Yanga waendelea kula viporo taifa

Benjamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
92,346
111,899


MASHABIKI wa Yanga jana waliendeleza vituko na mbwembwe za kuutafuta ubingwa, baada ya kwenda Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, wakati Yanga wakicheza dhidi ya Mbeya City, wakiwa na bakuli la pilau huku wakila, wakimaanisha ni ishara ya ushindi wa mechi zilizokuwa zimebakia (viporo).

Huu unaweza kuwa ni mtindo mpya wa ushangiliaji, kwani kumbukumbu na rekodi mbalimbali zinaonyesha kwamba, haukuwapo na haupo kwenye utamaduni wa soka la Tanzania, hivyo mashabiki wa Yanga wanakuwa wa kwanza kuutambulisha.

Mashabiki waliozungunza na DIMBA kwa nyakati tofauti wamesema kwamba, hiyo inatokana na furaha waliyonayo na kwamba wataendelea na ushangiliaji wa aina hiyo hadi ligi itakapokwisha, ingawa wanaweza kuuendeleza kwenye mechi nyingine nje ya ligi kama wataona unafaa.

Ushindi wa jana Yanga umeifanya kuhitaji pointi tatu pekee ili kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo.

Mashabiki walikuwa wakiwatania watani wao ya jadi, Simba, kuwa pilau la ubingwa linanukia Jangwani, huku wengine wakisema ni mazoezi ya kula pilau la ubingwa.

Yanga ina pointi 65, sawa na Simba, lakini ina mchezo mmoja mkononi, huku Yanga ikiwa na miwili. Kwa msimamo huo, vijana wa George Lwandamina wanahitaji pointi tatu tu ili kufikisha pointi 68 ambazo zinaweza kufikiwa na Simba, lakini uwiano mzuri wa mabao ya kufunga unaifanya kuupata ubingwa kwa mara ya 27.


Chanzo: Dimba
 
Yanga ni timu inayojua vyema kucheza mpira na kusaka points tatu muhimu ndani ya dakika 90 tena uwanjani.

Lkn simba wanauwezo mzuri wa kucheza mpira wa mdomo na makelele zaid pia ni mabingwa wa kutafuta points za mezani na za kubebwa
Simba in shiida sana midomoni
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom