Dunia hii sikuwahi kusikia eti mkataba wa kazi unavunijika kisa kutopewa mshahara wa just miezi minne tu, watu wanakaa miezi 6 mpaka mwaka bila mshahara na bado ni watumishi watiiifu.
Wacha Yusuph Manji na Kleb awavuruge vuruge mpaka watakaposhtuka is too late.
Dunia hii sikuwahi kusikia eti mkataba wa kazi unavunijika kisa kutopewa mshahara wa just miezi minne tu, watu wanakaa miezi 6 mpaka mwaka bila mshahara na bado ni watumishi watiiifu.
Wacha Yusuph Manji na Kleb awavuruge vuruge mpaka watakaposhtuka is too late.
Ss tff amemzuia kwa rufaa ya magumashi ya Rage?. Muda wote walisubiri ni? Kwena fifa. Walisubiri asajiliwe yanga ndio wapate hasira za kudai?. Hiyo imeshakua siasa za chadema na ccm NITOKE VIPI.mwandishi ni kama wa blog ya simba. Swali lako ungewauliza FIFA na CAF walimruhusu vipi -vibali vipo vimetolewa tar 15/Dec/2013-acheze yanga kama kuna hayo usemayo?
Nikumbushe ni lini FIFA walitoa hukumu na kumuidhinisha Okwi kuichezea Yanga kutokana na kutolipwa mishahara yake Tunisia.inawezekana hujasikia, lakini ndivyo ilovyofanyika kwa Anelka na Drogba hadi wakahama kwa hukumu ya FIFA kutoka timu za China na kurejea tena Ulaya wanakocheza hadi sasa.
Vibali Kutolewa na FIFA au CAF sio hoja, mbona hata leo ukitaka nyaraka halali za Passport, TRA, Tanesco, Dawasco, Driving License nk wakati hata sifa huna unapata kama kawaida??? Au wew unakaa Dunia gani?mwandishi ni kama wa blog ya simba. Swali lako ungewauliza FIFA na CAF walimruhusu vipi -vibali vipo vimetolewa tar 15/Dec/2013-acheze yanga kama kuna hayo usemayo?
Inaonekana wewe hata hufuatilii mambo yanavyokwenda, Hans Pope kwa hekima sana aliwaambia Yanga wameingia mkenge kwa kumsajili Okwi au hukusikia hilo au kila kitu Rage tu, mnaogopa hata kivuli chake nini??Ss tff amemzuia kwa rufaa ya magumashi ya Rage?. Muda wote walisubiri ni? Kwena fifa. Walisubiri asajiliwe yanga ndio wapate hasira za kudai?. Hiyo imeshakua siasa za chadema na ccm NITOKE VIPI.
Anayepaswa kujitambua nadhani ni wewe, maana ungekuwa sahihi leo hii ungemuona Okwi anaingiza makongoro yake kuichezea Yanga Michuano ya Afrika.FIFA inaongozwa na kanuni na sio njaa kama zenu wabongo zinazowafanya mgeuke watumwa. JITAMBUE!!
Monday, January 27, 2014
YANGA WAMEMNUNUA WAPI EMMANUEL OKWI?
Na BARAKA MBOLEMBOLE
Wakati ligi kuu ikianza, mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi, Mganda, Emmanuel Okwi amekuwa mmoja wa watazamaji mwenye thamani kubwa. Je, Yanga wameingia ' mkenge' katika usajili wake?. Hili linaweza kuwa swali ambalo majibu yake yapo wazi. Kwanza, Okwi ni mchezaji wa Etoile du Salehe ya Tunisia ambao walimnunua kutoka timu ya Simba.
Kwa nini yupo Yanga?. Alikuwa akiichezea timu ya SC Villa ya kwao Uganda kwa mkataba wa mkopo wa miezi sita akitokea Etoile. Narudia tena, alikuwa akiichezea Villa kwa mkopo. Fifa ilimruhusu Okwi kucheza Villa kwa muda wakati kesi tatu zinazomuhusu Mganda huyo zikitafutiwa mhuafaka. Okwi kwa upande wake anadai kuwa Watunisia hao walivunja mkataba kwa kushindwa kumlipa pesa zake kama ilivyotakiwa. Simba nao wanadai malipo yao kutoka kwa Etoile.
Okwi aliruhusiwa kuichezea Villa ili kulinda kiwango chake, na wala hakuwa mchezaji anayemilikiwa na timu hiyo. Alizuiwa kuichezea timu ya Taifa ya Uganda katika michuano inayoendelea ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani, CHAN, kwa kuwa alikuwa Villa kwa mkopo kutoka timu ya ng'ambo. Ila, ni Villa ndiyo wanaosemekana kumuuza Okwi kwa timu ya Yanga. Kwa mamlaka gani?. Hadi hapa Yanga watakuwa wameliwa. Kwa kuwa Okwi ni mchezaji wa Etoile si Villa.
Yanga wamemsaini Okwi huku wakijiaminisha kuwa wapo sahihi. Wanaamini Okwi ni mchezaji huru au wa Villa. Ila, alitakiwa kucheza Villa kwa miezi sita, lakini akaitumikia miezi isiyozidi miwili tu na kununuliwa. Caf, Shirikisho la soka Afrika wamemuhidhinisha Okwi kuichezea Yanga. Kamati ya sheria na hadhi ya wachezaji imemzuia matumizi yake hadi watakapopata ufafanuzi kutoka FIFA, Shirikisho la soka ulimwenguni.
Ndiyo, wapo sahihi kwa kuwa FIFA, ndiyo waliosema mchezaji huyo acheze Villa kwa miezi sita wakati kesi zake zikishughulikiwa.
FIFA, wanaweza kumruhusu Okwi kuchezea Yanga kwa maslai ya kipaji chake. Ila, wanaweza pia kumzuia endapo watajua kuwa mchezaji huyu amekiuka maagizo yao ya awali ambayo walimwambia acheze Villa. Inawezekana mchezaji huyo akaonekana tapeli, kwa kuwaadaa Yanga wakati akijua fika mkataba wake upo Etoile. Wapo wachezaji walioshinda vita kama hii ya Okwi, ila wapo pia walioingia katika vifungo vya FIFA.
Huenda Yanga wakamtumia Okwi siku za mbele, ila kwa sasa ni uhalali wa mchezaji huyo. Kama, Etoile wataendelea kushikilia msimamo wao kuwa hawajui mchezaji wao mahali alipo, Okwi ataoneka ni mtoro. Endapo, Okwi ataonekana ni halali madai yake anaweza kulipwa fidia na Etoile, ila kasheshe ni wapi ambapo Villa walipata kibali cha kumuuza Okwi kwa timu ya Yanga?
Kila upande udai una wanasheria wake. Duh!. Lakini mwanasheria wa Okwi anaweza kuwa mjanja zaidi, mwenye akili zaidi, kwa kuweza kupata saini na mamillioni ya Yanga kwa ufafanuzi wake wakati akimpigia debe mteja wake kuwa hana tatizo. Kama sheria iliwekwa ili ivunjwe, na kama mikataba siku zote inaweza kutenguliwa, Yanga watamtumia Okwi, ila tusije kushangaa FIFA, wakisema mchezaji huyo mali ya Etoile. Yanga walimnunua wapi Emmanuel Okwi? Labda hapa ndipo kuna hoja ya msingi
Imekuchukua muda mrefu kufikiria jawabu, kiasi kwamba umesahau hata hoja yako mama. Ni vyema nikukumbushe kwamba ulikuwa na mawazo kwamba mchezaji akishanunuliwa anachotakiwa ni kufanya kazi, mshahara baadaye. Nilichokifanya ni kukumbusha kwamba hali haiko hivyo. Nadhani nimefanikiwa. Sikukusudia kuanzisha malumbano ya uke wenza.Nikumbushe ni lini FIFA walitoa hukumu na kumuidhinisha Okwi kuichezea Yanga kutokana na kutolipwa mishahara yake Tunisia.
Inaonekana wewe hata hufuatilii mambo yanavyokwenda, Hans Pope kwa hekima sana aliwaambia Yanga wameingia mkenge kwa kumsajili Okwi au hukusikia hilo au kila kitu Rage tu, mnaogopa hata kivuli chake nini??
Kwa uelewa wako umeona kwa kutukana hayo matusi ndiyo umejibu hoja yangu?? Sikulaumu wewe bali ni malezi mabovu uliyopewa na mzazi/wazazi wako.Imekuchukua muda mrefu kufikiria jawabu, kiasi kwamba umesahau hata hoja yako mama. Ni vyema nikukumbushe kwamba ulikuwa na mawazo kwamba mchezaji akishanunuliwa anachotakiwa ni kufanya kazi, mshahara baadaye. Nilichokifanya ni kukumbusha kwamba hali haiko hivyo. Nadhani nimefanikiwa. Sikukusudia kuanzisha malumbano ya uke wenza.
FIFA inaongozwa na kanuni na sio njaa kama zenu wabongo zinazowafanya mgeuke watumwa. JITAMBUE!!
Hoja yako mama = Hoja yako ya msingi (the mother/basic/principal/ main argument)Kwa uelewa wako umeona kwa kutukana hayo matusi ndiyo umejibu hoja yangu?? Sikulaumu wewe bali ni malezi mabovu uliyopewa na mzazi/wazazi wako.
Anayepaswa kujitambua nadhani ni wewe, maana ungekuwa sahihi leo hii ungemuona Okwi anaingiza makongoro yake kuichezea Yanga Michuano ya Afrika.
Na kwa sababu mmekataa kujitambua na kuukataa utumwa dhalimu wa Yusuph Manji, ngoja aendelee kusajili kwa matakwa yake hata kama usajili wake ni mbovu ili tu kuikomoa Simba au angalau katika utawala wake arudishe Bao 5 lakini mtaendelea kufungwa na Simba SC mpaka atakapoondoka huyo Manji wenu. Na sasa hivi deni la magoli limefikia 8 kwa 1