza baada ya Maalim kuhamia ACT ? kwanini sio kabla ,jibu ni kuwa YERICKO NYERERE upo kazini kuhujumu mshikamano wa vyama pinzani hasa ACT na CHADEMA .Endelea na kazi yako,Kazi njema ila watu wanajua.

Abdul Nondo.

Abdulnondo10@gmail.com

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SHIKAMOO kIJANA. HAWA NDIYO VIJANA KAMA HAWATAAMBUKIZWA VIRUSI VYA KINA NAPE MBOYA ZITTO KIBAJAJI TAIFA LITAKWENDA MBELE
 
Dogo kwanza kajifunze kuandika kiswahili fasaha ndipo urudi kutuletea bandiko lako.

Pili, haujakanusha hoja hata moja ya yeriko bali umeishia kutuletea theories tuu hapa namna ya kutambua false informations.

Tatu, ni kweli viongozi wa hilo gazeti wapo karibu sana chama chenu cha ACT kwa hiyo iko wazi kabisa wanaandika taarifa za kukinufaisha chama chenu.

Kwenye bandiko la yeriko kati ya picha 3 alizozituma kuna kijana kasimama na hao wahariri ambaye ACT mnamuandaa kuja kugombea jimbo la Singida magharibi.

Kanusha na comment hii nikuletee na nyaraka kabisa.

Over.
 
Wanasema mchawi ndiye hulia sana Msibani! Naendelea kuunganisha Dots za mpambano wenu. Ila niseme hili wote mpo level moja ya utumikaje kwa mabwana zenu na mnakijua mnachokifanya kuwahadaa WaTz.
 
Sasa mdogo wangu Nondo, unaongelea gazeti halafu unanukuu kitabu cha mhindi Srijan Kumar ili utuchoshe tu wasomaji! Kwa nini usiende direct to the point? Ana u 'guru' gani huyu unayemnukuu hadi ku deserve recognition????

Angekuwa Maheshwari (nguli wa finance) au Chand (nguli wa Physics) sawa

Yawezekana kabisa unamnukuu mtu wa nje mwenye akili kama ya Cyprian Musiba

Jifunze ku summarize

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Abdul Nondo naona unavimba kichwa sasa. Wakati akina Yericko wanailinda Chadema kwa jasho na damu sijui kama ulikuwa hata unajielewa.

Pamoja na mapungufu ya Yericko lakini kuwa na adabu, umeandika maelezo marefu unnecessarily kwa jambo lililohitaji short statement. Naona unaota sharubu na kujibizana bila adabu kwa kaka zako.

Nyie wote mnatumika na wanasiasa hakuna cha uzalendo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Abdul Nondo na Yericko kila mtu anatetea chama chake. Abdul anatetea ACT, na Yericko anatetea CHADEMA. Ila sasa we Nondo uwe unajibu hoja hapa kwenye comment kama Yericko anavyojibu. Kazi ya kutuandikia alafu unakimbia kujibu, hiyo ni ishara ya kutudharau. Inakuwa kama unatupa muhadhara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku ukijua kuwa Yericko alikuwa sahihi hili andiko lako litakusuta.

Tafuta uhusiano wa Jamvi la Habari, Tetere Media na ZZK na Habib Mchange.

Unaonekana bado mdogo sana kuelewa na kuchanganua baadhi ya mambo.
 
Dogo kwanza kajifunze kuandika kisawahili fasaha ndipo urudi kutuletea bandiko lako.

Pili, haujakanusha hoja hata moja ya yeriko bali umeishia kutuletea theories tuu hapa namna ya kutambua false informations.

Tatu, ni kweli viongozi wa hilo gazeti wapo karibu sana chama chenu cha ACT kwa hiyo iko wazi kabisa wanaandika taarifa za kukinifaisha chama chenu.

Kwenye bandiko la yeriko kati ya picha 3 alizozituma kuna kijana kasimama na hao wahariri ambaye ACT mnamuandaa kuja kugombea jimbo la Singida magharibi.

Kanusha na comment hii nikuletee na nyaraka kabisa.

Over.
Bado hoja za Yericko hazijajibiwa...... Still Yericko yuko juu. Nimefuatilia hili gazeti ni la kusifu ACT na kuponda CHADEMA

Cha kufanya ni gazeti lijirekebishe na Yericko aendelee kufukumua zaidi for the betterment of opposition

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom