Danny greeny
JF-Expert Member
- Feb 6, 2014
- 3,856
- 1,647
Hatimaye timu ya Wananchi Dar es Salaam Young African ( Yanga ) imetwaa ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara huku ikiwa na Mechi 3 Mkononi Baada ya kufikisha point 68 katika Michezo 27. Point ambazo haziwezi kufikiwa na Timu yoyote.
Yanga sasa anakuwa bingwa kwa kuweka historia ya kuchukua Kombe la ligi kuu Mara 26.
=======
Timu ya Yanga inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania Bara leo imetwaa taji la ligi hio inadhaminiwa na kampuni ya mitandao ya simu ya Vodacom. Yanga imefanikiwa kutwaa kombe kabla ya mechi yake kutokana na timu ya Simba kukubali kipigo kutoka timu ya Mwadui hivyo haitaweza tena kufikisha alama ilizonazo Yanga.
Yanga inatwaa taji la ligi kuu kwa kufikisha alama 68 ambazo kutokana na kufungwa Simba hawatoweza kuzifikisha tena na ilikuwa ndio timu pekee ambayo ingeweza kufikisha alama hizo hivyo kuhitimisha mbio ubingwa na Yanga kufanikiwa kutwaa taji kwa mara ya pili mfululizo.