Yanga na utawala wa miaka 5 watala tofauti

moodykabwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
625
602
YANGA NA UTAWALA WA MIAKA 5 WATALA TOFAUTI
__________Na moody kabwe
Moodykabwe@gmail.com
---0715268499
---0683201492

18/6/2010 Club ya Yanga ilifanya Uchaguzi wake wa kikatiba Baada ya aliekuwa mwenyekiti wa Club hiyo Madega kumaliza mda wake kikatiba.

Uchaguzi huo uliosimamiwa na makamu mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi Ridhiwani Kikwete uliwaingiza madarakani viongozi wafwatao.
naweka na idadi ya kura zao.

1) MwenyekitiLOYD Nchunga.kura 1437
2) M/mwenyekiti
Davis Mosha.kura 2142

Viongozi hawa walichaguliwa na wa jumbe wao (nane 8) ambao ni

1)Ally mayai Tembele kura 1734
2) Mzee yufu kura 1517
3) Sara Ramadhani kura 1500
4) Tito Osoro kura 1460
5) Mohamedy Bhinda kura 1458
6) Charles Mgondo kura 1300
7) Salumu Rupia kura 1231
8) Rutashoborwa kura 1225

--------Uongozi huu ilipofika
10/3/2011 Makamu Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Yanga, Davies Mosha, alijiuzulu wadhifa wake, kutokana na kile alichokiita kuchoshwa na masimango kutoka kwa wanachama na mashabiki wa klabu anayoyasikia kupitia vituo mbalimbali vya redio, vipeperushi nk., kiasi cha kuhatarisha maisha yake,

Nanukuu

“Wananishutumu mimi ni Simba na nachukua fedha kwa Makamu Mwenyekiti wa Simba Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ kuimaliza Yanga, sasa nawaacha na Yanga yao ili nitafute ustaarabu mwingine wa kufanya,” alisema Mosha.“Hebu fikiria sasa hivi wananituhumu kuwa nimehujumu mechi yetu na Simba, nihujumu kwa sababu gani, nimechoka bwana kutukanwa ovyo kama mtoto, nimewaachia klabu majungu yanatawala hapo kuna watu wapo pale hawataki kufuata katiba, ukiwaambia fuateni na kuiheshimu katiba ndiyo iliyotuingiza madarakani unaundiwa zengwe sasa hayo maisha gani, nimechoka mimi,”alisisitiza.

“Najiweka pembeni kwa manufaa yangu na klabu pia, kumbuka nimeshawahi kuvunjiwa kioo changu cha gari kwa madai eti naihujumu timu, hivyo nadhani hii ni nafasi kwao walioniombea mabaya Yanga,” alimaliza Mosha.

Mwishwo wa kunukuu

Hapo ndipo wana yanga walipo gawanyika timu mbili na kuisahau kilabu

Kuna timu mosha
Kukawa na timu Nchunga


Haikuchukua muda mrefu Nchunga nae akaundiwa Zengwe atoke madarakani kuwa Timu imemshinda

Tarehe 24/5/2012 saa 16:23 jioni

Nae Mwenyekiti wa Yanga, Wakili Lloyd Baharagu Nchunga alitangaza kujiuzulu wadhifa wake ofisini kwake, jengo la NSSF, barabara ya Bibi Biti, Dar es Salaam, siku moja baada ya kuvamiwa na kundi la watu nyumbani kwake, Mbezi, Jijini mida ya usiku wa wa manane. Hata hivyo, Nchunga alikataa kulihusisha tukio la kuvamiwa kwake usiku wa na kujiuzulu kwake, akisema kwamba amefikia uamuzi huo kuinusuru Yanga, kwa sababu wapo watu wako tayari Yanga ife, lakini wamng'oe yeye madarakani, kitu ambacho yeye hapendi kitokee.Nchunga alisema kwamba majira ya saa nane usiku alivamiwa na kundi la watu takribani 15, lakini hawakufanikiwa kufanya chochote kutokana na ulinzi mkali uliopo katika nnyumba hiyo."Kwanza mbwa walianza kubweka, walinzi wakashituka wakaomba msaada kwa walinzi wenzao, nasi tukapiga simu polisi, wakaja haraka sana na kukuta watu hao wamekwishakimbia,"alisema"



Baada ya heka heka kubwa ya kumtoa madarakani Loyd Nchunga na kufanikiwa mipango hiyo Ndipo Tarehe

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Jaji mkwawa akaitisha uchaguzi

Tarehe 15/6/2012
Uchaguzi huo ndiyo uliompa madaraka Yusufu manji wa kuwa mwenyekiti wa YANGA YEYE na Clemant Sanga na wajumbe wanne ambao ilkuwa ni uchaguzi wa kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wajumbe wanne waliojiuzulu na mwenyekiti na makamu wake
Mchakato ulianza na washindi walipatikana
Ambao walikuwa kama ifwatavyo

1) mwenyekiti Yusuphu Manji kura 1876) 97.0%
2) M/mwenyekiti
Clement Sanga kura 1948) 62.6%

Nafasi ya wajumbe ilikuwa hivi walioshinda

1) Abdallah Bin Kleb kura 1942
2) Moses katabaro kura 1068
3) Aaron Nyanda kura 922
4) Geroge Manyama kura 682

Kikatiba uongozi huu kwa ujumla ulimaliza mda wake mwaka ajana ila wanachama wa yanga kwenye .

