Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
Mpira umemalizika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Yanga wameifyatua klabu ya Cercle de Joachim ya Mauritius mabao 2-0, hivyo kusonga mbele kwenye raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-0.
Mrundi Amisi Tambwe ameiandikia Yanga bao la kwanza kwa kichwa katika dakika ya tatu ya mchezo akiunganisha krosi ya Simon Msuva.
Dakika ya 56 Thabani Kamusoko ameifungia Yanga bao la pili kwa mkwaju wa faulo baada ya Msuva kumuachia mpira Haji Mwinyi aliyempasia Kamusoko ambaye naye alifumua shuti kutoka umbali wa meta 21 na kujaa kimiani.
Yanga sasa inasubiri mshindi wa mechi ya Mbambane Swallows ya Swaziland na APR ya Rwanda ambayo inapigwa kwenye Uwanja wa Amahoro jijini Kigali. Katika mechi ya kwanza APR ilifungwa 1-0.
Kikosi cha Yanga kilikuwa na:
1. Ally Mustapha 'Barthez'
2. Juma Abdul
3. Haji Mwinyi
4. Kelvin Yondani
5. Vicent Bossou
6. Mbuyu Twite
7. Simon Msuva
8. Thabani Kamusoko
9. Amissi Tambwe
10. Malimi Busungu
11. Deus Kaseke
Sub:
12. Deo Munishi
13. Oscar Joshua
14. Pato Ngonyani
15. Matheo Simon
16. Paul Nonga