Yanga SC msirudie dharau mlizozionyesha kwenye michuano ya Sportpesa Super Cup.

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
5,647
2,000
SPORTPESA SUPER CUP: Yanga SC acheni dharau.!

Sijui niseme nini. Ila iko namna hii. Kwanini mmeshindwa kuyapa heshima mashindano ya SportPesa super cup?

Mmeona wenzenu walivyokuwa wanajua kutumia fursa? Au ndio tuseme kuwa mil 60 kwenu nyinyi ni ndogo sana...?

Ngoja nianze na "Dar es salaam Young Africans SC''. Hivi nyinyi, tena hasa nyinyi ndio mmetia fora sana kwenye hii michuano.

Kwanini hamkuipa uzito sana hii michuano? Msinipe sababu kuwa wachezaji 8 ambao ni First Choice wote hawapo!

1. Tambwe
2. Hajji
3. Bossou
4. Kamusoko
5. Niyonzima
6. Msuva
7. Kessy
8. Beno

Mkinipa hiyo sababu, nitawauliza kwanini mmewapa mapumziko wachezaji hawa ambao kwa namna moja au nyingine wangeweza kushindana (ambao wengi wao ni Second Choice (SC)).

1. Mwashiuya (Rested)
2. Yondani (Rested)
3. Barthez (Rested)
4. Busungu (Rested)
5. Osca Joshua (Rested)
6. Zullu (Rested)
7. Matheo Anthony (Rested)

8. Ngoma (Huyu tunajua ni Majeruhi)

Hivi nini lengo lenu la kutumia wachezaji wengi wa Under 20? Kwani mmeambiwa kuwa hii ni michuano ya pre season? Acheni dharau. Mwambusi alipoulizwa kwanini wanatumia kikosi hiki ambacho ni dhaifu kwenye michuano hii, alijibu kuwa Anatafuta wachezaji wa kuwapandisha 11 eleven ya Kikosi kikuu pamoja na kuwafanyia majaribio wachezaji 2 waliosajiliwa

Kikosi cha Dar Young Africans SC kwenye michuano ya SportPesa Super Cup.

FC - First Choice Player
SC - Second Choice Player
NP - New Player
U20 - Under 20 Player

1. Munishi (FC)
2. Abdul (SC)
3. M Ally (U20)
4. Nadir (SC)
5. Andrew (SC)
6. Pato (SC)
7. Mhilu (U20)
8. Makka (U20)
9. Obrey (FC)
10. Martin (SC)
11.Mahadhi (SC)
12. Samwel Greyson (U20)
13. Babu Seif (NP)
14. Mbaraka Jumanne (U20)
15. Bakari Othman (U20)
16. Said Mussa (U20)
17. Ema Kichiba (NP)

Siku nyingine kama mnadhani hii michuano ni ya majaribio ni kheri mkaomba nafasi yenu ichukuliwe na wengine wenye nia ya kushindana.

USHAURI; kwa waandaaji wa michuano ya SportPesa Super Cup. waandaaji wanapaswa kuangalia hili suala la kuandaa michuano kipindi ambacho kila klabu inawacgezaji wake muhimu ili kuondoa visingizio vya wachezaji muhimu kukosekana.
FB_IMG_1496987061591.jpg
 

Mbojo

JF-Expert Member
May 31, 2011
1,408
2,000
Isee aibu hii sijui tujifichie wapi maana nyang'au zinabweka sana mitandaoni.
 

PROSPER 05

JF-Expert Member
Oct 14, 2013
230
250
Tehe teheteheeee, Eti Dharau..... Mmepigwa. Isipokuwa Nawapongeza Yanga Simba Kwa kulinda Heshima Ya TZ na Samatha Maana Mngekutana na Everton!!!!
 

Konaball

JF-Expert Member
Mar 11, 2009
2,951
2,000
Jun 9, 2017 15:44:34

Juma Mwambusi amesema pamoja na timu yake kutokuwa na bahati, mfungo wa mwezi wa Ramadhani umechangia timu yake kufungwa kwani wachezaji wamefunga


Kocha msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema timu yake haikuwa na bahati kwenye michuano ya SportPesa Super Cup baada ya jana kutolewa kwa mikwaju na penalti na timu ya AFC Leopards Kenya.

Mwambusi ameiambia Goal, timu yake ilicheza vizuri kwenye mechi zote mbili lakini tatizo lililowasumbua ni kumkosa Bahati ya kufunga mabao.

"Tumekosa Bahati kusema kweli tulicheza vizuri mechi zote mbili hata huu mchezo wa nusu fainali lakini tulikosa Bahati na hiyo hi kutokana na kutakuwa na wachezaji wenye uwezo pale mbele," amesema.

Kocha huyo amesema hana wa kumlaumu kwa sababu michuano hiyo ilikuwa ya kustukiza mno na baadhi ya wachezaji wao nyota walishaondoka nchini kwenda mapumzikoni baada ya Ligi kumalizika.

Amesema kwa kuitambua michuano hiyo msimu ujao watajipanga na kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi ikiwemo kucheza fainali na timu za Kenya ambayo ndizo zilitamba zaidi kwenye michuano hiyo.

Amesema nao mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan umechangia kwa timu yao kutolewa mapema kwani asilimia kubwa ya wachezaji wake ni waislamu na wamecheza wakiwa wamefunga.

Yanga imeondoshwa kwenye michuano hiyo wakivishwa medali kama washindi wa nne na kujinyakulia kitita cha Sh. Mililani 17 sawa na Nakuru All Stars ya Kenya iliyomaliza nafasi ya tatu.
 

nkese

JF-Expert Member
Mar 8, 2017
2,913
2,000
Kwani walipo banjuliwa mashindano ya Caf waliyadharau? Uwezo wao ni huo,labda timu malinzi iingilie kati
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions
Thread starter Title Forum Replies Date
brave_3 Viongozi wa Yanga Jitokezeni Museme na Mashabiki Wenu Sports 0
A NINA HOJA ZANGU YANGA AFRIKA. Sports 1
Abby Newton Karibu tujadili Ubovu wa Yanga kitaalamu. Sports 53
A Yanga ni ile ile haijabadilika jambo Sports 9
Smt016 Yanga imerudi nyuma hatua kumi Sports 16

Similar Discussions

Top Bottom