Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 17,427
- 21,118
Kiukweli timu ya dar es salaam Young Africans(Yanga) tangu wamnyang'anye mikoba Hans Van Pluijm na kumkabidhi George Lwandamina mambo yamekuwa hovyo kila kukicha.
Mpaka sasa viwango vya wachezaji kama Juma Abdul,Donald Ngoma,Kelvin Yondan na Juma Mahadhi havionekani kabisa yote haya kwa sababu ya ubovu wa huyu kocha.
Sana sana ngoma ndo kaisha kabisa hana makali kabisa kama yale ya kipindi kile cha Hans Pluijm.
Yanga kila kukicha inazidi kuwa timu mbovu,hata aina ya ushindi wanaopata ni kiduchu sana ,mpira wanaocheza hauvutii kabisa na wanacheza kana kwamba timu bado ni ngeni kwenye ligi kuu.
Kikubwa cha kushukuru ni ubora wa kipa tuliyempata bila hivyo tungekuwa tunaoga mvua ya magoli kila kukicha.
Natamani leo kesho huyu bundi(lwandamina) anayetujaribia timu yetu aondoke.
Yanga tumekuwa wakiwa sana tangu Hans aondoke Yanga na Lwandamina kukabidhiwa mikoba.