Yanga muiache simba ipumue

Yanga muiache simba ipumue

PhD

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2009
Posts
4,835
Reaction score
4,240
kama wale wazanzibari wanavyoomba waachwe wapumue, na mimi nawaomba yanga na uongozi wao waiache simba ipumueee, wametengeneza mgogoro wa wachezaji na pia wanazipanga timu zinazokutana na simba zinakaza sana, jamani yanga iacheni simba ipumue.
 
i hate manji. ana mbinu chafu na za kitoto. even mr 'nyingi' hates him
 
Ugonjwa ni WENU nyie SIMBA Mnabagua Wachezaji... Soma CHINI !!! ACHENI KUILAUMU YANGA

Na Mwandishi maalum
Nongwa na mgomo baridi unaofanywa na wachezaji wazalendo wa Simba inatokana na uwiano usio sawa wa mishahara baina yao na wachezaji wageni, kiasi hata timu hiyo kuboronga katika mechi zake za ligi kuu ya Tanzania Bara.

Uchunguzi umebaini kuwa, baadhi ya wanasoka wazalendo hawafurahii wenzao wa kigeni kulipwa mishahara minono wakati mchango wao katika timu ni mdogo.

Uchunguzi huo umegundua kuwa, hali hiyo imewafanya wachezaji hao wacheze chini ya kiwango kwa lengo la kuushinikiza uongozi kuweka uwiano mzuri wa mishahara.

Mchezaji mmoja mwandamizi wa timu hiyo, alitoa mfano wa wachezaji kama Komabil Keita na Paschal Ochieng, ambao alidai wanalipwa mshahara wa shilingi milioni 1.5 kwa mwezi, lakini wamecheza idadi ndogo ya mechi hadi sasa.

Mchezaji huyo alisema kuwa, viwango vya mishahara kwa wachezaji wazalendo ni kati ya shilingi laki tano na milioni moja wakati kiwango cha juu kwa wanasoka wageni ni shilingi milioni tatu. Felix Sunzu, raia wa Zambia ndiye mchezaji ghali kuliko wote katika klabu ya Simba akiwa analipwa mshahara wa shilingi milioni tatu wakati Mganda Emmanuel Okwi naye amekuwa akishinikiza kuongezwa mshahara katika mkataba wake mpya.

Kwa sasa, Okwi anaramba shilingi milioni 1.5. Wachezaji, ambao wamekuwa wakitajwa kulipwa kiwango kidogo cha mshahara wakati mchango wao ni mkubwa katika timu ni pamoja na Shomari Kapombe, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto na Nassor Masoud 'Cholo'. Mrisho Ngasa, ambaye amesajiliwa na Simba akitokea Azam, analipwa mshahara wa shilingi milioni mbili wakati Kapombe anakunja shilingi laki saba baada ya kupandishiwa hivi karibuni kutoka shilingi laki tano.

Kwa mujibu wa chanzo chetu hicho, mgomo huo ndio uliosababisha Simba ilazimishwe kutoka sare ya bao 1-1 na Polisi Morogoro kabla ya kuchapwa mabao 2-0 na Mtibwa Sugar, na juzi Jumamosi kulala kwa bao 1-0 dhidi ya Toto African katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam .

Alipoulizwa, kiongozi mmoja wa Simba alikiri kutambua kuwepo kwa mgomo huo na kuongeza kuwa, wanatarajia kukutana hivi karibuni kujadili hatua za kuwachukulia wachezaji wanaowashawishi wenzao kucheza chini ya kiwango.

Simba, ilianza ligi kuu kwa kishindo na ushindi wa mfululizo, lakini katika siku za hivi karibuni imekuwa ikidorora na kujikuta ikimaliza mzunguko wa kwanza ikishika nafasi ya tatu nyuma ya Azam na Yanga, na kuchafua rekodi yake kwa kupoteza michezo miwili, dhidi ya Mtibwa na Toto African.

SUNDAY, NOVEMBER 11, 2012 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG

i hate manji. ana mbinu chafu na za kitoto. even mr 'nyingi' hates him

alimwambia rage naomba timu hizi sasa zicheze soka, maharage akakubali gafla maharageakabadilika na kuendelea na michezo michafu manji akamwonyesha kua ye nitype nyingine sasa maharage hapumui
 
kama wale wazanzibari wanavyoomba waachwe wapumue, na mimi nawaomba yanga na uongozi wao waiache simba ipumueee, wametengeneza mgogoro wa wachezaji na pia wanazipanga timu zinazokutana na simba zinakaza sana, jamani yanga iacheni simba ipumue.

UUm kweli jamani watu wanakosana na wake zao sababu ya simba kufungwa kila siku, acheni wapumue jamani
 
Sasa kama hivi ndivyo soka la bongo lina raha gani? kama kweli wachezaji wanacheza chini ya kiwango eti kwasababu Manji kawahonga wafanye hivyo basi nadiriki kusema Manji hana akili wala hao wachezaji hawana akili, inawezekana vp ukazembea kufanya kazi inayokupa kula eti kwasababu umehongwa ili uzembee, upuuzi! na kama sababu ni kwamba ndani ya Simba wageni wanathaminiwa kwa upande wa malipo ni kwanini hao wachezaji wasikae chini na viongozi wao wakayamaliza kuliko kususa?

Mpira ni burudani, mpira ni kazi, tunalipa kuja kuangalia mpira tukijua mtatuburudisha na wakati huo nyinyi mupo kazini hatuji uwanjani kuja kuangalia mukicheza mpira kama wagonjwa.

