Yanga Yahaha Kusaka Kocha

[h=1]MZEE WA KUTIBUA: Tatizo la Yanga si kocha tu hata wachezaji[/h]
Michael+Mombuli.jpg

BADO msimu wa sikukuu unaendelea, hii ni Jumamosi ya mwisho ya mwaka 2013. Jumatano ijayo tutaukaribisha mwaka mpya wa 2014. Kuna mambo mengi yametokea mwaka 2013 mengine mazuri na mengine mabaya.

Kila moja lilikuja na changamoto zake lakini kama binadamu ni wakati wa kujipanga na kujitafakari upya kwa kupitia malengo na mambo uliyokuwa umejiwekea na kuangalia ni changamoto zipi za kukabiliana nazo ili kupiga hatua.

Kwenye michezo kulikuwa na mengi lakini hakukuwa na kitu kipya, timu zote kuanzia ya Taifa na klabu hazikuwa na jipya kimataifa. Hakuna hata moja iliyofanya cha ajabu kimataifa, maisha yalikuwa ni yaleyale. Yanga imempa notisi ya siku 30 Kocha Mkuu Ernest Brandts, hiyo inamaanisha kwamba si kocha tena na itamlipa mshahara wa mwezi mmoja kabla ya kuachana naye. Sababu ya msingi waliyoieleza ni kwamba ufanisi wake ni mdogo na ameshindwa kuimudu timu kwani inazidi kuporomoka kila kukicha.

Lakini ukitafakari kiumakini utaona tatizo linaloikuta Yanga sasa ndiyo tatizo lililokuwa likiisumbua Simba miaka minne iliyopita.

Uongozi unahusika moja kwa moja na kinachotokea. Brandts ameshindwa kuimudu timu kwa vile haina nidhamu ya kawaida wala nidhamu ya kazi.

Kocha ameshindwa kuwadhibiti baadhi ya wachezaji haswa wa kigeni ambao wamekuwa na jeuri na wanajifanyia mambo wanavyotaka, wanajibizana na kocha wanataka kocha afanye wanavyotaka wao. Kazi haiwezi kufanyika katika mazingira hayo lazima sehemu ijulikane kiongozi ni nani na mfanyakazi ni nani, hamuwezi kuwa mabosi wote.

Mchezaji haji mazoezini kwa wakati, anachelewa kuripoti kambini kwa sababu zisizo na msingi, anapandisha hasira na kutamka maneno yanayoashiria utovu wa nidhamu hadharani yote hayo uongozi umekaa kimya kabisa.

Kocha anashindwa kuchukua hatua kwa vile baadhi ya viongozi wamehusika moja kwa moja na usajili wa wachezaji hao na inafikia hatua wanawalinda bila kujua madhara yake. We fikiria mchezaji anaondoka kwenye chumba cha kubadilishia anamtamkia kocha "ama zangu ama zako, niondoke mimi au uondoke wewe" hiyo inaashiria dharau na kiburi kilichopitiliza. Anafanya hivyo akijua wazi kwamba mabosi wake watamlinda.

Hiyo hali ilikuwa ikiwaathiri Simba wakati fulani ambapo kulikuwa na migomo ya ajabu ajabu viongozi wanatumia wachezaji wao kuhujumiana jambo ambalo halikuwa zuri. Uongozi wa Yanga unapaswa kurejesha nidhamu kwenye timu na kuacha kulea baadhi ya wachezaji, hatua za nidhamu zichukue nafasi yake.

Haiwezekani mchezaji hahudhurii mazoezini halafu anampigia simu kiongozi badala ya kuongea na meneja au kocha, mchezaji anakwenda kwao anarudi anavyojisikia na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa.

Huko si kujenga ni kuweka makundi kwenye timu na hiyo inaathiri mpaka utendaji wa uwanjani kwa vile wengine wanajisikia vibaya kwa kuona wenzao wakipendelewa waziwazi.

Lakini Brandts naye alionyesha udhaifu. Kwa jinsi hali ilivyokuwa ikiendelea alipaswa kufanya uamuzi mgumu kudhibiti nidhamu ya ufanisi wa timu, angefukuza wachezaji waliokuwa na kiburi na ambao walikuwa wakiropoka hovyo au kushindwa kufuata taratibu za timu.
 
[h=1]KOCHA LOGARUSIC AINGIA KWENYE LADA ZA YANGA[/h]





Yanga imemjumuisha Kocha Zdravko Logarusic wa Simba katika idadi ya makocha inaowataka.

Habari za uhakika zimeeleza Yanga imemjadili kocha huyo na huenda ikafanya naye mazungumzo ili asitishe mkataba wake wa miezi sita Simba na kutua Jangwani.


Ingawa viongozi wa Yanga wamekuwa wagumu kulizungumzia suala la kocha mpya baada ya kumtema Ernie Brandts, lakini Logarusic ni kati yao.


"Kweli kabisa, Yanga wamevutiwa na kazi ya Logarusic na wanaamini ana uwezo wa kuwathibiti mastaa wa Yanga.


"Hivyo wamempa mtu kazi ya kuwasaidia kuzungumza naye na ikiwezekana mara moja ajiunge na timu hiyo.


"Unaweza ukasikia wakati wowote amechukuliwa na kuanza kuifundisha timu hiyo," kilieleza chanzo cha uhakika.
Juhudi za kumsaka Logarusic akiwa nchini kwao Croatia kwa ajili ya mazungumzo zilifanikiwa na alisema hivi:
"Naiheshimu Yanga, lakini naheshimu zaidi mkataba wangu wa miezi sita na Simba, sasa imebaki miezi mitano. Sipendi kuzungumzia timu nyingine kwa kuwa mimi ni mtu ninayefuata weledi," alisema Logarusic bila kukataa au kukubali kama amefanya mazungumzo na Yanga.
Imeelezwa viongozi wa Yanga wamefurahishwa na kazi yake siku Simba ilipoilamba Yanga kwa mabao 3-1 katika mechi ya Nani Mtani Jembe, huku akionyesha hajali nani ni staa kwenye timu na aliyeharibu, mara moja alisukumizwa kwenye benchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom