Yasome Maneno ya nguvu juu ya mapenzi na maisha (3)

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
1. Maneno ni mengi, kila mtu huwa na mazoea yake na namna anavyoishi na watu, siyo wote watakuona sawa unaposimama au kuzungumza na jinsia nyingine, mawazo ya mtu uweza kuwa tuhuma na shtaka kwa umpendaye.

Wanga wa mapenzi, ni fungu baya, yeye akifanya ni sawa ila wengine ni kosa, ni rahisi sana kuyaona ya wengine kuliko yao.

Unapojitenda na maisha ya kupokea kila usikialo ni kujitengea na majaribu ya imani ya mapenzi kwa uliyenaye.
Mtu mzima na mpenzi bora huwa achungwi.

2. Ukiwa siyo muoga wa maisha, usiogope kutoa ahadi kwa umpendae, ni rahisi kuogopa kushindwa kutimiza ila ni fedheha ukionyesha huna juhudi ya kuifikia ahadi na huna ahadi naye wala ndoto.

Maisha ya mahusiano ni ahadi, kufikia, kupoteza na kutimiza chache, ikiwa wewe ni binadamu, uwezi kufanya mia kwa mia, siyo maskini siyo tajiri kila mmoja ana uko wake. Mwenye kuzitambua juhudi zako atakutunza na kuibeba thamani yako.

Ni rahisi kutimiza ndoto za mtu umpendae, ila kama hajui nini maana ya kupendwa akakuumiza.
Jifunze kufanya kilicho kwenye uwezo wako kwani kila mtu anaye wake wa mapenzi asiyehitaji kingi wala kidogo zaidi ya uwepo wako katika dunia.

3. Maisha ya mapenzi ni uamuzi, hakuna kosa kumpenda mtu. Mbaya ni kumpata limbukeni wa mapenzi akauchokonoa ubongo wako, heshima yako na mwili wako.

Japo maana ya mapenzi siyo wote ni raha, lakini huwa ni kama riziki, ikiwa ni wakati wako na fungu lako, utaona kwanini ulichelewa kuwa naye uliyempata.

Maana furaha za mapenzi uzidi vyote vya dunia, upendo ni sehemu kubwa ya amani ya dunia, ukiishi kwa mitazamo ya watu juu ya mapenzi kwa uliyenaye utaishi kwa hofu, pesa ukupa maamuzi ila hainunui furaha, umaskini ukupa maamuzi ila haununui furaha.

Jifunze kupenda na jifunze kuwa na dharau ya nyege zako na kuwa na mipaka na mapungufu yako.
Ishi kama wewe na siyo kama wale wasemavyo na wanavyo, maana za mapenzi zipo kukufunza uwe bora na siyo kuwa muoga.

#imarika katika maisha na mahusiano
#mnogeshe umpendae
#kupenda ni utashi
#kutendwa na hulka za mtu ni fumbo, ndio maana binadamu hatufanani ila tunajengana kuelewana.
Na mmmuhumba.
textgram_1675399505.jpg
textgram_1675336056.jpg
textgram_1674631722.jpg
 

Attachments

  • textgram_1675336056.jpg
    textgram_1675336056.jpg
    140 KB · Views: 20
Back
Top Bottom