TFF na vyama vyote vya mpira wa miguu pamoja na viongozi wa vilabu vya ligi kuu hembu kaeni chini mujadili mustakabali wa soka letu, kwa dhati kabisa na mujiulize TAIFA hili mumelifanyia nini katika medani ya Soka ulimwenguni, mukigundua hakuna mulichofanya basi tokeni muawaachie wengine.
 
pole sana ndugu ila ombi lako halikubaliki hata kidogo, kilichopo ni kukaza zaidi mpaka kitakapoeleweka. Daima mbele, nyuma mwiko.
 
Wakati wanaongoza ligi walikuwa wanamponda sana Manji leo hii kibao kimegeuka
 
pole sana ndugu ila ombi lako halikubaliki hata kidogo, kilichopo ni kukaza zaidi mpaka kitakapoeleweka. Daima mbele, nyuma mwiko.

...simba timu yenu inaongozwa na mwanasiasa,mla rushwa,mfungwa,mlopokaji,kwa hayo unafikiri kitatokea nini, jiangalie msitupe lawama kwa wapinzani wenu
 
Sasa kama hivi ndivyo soka la bongo lina raha gani? kama kweli wachezaji wanacheza chini ya kiwango eti kwasababu Manji kawahonga wafanye hivyo basi nadiriki kusema Manji hana akili wala hao wachezaji hawana akili, inawezekana vp ukazembea kufanya kazi inayokupa kula eti kwasababu umehongwa ili uzembee, upuuzi! na kama sababu ni kwamba ndani ya Simba wageni wanathaminiwa kwa upande wa malipo ni kwanini hao wachezaji wasikae chini na viongozi wao wakayamaliza kuliko kususa?

Mpira ni burudani, mpira ni kazi, tunalipa kuja kuangalia mpira tukijua mtatuburudisha na wakati huo nyinyi mupo kazini hatuji uwanjani kuja kuangalia mukicheza mpira kama wagonjwa.

TFF na vyama vyote vya mpira wa miguu pamoja na viongozi wa vilabu vya ligi kuu hembu kaeni chini mujadili mustakabali wa soka letu, kwa dhati kabisa na mujiulize TAIFA hili mumelifanyia nini katika medani ya Soka ulimwenguni, mukigundua hakuna mulichofanya basi tokeni muawaachie wengine.

Pole sana inaonyesha ww sio mdau wa soka maana hujui unachokiongea.YANGA OYEEEEE!!
 
kama wale wazanzibari wanavyoomba waachwe wapumue, na mimi nawaomba yanga na uongozi wao waiache simba ipumueee, wametengeneza mgogoro wa wachezaji na pia wanazipanga timu zinazokutana na simba zinakaza sana, jamani yanga iacheni simba ipumue.

Hao Wazanzibari hawajakuuzia maneno yao tu, bali hata akili zao.

Simba wamefungwa uwanjani ambako Yanga hakukuwepo mkuu. Jana tumejikaangia Cost of Onions kwa raha zetu, nyie mnatupigia kelele.
 
Pole sana inaonyesha ww sio mdau wa soka maana hujui unachokiongea.YANGA OYEEEEE!!

Ni kweli ndugu mimi sio mdau wa soka pengine kuliko wewe, lakini naamini sana katika ushindani na ndio raha ya soka timu ifungwe kwa kuzidiwa mchezo na sio matokeo yajulikane kabla hata ya mechi, nashukuru kama wewe ni mdau wa soka naomba uwapelekee kilio changu wadau wenzako kuwa tumezoea kununua mechi za ndani na kujiona tunajua mpira matokeo yake tukikutana na timu za nje tunafungwa na hatufiki popote maana hatuwezi kuwanunua hao wa nje.

Ni kweli YANGA OYEE hata mimi ni mshabiki wa YANGA ila nataka timu ninayoishabikia icheze soka la kisayansi na sio fitina,rushwa na uchawi.
 
Sasa kama hivi ndivyo soka la bongo lina raha gani? kama kweli wachezaji wanacheza chini ya kiwango eti kwasababu Manji kawahonga wafanye hivyo basi nadiriki kusema Manji hana akili wala hao wachezaji hawana akili, inawezekana vp ukazembea kufanya kazi inayokupa kula eti kwasababu umehongwa ili uzembee, upuuzi! na kama sababu ni kwamba ndani ya Simba wageni wanathaminiwa kwa upande wa malipo ni kwanini hao wachezaji wasikae chini na viongozi wao wakayamaliza kuliko kususa?

Mpira ni burudani, mpira ni kazi, tunalipa kuja kuangalia mpira tukijua mtatuburudisha na wakati huo nyinyi mupo kazini hatuji uwanjani kuja kuangalia mukicheza mpira kama wagonjwa.

TFF na vyama vyote vya mpira wa miguu pamoja na viongozi wa vilabu vya ligi kuu hembu kaeni chini mujadili mustakabali wa soka letu, kwa dhati kabisa na mujiulize TAIFA hili mumelifanyia nini katika medani ya Soka ulimwenguni, mukigundua hakuna mulichofanya basi tokeni muawaachie wengine.

Mbona povu mkuu?

Mara Manji mjinga, mara Manji sijui kitu gani mbona mnatapatapa? Matusi ya kumtukana mtu asiyehusika yanakujaje? Au wewe ndio umeamua kulikuza soka kwa maneno makali kwa mfadhili wetu?

Simba fanyeni mazoezi, mambo ya kumtafuta mchawi wala hayana tija. Timu zote zimejiandaa kushindana sasa kama mlitarajia ubwete sasa mmekumbana na mambo si mambo rudini mjipange, sio kutukana watu.

Y ang a Hoy eeeeeeeeeeeee!!!
 
Back
Top Bottom