Yanga waliweza,kwanini simba tunashindwa?

Nakapanya

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2012
Posts
2,096
Reaction score
709
Klabu ya simba imekuwa katika mwenendo mbovu katika msimu uliopita na mpaka sasa,tatizo kubwa ni uongozi uliopo madarakani ukiongozwa na mwenyekiti Rage.Amekuwa mtu maneno mengi pasipo tendaji,mapato na matumizi hayaeleweki,usajili na uuzaji wa wachezaji hauko strategically,Rage ametoa ahadi nyingi ambazo hazitekelezi.

Sasa nafikiri ni wakati wa bwana Rage kuondoka(niliisha wahi kuandika hili huko nyuma).

Nashangaa kwanini wanasimba tunashindwa kumuondoa huyu bwana kama ambavyo wenzetu wa YANGA WALIVYOWEZA KUMUONDOA ALIYEKUWA MWENYEKITI WAO BWANA LOYD NCHUNGA.Nafikiri hatua zile zilizochukuliwa na Yanga zitumiwe na Simba kumuondoa huyu bwana Rage.
 

Hoja yako ni nzuri lakini kuna sehemu hujasema ukweli, Yanga hawakumwondoa Madega, aliyeondolewa ni Nchunga; kaangalie rekodi zako vizuri.

Harakati za kumwondoa Nchunga sababu haikuwa kwamba timu ilifanya vibaya bali kulikuwa na back up ya watu wenye hela ambao nafasi yake walikuwa wanaitaka, timu kufanya vibaya ilikuwa ni chachandu tu lakini mboga ilikiwepo tayari. Ukweli wa hili fuatilia matamko ya mzee Akilimali na yule kiongozi wao wa vijana.

Kuhusu kumwondoa Rage ni kweli inafaa aondoke lakini sasa kuna waliojipanga kuchukua timu, nakumbuka kipindi wanachama wamefanya mapinduzi matokeo yake wakaishia kuikabidhi timu kwa watu ambao hata hawakushirikishwa kwenye huo mpango. Kumwondoa sawa, tukishamwondoa tunamuweka nani? Kwa sababu mara nyingi unapotaka kufanya mapinduzi lazima ujue kabla kwamba mapinduzi yakishafanikiwa nani atashika madaraka sio mapinduzi yamefanikiwa halafu ndo mnaanza kuulizana nani sasa awe mwenyekiti.
 

Masuke kwanza nashukuru kwa kunisahihisha,ni kweli alikuwa ni Nchunga,kuhusu suala la simba kuhofia tutamuweka nani baada ya mapinduzi ni suala la kujipanga tukiishakuwa na dhamira ya kufanya hivyo.Pia mapinduzi yanaweza kufanyika then wakawekwa viongozi wa mpito kwa muda mfupi kabla ya kuitishwa kwa uchaguzi mkuu.Tukiendelea kuwa na Rage simba hatutafanya lolote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…