Yanga ni kama Imerusha upupu au bomu ndani ya Simba.

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Yes pale Simba wamevurugana haswa wamevurugwa na kichapo kizito cha magoli matano kutoka kwa Yanga. Wamekua kama wajenzi wa mnara wa Babeli hawaelewana kabisa huyu akiambiwa lete ndoo yeye analeta viti vya kukalia, huyu akiimbiwa lete filimbi anapeleka mpira ili mradi vitimbi tu.

Yanga ni kama imetupa upupu chumba walicholala watu, watu wanaanza kutoka nje kwa spidi wakipiga kelele wanawashwa na upupu mkali, wakati Yanga wametupa upupu wao wamekaa mbali wanawatizama tu Simba wakijikuna.

Kichapo cha goli 5 kimekuja muda muafaka Simba walizidi kelele sana mtaani, kila aina ya tambo kutoka kwa viongozi wao sio ajabu walimtaka Gamondi akwende pale Bunju kuwatizama kumbe Gamondi anawaandalia upupu wao tu limewafika kwa sasa.

Upupu umeanza kwa kocha mkuu na kocha wa viungo hawa wamekua kama mbuzi wa kafara kwa upupu huu waliomwaga tutegemee makubwa zaidi hakika tutajionea mengi ila yote hayatakua na tija kama timu bado itaendelea na mambo yao ya kiswahili na kutegemea mvua kushinda.

Mara papu Namungo naye akamwaga upupu zaidi.


Roma ikisema imesema
 
Kilichomponza fala ni kujiona Simba kumbe swala kwenye mpira uchwara badala ya kusaka wachezaji imara
 
Back
Top Bottom