Yanga yamtupia virago Salumu Telela!!

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,347
5,984
DSC_9775.jpg
Taarifa nilizonazo ni kwamba kocha mkuu wa Yanga SC Hans amependekeza kuwa na kikosi kidogo lakini chenye ufanisi na amependekeza kumuacha kiraka wake mkongwe Salumu Telela ili akajaribu maisha kwingine.
Wakati huo huo club ya Yanga imewatoa kwa mkopo wachezaji wake wawili mshambuliaji Paul Nonga anayekwenda Mwadui fc na kipa wake aliyekosa namba klabuni hapo Benedict Tonocco ambaye anaweza enda Toto Africa ya Mwanza au Ndanda ya Mtwara.
 
Wa matopeni walikuwa wanamtaka. Sasa kazi kwao. Sijui tatizo ni nini maana ni mchezaji mzuri mzuri mwenye uwezo wa kucheza sehemu zaidi ya moja. All the best Telela.
 
TELELA ATEMWA RASMI YANGA, TINOCCO ATOLEWA KWA MKOPO

Posted by: BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE Posted date: Sunday, June 12, 2016 / comment : 0



Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
KIPA Benedictor Tinocco atatolewa kwa mkopo, wakati kiungo Salum Abdul Telela hataongezewa Mkataba Yanga.
Habari za ndani ambazo BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE imezipata kutoka Yanga zimesema kwamba maamuzi hayo yamepitishwa na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm.
“Tinocco atatolewa kwa mkopo sehemu ambayo anaweza kupata nafasi ya kucheza, ili kama atapandisha uwezo wake, anaweza kurudishwa, lakini Telela kocha (Pluijm)” kimesema chanzo kutoka Yanga.
Bado haijafahamika haswa sababu za Telela kutoongezewa Mkataba, licha ya umuhimu wake wa wazi unaoonekana katika timu kwa sababu ni kiraka anayeweza kucheza kama beki wa kulia, kati na nafasi zote za kiungo.

Fundi Salum Telela ameachwa Yanga SC licha ya kwamba bado ni mchezaji muhimu katika timu

Na kuhusu suala la nidhamu, Telela anaonekana ni mchezaji mwenye nidhamu, bidii ya mazoezi na kujituma, ambaye wakati wote anapoingizwa uwanjani licha ya muda mwingi kuwa mchezaji wa akiba hucheza vizuri.
Wakati huo huo, Yanga inaendelea kusubiri ofa ya kumuuza mshambuliaji Paul Nonga ambaye ameombwa mwenyewe kuuzwa, ili kwenda timu ambayo atakuwa anacheza.
Nonga aliyesajiliwa Desemba kwa dau la Sh. Milioni 20 kutoka Mwadui FC ya Shinyanga ameamua kuondoka baada ya kushindwa ushindani wa namba.
Washambuliaji chaguo la kwanza wa Yanga ni Mzimbabwe Donald Ngoma na Mrundi, Amissi Tambwe wakati Nonga alikuwa wa akiba pamoja na Malimi Busungu na Matheo Anthony.
Tayari Yanga SC imekwishamuacha kiungo kutoka Niger, Issoufou Boubacar ambaye pia alisajiliwa dirisha dogo Desemba.5
 
hatutaweza kujua ni sababu gani iliyosababisha aachwe labda mpaka uongozi wa yanga uamue kuweka wazi sababu za kumuacha na uongozi haubanwi kuweka wazi sababu za uamuzi huo. labda kama mchezaji mwenyewe anajua sababu na akaamua kufunguka. kwangu mimi naona anatakiwa asikate tamaa kwani maisha ndivyo yalivyo afanye mazoezi bado uwezo anao na hata umri unamruhusu ila timu zinazomhitaji zimfanyie vipimo labda ana majeraha ya muda mrefu ambayo yamewatisha viongozi wa yanga. ajifunze kwa wachezaji wengine waliopitia matatizo kama yake, kwa mfano mohamed banka aliachwa na yanga akasajiliwa na simba akaja akacheza zaidi ya misimu 4 ya ligi kwa mafanikio na hata Idd Athumani Chuji alisajiliwa na simba akitokea yanga wakamkomoa wakamwacha akarudishwa yanga na kocha aliyewahi kumfundisha hapo hapo yanga (nimemsahau jina) akacheza takribani msimu 3 kwa kiwango cha juu.
 
Back
Top Bottom