Mkutano Mkuu wa marekebisho ya baadhi ya vipengele kwenye Katiba ya Yanga uliofanyika Ukumbi wa Bwalo la Polisi -Oysterbay huku wanachama wakipitisha kipengele cha kuundwa kwa kamati ya maadili.

wanachama wapatao 1560 siku hiyo waliamua kuazimia kuwaongezea muda wa mwaka mmoja Mwenyekiti Yusuf Manji pamoja na Makamu wake Clement Sanga ili waweze kukamilisha masuala ya katiba na kuweza kuandaa mkutano wa uchaguzi baada ya katiba kupitishwa na TFF

Hivyo basi Ndugu zangu wana Yanga Tukubali tukatae Kilabu yetu imepitia misuko suko mingi sana
[00:33, 03/05/2016] Moody Kabwe Comredy: Tunahitaji uchaguzi sasa Demokrasia ifwate mkondo wake tusirudi huko tunako toka lamda niwasaidie kiufupi wale wasiojua maana ya uchaguzi

UCHAGUZI MAANA YAKE NI

Uchaguzi ni nguvu ambayo Mwenyezi Mungu ameiweka na kuiachilia ndani ya kila mwanadamu. Nguvu hii ya uchaguzi ndiyo inayoachilia mafanikio au matatizo katika maisha ya watu, taifa na dunia nzima. Kwa wale ambao tunaamini tuliumbwa na Mwenyezi Mungu tunajua ametupa kuchagua tumtumikie yeye au shetani. Hii inadhihirisha ni kwa kiasi gani uchaguzi ulivyo na maana kubwa katika Club yetu ya sasa na ya baadaye. Lakini alituonya kuwa hatuwezi kutumikia mabwana wawili kwa hiyo ni lazima kumchagua mmoja. Uchaguzi ndio unaompa mwanadamu fursa ya kutawala vile vilivyowekwa chini yake na Mwenyezi Mungu. Changuzi mbalimbali unazofanya ndizo zinazoamua mustakabali au hatima ya Club Yetu Ili Tufanye kitu cho chote ni lazima kwanza Tufanye uchaguzi. Kwa hiyo unaweza kuona ni kiasi gani uchaguzi ulivyo kitu cha muhimu katika maisha ya Club Yetu

Tunafanya uchaguzi pale Tunapokuwa na vitu viwili au zaidi ambavyo haviko sawa na kila kimoja kina faida au hasara zilizo tofauti na Tunatakiwa Tuchague kimojawapo kati ya hivyo vitu na mara Tunapokuwa Tumekwisha kufanya uchaguzi Tunalazimika kuwajibika kwa zile hasara ambazo kile Tulichokichagua kitatupatia au tuna haki ya kufaidi zile faida ambazo zinatokana na kile tulichokichagua. Kwa hiyo maana yake ni kwamba ni lazima tujue kuwa baada ya wewe kufanya uchaguzi tunawajibika kutokana na matokeo mabaya ya kile tulichokichagua au tujue kuwa tunakuwa na haki ya kufaidi mafanikio au matunda ya kile Tulichokichagua.

Maisha ya mwanadamu siku zote yanaongozwa na chaguzi mbalimbali anazofanya kila siku. Chaguzi unazofanya ndizo zinazobeba, zinazoonyesha na kutafsiri maisha yako ulioishi, unayoishi leo, utakayoishi kesho na yale ambayo vizazi vyako vinavyofuata vitaishi.

Hivyo tunapaswa kujiuliza inakuaje wazee wa zamani wametuachia jengo safi tena sio moja mawili jangwani na mafia sisi tulioko wengi tumefanya nn
.
Namalizia kwa kusema tumeitendea zambi sana yanga ni zamu ya kuitendea mema sasa

Ni mimi mtoto wenu
MOODY KABWE COMREDY
______________________________
Telly 0683201492
Au 0715268499
____________________________
Moodykabwe@gmail.com

Nawatakia mitazamo mema
ecd34bce5b91fd0c000d88381070b864.jpg
17a9f963a18ad8ab78a6d265eca4832c.jpg
 
Wamatopeni tuachieni timu yetu mbona kwenu kuna migogoro hamuimalizi?
 
wanaotaka uchaguzi yanga ni wale wenye njaa majumbani mwao wanayanga komeni kabisa wanao jipigia kampeni kwenye kura muwapige chini ni bora mpitishe sheria ya kuingia ubia mwenye hela awekeze 50% ili matapeli wakae pembeni
 
Nashangaa timu imetulia chini ya Manji majitu hayaishi chokochoko. Watu wa Dar hawapendi utulivu
 
Napendekeza Manji aendelee kuwa Mwenyekiti wetu.
Tofauti na hapo Club itaanza kuyumba tena.
Sijaona ubaya wa uongozi wa Manji kabisa.
 
Ndugu zangu hata TFF humu wamepotea

kwani kuna aliyekataa uchaguzi wanasema wanaitaji muda baada ya ligi sio kuchanganya na sio kwa shinikizo la bmt kinyume na katiba ya yanga lzma ufanyike mkutano mkuu wa wananchama wa mapato na matumizi na pia kujadili tarehe ya uchaguzi mkuu kwa mujibu wa katiba ya yanga uchaguzi ni ajenda hvyonhyo ajenda inajadiliwa wapi kama sio na wanachama katka mkutano pia wanachama waunde kamati yao ya uchaguzi chini ya baraza la wadhamini wa klabu
 
Nashangaa timu imetulia chini ya Manji majitu hayaishi chokochoko. Watu wa Dar hawapendi utulivu
Sana yaani yanga inafanya vizuri,tayari majungu eti uchaguzi ufanyike,mbaya sana.Hao hao washabiki wa arsenal mbona hawamuondoi Wenger!
 
Back
Top Bottom