Yatakayojiri CHADEMA baada ya kushindwa uchaguzi mkuu

May 8, 2015
52
30
Chama cha Demokrasia na maendeleo kimeamua kufanya uamuzi wa karne wa kumkaribisha mtu kutoka chama kingine na kumkabidhi dhamana ya kugombea Urais ndani ya siku mbili tu.
Hii inapaswa kuingia kwenye rekodi za dunia maana haijawahi kutokea katika historia ya demokrasia duniani.
Lakini pamoja na uamuzi huu unaofananishwa na kumualika Simba kijijini muishi nae, yako mambo nyeti ambayo wana Chadema hawayajui na watakuja kuyajutia mbeleni, na in fact wameanza:-

1 . Edward Lowasa sio mtu, ni taasisi. Ni taasisi kamili yenye watu walioahidiwa vyeo vyote vya kitaifa kuanzia watendaji wa vijijini, maafisa tarafa, wakuu wa wilaya na mikoa, makatibu wa chama, wajumbe wa bodi mbalimbali n.k.
Lowasa hahitaji wasaidizi wala washauri wa Chadema, ana vyombo vyake atakavyovitumia. Ukiangalia wakati anakwenda kuchukua fomu ya Urais, utamuona mzee mmoja ana mvi anaitwa Chizii, huyu ndiye mshauri wa Lowasa wa mambo ya uchaguzi. Sio mwana Chadema, bali aliingia Chadema siku moja na Lowasa. Leo ni mshauri wa mgombea.Ajabu.
Wana Chadema wasijiroge kuwaza kuwa mipango ya Lowasa itaamuliwa na kamati kuu yao au kampeni zitaratibiwa na Chadema. La hasha.

2. Kitu pekee kinachowaunganisha Chadema na Lowasa ni Urais. Hakuna mfanano wa itikadi, falsafa na hata mfumo wa uendeshaji wa chama. Siku mbili zisingetosha kuleta uwiano huo.Ndio maana Lowasa anaona kinyaa hata kuvaa kombati la Chadema. Tazama picha na video zote, hutamuona na kombati, labda aanze leo baada ya makala hii.

3. Baada ya Oktoba 25 ya uchaguzi mkuu, patakua na Chadema asili na Chadema Lowasa. Lowasa na timu yake wataiteka Chadema. Hapa timu Lowasa, 4u movement n.k ndio watakaobeba vyeo na nafasi za maamuzi zinazoshikiliwa na Chadema asilia. Mfano mkubwa ni Dr. Slaa alivyotolewa sadaka pamoja na jasho lake lote kujenga Chadema. Chezea nguvu ya Lowasa!

4. Lowasa ana kiu ya kutaka mamlaka isiyokwisha hata anywe maji ya bahari.
Atahakikisha anaiteka kamati kuu ya Chadema na vyombo vyote vya maamuzi kwa kutumia nguvu ya pesa vimtumikie yeye. Mbowe,Mtei watajikuta hawana tena uwezo wa kuamuru (command) ndani ya chama. Kila jambo litaamuliwa kama Lowasa atakavyo.Hayo ndiyo aliyoyataka CCM akayakosa.
 
hahahaha, ndo maana lowassa alipoondoka ccm kuna waliomfuata, na wa;liomfuata ndo hao chadema lowassa ambao walikuwa ccm lowassa
 
CCM inakufa vibaya na haitarudi kwenye historia ya kutawala milele.mlikoswa koswa 2010.shukuruni wizi uliowarudisha madarakani.mwaka huu hakuna namna ,you must go.CCM out.
 
Nauona mwisho mbaya wa CHADEMA!Tamaa za muda mfupi na kupenda shortcut vitawacost sana!Bahati mbaya wabunge wengi vijana wa Chadema hatutowaona kwenye bunge lijalo!wamegaiana majimbo kwa kujuana
 
hahaaaa yaaani mnavyoongozana kuanzisha thread na kucoment hadi raha.
 
Back
Top Bottom