Yawaje mtu asionwe wakati yupo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yawaje mtu asionwe wakati yupo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtambuzi, Dec 30, 2009.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Dec 30, 2009
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kwa kawaida huwa tunajidanganya na kudhani tunajua mengi sana kuhusu maisha au yote kuhusu maisha, wakati ukweli ni kwamba tunayoyajua ni yale kidogo tu ambayo tumekutana nayo au kujifunza maishani. Mara nyingi mtu anapozungumzia nguvu fulani zilizoko kwenye dunia hii au ulimwenguni anaweza kuonekana kituko.

  Hebu soma habari hii ya kweli ambayo imewahi kuandikwa kwenye vyombo mbali mbali vya habari huko Ulaya siku za nyuma.

  Peter wa Gloucestershire huko Uingereza alipatwa na jambo lenye kushangaza sana mwaka 1987. Akiwa katikati ya sherehe ya jamaa yake mmoja alishikwa na haja ndogo.
  Aliamua kwenda kujisaidia maliwatoni. Nyuma yake kulikuwa na mwanamke aliyekuwa anelekea huko huko maliwatoni {kumbuka sherehe ilikuwa nyumbani ambapo vyoo havikutengwa vya wanawake na wanaume}

  Peter alijisaidia haraka na kutoka ili huyo bibie naye akajisaidie. Alimsalimia wakati anatoka ****** baada ya kujisaidia, lakini yule mwanamke hakuitikia. Kwa Peter halikuwa ni jambo la maana sana na hakulitilia manani. Alienda zake sebuleni ambako muziki na vinywaji vilikuwa vikiendelea. Alipofika hapo alienda kukaa kwenye meza ambapo rafiki zake walikuwepo.

  Alipokaa alichukua kinywaji chake na kuanza kuzungumza na hao rafiki zake. Lakini hao rafiki zake walionekana kumpuuzia. Kila aliposema wao hawakumjibu wala kumtazama, waliendelea tu na mazungumzo yao. Peter alijua wameamua kumfanyia mzaha, hivyo aliamua kunyamaza ili kujua lengo la ule mzaha wao.

  Kwa kuwa alikuwa ameshikwa na hamu ya sigara, aliamua kuinuka na kumfuata bibi yake ili ampatie moto awashe sigara yake. Ajabu ni kwamba, alipofika pale kwa bibi yake na kumnyooshea mkono ili ampatie sigara aliyokuwa anavuta ili awashe yake, bibi yake hakuonekana kujali. Peter alinyoosha mkono karibu na bibi yake huyo, lakini bibie aliendelea kucheza bila dalili kwamba mbele yake alikuwa akiona mtu.

  Peter kuona hivyo alikasirika. Ni mzaha gani wakijinga, aliwaza!Rafiki zake pale mezani wamempuuzia na bibi yake tena anampuuzia, kwa nini? Aliamua kurudi ****** ili ajikague vema, huenda kuna kitu hawataki kumwambia kwamba amechemsha, hasa mavazi.

  Peter anasimulia: Nikarudi ******, kufika namkuta yule mwanamke bado anasubiri pale mlangoni labda akiamini kwamba, labda sijatoka humo. Nilipomuona bado anasubiri, nilikumbuka kwamba, nilipotoka nilimsalimu na hakuitikia. 'Yule mwanamke aligeuka na kuniona. Aliponiona alishtuka sana, 'kumbe umeshatoka wala sikukuona, ningejikojolea nikiwa hapa hapa, 'yule mwanamke alisema kwa mshangao'

  Peter alisema alipoenda tena sebuleni rafiki zake na bibi yake walimuuliza alipokuwa muda wote huo. '****** ndio ukae mwaka mzima?' Walimwambia.
  Anasema, alipowauliza kama ni kweli hawakumwona, walimwambia, hawakumwona. Aliwaeleza kilichotokea na wakabaki wameshangaa.

  Je wewe imeshakutokea hali kama hiyo? Kama bado au kama hujawahi kuisikia , haina maana kama haipo. Hiyo ni hali yenye kuwatokea watu kwa idadi ya kutosha. Tofauti iko kwenye kiwango tu. Wengine huwatokea kwa muda mfupi sana, kama sekunde tano au kumi na wengine hata dakika tano au zaidi, kama ilivyotokea kwa Peter.

  Ni hali ambayo mtu anapoteza uwezo wake wa kuonwa na wengine. Mtu anaamini kwamba wengine wanamuona kama kawaida, wakati wala hawamuoni. Hawamuoni mwili na wala hawasikii sauti yake. Hali hii ambayo kitaalamu hufahamika kama invisibility, huwatokea wengi pengine hata ukiwemo wewe, bali inakuwa vigumu kung'amua kwa sababu unaweza kutafsiri kama dharau.

  Kwa mfano, kuna siku nilikuwa ninampa kondakta wa basi la daladala nauli, nikaona hapokei, bali anapokea za wengine tu. Kuona hivyo nilikasirika sana, na kuacha kumpa. Nilishuka kituo kinachofuata nikiwa nimenyoosha mkono ili achukue pesa zake, lakionoi wala hakunitazama, alikuwa anawadai wengine tu.

  Kwa sababu naijua hii hali ya invisibility, sikushangaa sana, nilitabasamu. Kwa asiyeijua ataitafsiri kwa njia mbali mbali na hivyo hatajua ukweli.
  Kuna wakati mtu anakwenda hotelini, halafu anakuta wahudumu wote wanampita tu , hadi baada ya dakika fulani, kama vile wahudumu wanatoka usingizini ndio wanamwona na kumfuata. Mwingine anaweza hata kufoka, lakini wahudumu wanaonekana hawamjali , kumbe hawamwoni.

  Hivi ni kitu gani kinatokea hadi mtu haonekani? Hilo ni swali ambalo bado halijapatiwa jibu. Lakini, huenda Wajapani watatoa jibu hivi karibuni, kwani wamegundua tayari.
   
 2. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mtambuzi, usemacho ni kweli ingawa kwa upande wangu huwa naichukulia tofauti. Ni kwamba imewahi kunitokea mimi binafsi nakutana na mtu ninayemfahamu kabisa lakini tunapishana bila ya yeye kuniona kiasi kwamba tukikutana muda mwingine nikimwambia tulikutana sehemu fulani naye anashangaa eti hakuniona. But mimi hudhani may be mtu anakuwa na mawazo mengi kiasi kwamba akili yake inakuwa imezama katika kile anachowaza ingawa macho yanaangalia.Hii hali mtu asipokuwa makini anaweza kutafsiri ni dharau lakini hali hizo zipo.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,322
  Likes Received: 22,149
  Trophy Points: 280
  invisibility ni kawaida mbona.
  lakini sijajua haswa hali hiyo husababishwa na nini
   
 4. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hiii habari mpya! Sasa ikitokea mwalimu haonekani ubaoni na yeye kakazana kufundisha si hatari
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Dec 30, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Nadhani hili linatokea kwa sababu watu wanakuwa na mawazo mengi. Unaweza kuwa unatazamana na mtu na kakukodolea macho unamsemesha lakini mawazo yake yanakuwa mbali na wala hakuelewi.
   
 6. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #6
  Dec 30, 2009
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Ahahahahaaaaah! Wanafunzi wanaweza kukimbia kwa kusikia sauti tu na mwalimu haonekani!
   
 7. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2009
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ndio maana hata katika lugha ya kiswahili kuna maneno tofauti KUELEZA utofauti uliopo.

  Unaweza kutizama lakini USIONE; unaweza kusikia lakini USISIKILIZE.
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Apr 13, 2017
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
 9. SAUTI YAKO

  SAUTI YAKO JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2017
  Joined: Jan 25, 2014
  Messages: 2,313
  Likes Received: 754
  Trophy Points: 280
  Inawezekana mkuu ndio maana duniani watu hawalielewi somo LA hisabati inawezekana walimu wa hesabu huwa hawaonekani muda wanaofundisha
   
Loading...