Yanga yachukua tahadhari Misri

Yanga yachukua tahadhari Misri

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,687
"Yanga wajiandaa kivita - Watarajia kufanyiwa hila"


Kocha Mkuu wa Yanga, Hans Van Der Pluijm amesema timu yake haitakwenda Misri ikiwa na dhana ya kwenda kujilinda ila itashambulia muda wote kwa lengo la kusaka mabao.
Yanga na Al Ahly zitashuka uwanjani kukabiliana katika pambano la marudiano litakalopigwa Jumapili hii jijini Cairo, Misri.
Katika pambano la kwanza lililopigwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Yanga ilichomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly.
Pluijm alisema staili ya kushambulia muda wote ambayo kikosi chake kiliitumia katika pambano la kwanza ndiyo atakayoitumia ugenini Misri.
¡°Jambo la kwanza tutamiliki mpira halafu tutashambulia muda wote kama tulivyofanya nyumbani, kama tukienda kucheza soka la kujilinda kwa sababu ya bao moja hapo tutakuwa tunajidanganya kwani katika soka njia sahihi ya kuzuia mashambulizi ni wewe kumshambulia adui,¡±alisema Pluijm.
Alisema,¡±Tumetengeneza nafasi nyingi katika mchezo wa kwanza, lakini tuimetumia moja tu, nafikiri tutaongeza umakini zaidi katika mchezo wa marudiano kwa kuhakikisha kila nafasi tutaitumia.¡±
¡°Nikiri kwamba mbinu tuliyoingia nayo katika mchezo wa kwanza ilifanikiwa, utaona Emmanuel Okwi alikuwa anacheza kama mshambuliaji pekee, Mrisho Ngassa nyuma yake huku tukiwa na mawinga Simon Msuva na Hamis Kiiza na ndio maana tulitengeneza nafasi nyingi,¡±alisema Pluijm.
Naye kocha msaidizi wa Yanga, Charles Mkwasa alisema watawaandaa wachezaji wao kisaikojia na kimwili kwa ajili ya kukabiliana na mizengwe ambayo inaitarajiwa itajitokeza katika pambano la marudiano dhidi ya Al Ahly.
Mkwasa alisema kuwa timu yake inafahamu itakutana na changamoto ya mizengwe katika pambano la marudiano, hivyo wamejiandaa kukabiliana nayo.
¡°Tunafahamu kwamba mechi ya marudiano itakuwa na mizengwe mingi, lakini benchi la ufundi litawaandaa wachezaji kisaikolojia na kimwili kwa ajili ya kukabiliana na hali hiyo,¡±alisema Mkwasa.
Wakati huo huo, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amewataka wachezaji wa Yanga kutobabaishwa na mizengwe katika pambano la marudiano na badala yake waelekeze akili zao kusaka ushindi.
¡°Hivi karibuni nilikuwa Misri na nilishuhudia mechi kati ya Al Ahly na Sfaxien ya Tunisia, wale jamaa wamezoea mambo ya ajabu ajabu kama kulipua baruti au kuwasha miale ya moto na kupuliza filimbi kama ya mwamuzi wakati unaenda kufunga.
¡°Lakini mimi nasema hayo mambo yasiwababaishe wachezaji wa Yanga kwa sababu uwanjani kuna mtu mmoja tu mwenye mamlaka naye ni mwamuzi atawalinda, wao waelekeze akili zao kusaka ushindi tu na wale wanafungika kabisa hata kwao,¡±alisema Malinzi.
Kwa upande wake nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ¡®Canavaro¡¯ aliwatahadharisha wachezaji wenzake kwa kuwataka wasibweteke na ushindi walioupata katika mechi ya kwanza baina yao na Al Ahly badala yake wajiandaae kikamilifu kwa ajili ya mechi ya marudiano.
Canavaro alifunga bao pekee lililoipa Yanga ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly katika pambano la kwanza la raundi ya kwanza la Ligi ya Mabingwa Afrika lililopigwa Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Canavaro alisema anaamini mchezo wa marudiano utakuwa mgumu zaidi kwa vile wapinzani wao watakuwa nyumbani, hivyo ni wajibu wa kila mchezaji wa timu hiyo kujituma.
¡°Wachezaji wa Yanga hatutakiwi kubweteka na matokeo tuliyopata katika mechi ya kwanza, Al Ahly ni timu kubwa na mechi ijayo itakuwa nyumbani, hivyo kila mmoja wetu anapaswa kujituma,¡±alisema Canavaro
Alisema,¡±Naamini tukijituma na kutumia nafasi tutakazozipata tutawafunga huko huko kwao na hakuna linaloshindikana.¡±


MCL
 
*Taarifa ya kuzuiliwa kwa mashabiki kwenye mchezo wa Yanga vs Al Ahly Cairo:


Mchezo wa marudiano wa michuano ya CAF Champions League baina ya klabu bingwa ya Tanzania bara Dar Young Africans dhidi ya mabingwa watetezi wa kombe hilo Al Ahly ya Misri utachezwa kwenye uwanja usiokuwa na mashabiki, imethibitishwa na mamlaka za usalama na chama cha soka cha nchi hiyo.
Yanga na Al Ahly ambao walichuana wikiendi iliyopita katika mchezo wa kwanza katika dimba la uwanja wa taifa Dar es Salaam, kwenye mchezo ambao uliisha kwa Yanga kushinda 1-0. Timu hizo zitarudiana jumapili wiki hii.
Hata hivyo habari nzuri kwa Yanga na mbaya kwa Al Ahly, ni kwamba mchezo huo hautokuwa na mashabiki kutoka na sababu za kiusalama.
Azmi Megahed, msemaji wa chama cha soka nchini Misri, amesema mashabiki hawatoruhusiwa kuhudhuria mechi hiyo kutoka sababu za kiusalama.
Jumamosi wiki iliyopita, polisi walipambana na mashabiki wa Zamalek White Knights ambao walijaribu kuingia katika uwanja wa Cairo kuangalia mchezo kati ya Zamalek dhidi ya mabingwa wa Angola Cabo Schrob. Fujo hizo zilipelekea kwa kukamatwa kwa mashabiki 33.
 
Wamisri wainyima ulaji Yanga:

Klabu ya Yanga imepoteza dola 70,000 za Kimarekani (Sh 111.2 milioni) baada ya kampuni ya MGB ya Misri kushindwa kurusha moja kwa moja ‘Live’ mechi kati ya timu hiyo na Al Ahly iliyochezwa Uwanja wa Taifa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Awali, Yanga iliingia mkataba wa Dola za Marekani 90,000 na kampuni hiyo kwa ajili ya kuonyesha mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kuwania kucheza raundi ya pili na ikapewa malipo ya awali dola 20,000.
Mwakilishi wa Kampuni ya MGB, Francis Gaitho aliuambia mtandao wa Al Ahly.com kuwa wanailaumu Yanga kwa kukwamisha zoezi la kurusha mechi hiyo, akidai waliwafukuza uwanjani wafanyakazi wa televisheni ya Star TV na kamera zao waliokwenda kurusha moja kwa moja pambano hilo.
Alisema baada ya kusaini mkataba na Yanga, waliwalipa fedha za awali kutoka kwenye akaunti yao nchini Misri kwenda kwenye akaunti ya klabu hiyo Tanzania.
Gaitho alisema timu ya watu wa utayarishaji waliotakiwa kuja Dar es Salaam kurekodi mchezo huo ilishindwa kufika kwa wakati kutoka Cairo, hivyo wakalazimika kutafuta kampuni ya Tanzania kufanya kazi hiyo na Star TV ya Tanzania ikabahatika kupata zabuni kutoka kwao.
Alisema kuwa licha wa ubalozi wa Misri nchini Tanzania kuiandikia barua klabu ya Yanga kwamba MGB italipa malipo yaliyobaki baada ya mechi na kudhaminiwa na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, uongozi wa Yanga iligoma kurekodiwa kwa mechi hiyo.
“Wakati tulipofikia mwafaka na kukubaliana mechi irekodiwe, kwa bahati mbaya Star TV walikuwa tayari wamekwishaondoka uwanjani na muda ulikuwa umeenda,” alisema Gaitho.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Mussa Katabaro akizungumzia madai hayo katika mahojiano na mtandao wa Bin Zubery alikiri klabu hiyo kupokea malipo ya Dola 20,000 na kudai kuwa klabu yake ilipaswa kulipwa kiasi kingine cha Dola 35,000 kabla ya mechi na Dola 35,000 nyingine baada ya mechi, lakini MGB ilishindwa kutekeleza kipengele hicho cha mkataba. “Mbaya zaidi, katika mkataba wetu na wao tulikubaliana hakuna kupelekana mahakamani, sasa tulipoona wameshindwa kulipa zile fedha.
Katabaro alisema wateja wao hawakuwa wa kweli katika maelezo yao baada ya kudai kwamba kuna mtu alikuwa anakuja na fedha kutoka Misri akakamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cairo wakati si kweli.
Alisema baadaye walidai ubalozi wa Misri hapa nchini utalipa hizo fedha, lakini ulipoulizwa ulikana na ndipo TFF ilipojitolea kuwaandikia Yanga SC hundi ya dola 35,000 na dola 10,000 kwa Stars TV ili mechi ionyeshwe.
“Sisi tulikubali kupokea hundi ya TFF mechi ionyeshwe, lakini Star TV wakagoma kupokea hundi ya TFF wakaondoka, sisi hatukuwafukuza kama wanavyodai hao jamaa, kimsingi hawa jamaa wametukosesha fedha dola 70,000.
“Kuna kampuni nyingine ya Misri ilijitokeza ikiwa tayari kutupatia dola 100,000 kununua haki za TV za hiyo mechi, lakini sisi tukaheshimu mkataba wetu na MGB, ila mwisho wa siku uungwana wetu umetuponza,”alisema Katabaro.
 
Back
Top Bottom