Ktk masiku ya hivi karibuni wananchi ni kama tunaburuzwa hapa jukwaani, yaani hakuna amsha amsha kabisa kiasi cha kuwa wanyonge sana. Hakuna kitu tunajivunia na kutamba nacho mbele ya Makolo japo tunaongoza Ligi. Makolo wanatuburuza utafikiri wana kitu spesho ambacho wananchi hatuna. Makolo Kufika fainali ya kombe la Luza ni kitu cha kututambia kweli? Suala la CAS nalo limetuongezea unyonge na linatuumiza roho kweli kweli. Japo naamini suala hili limekosa watu makini wa kulisemea. Tarehe 8, Makolo wao ndio walikimbia mechi, lakini sasa aibu tunabebeshwa sisi. Yaani kweli tumekubali kunyongeshwa na makolo ambao kila tukisimama nao tunawachapa? Kombe la Muungano nalo aakh.. Basi bana!!